Kenya kuchuana dhidi ya Inter Milan

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,667
Kenya kuchuana dhidi ya Inter Milan



Kenya kuchuana dhidi ya Inter Milan Nairobi
Kwa mara ya kwanza klabu mashuhuri duniani
Inter Milan ya Italia inazuru bara la Afrika.
Inter inatarajiwa kuwasili nchini Kenya kesho
kwa mechi yao ya kirafiki dhidi ya timu ya
taifa Harambee Stars Jumapili, kama
anavyotueleza mwaspoti wa BBC John Nene.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirikisho la
kandanda nchini Kenya Sam Nyamweya klabu
hiyo ya Italia Inter Milan inawasili Nairobi siku
ya Ijumaa na kisha ipambane na Harambee
Stars Jumapili kwenye mechi ya kimataifa ya
kirafiki kuanzia saa kumi za afrika mashariki.
Ziara ya Inter inatokana na ushirikiano mpya
kati ya shirikisho la kandanda nchini Kenya
na lile la Italia.
Wengine ambao wamechangia kwa ziara hiyo
ni wizara ya michezo, bodi ya utalii nchini
Kenya na wasimamizi wakuu wa uwanja wa
Kasarani.
Shirikisho la kandanda la Kenya hatahivyo
halijataja kikosi cha Inter kwa ziara hii lakini
wamesema mabingwa hao wa ligi ia Italia
serie A mara 18 watakua na wachezaji wake
wa kutegemewa.
Tayari mmoja wa nyota ya Inter MacDonald
Mariga wa Kenya yuko Nairobi akijiandaa kwa
mechi hiyo.
Kenya kuchuana dhidi ya Inter Milan
Mariga aliiwakilisha Harambee Stars wikendi
iliyopita kwenye mechi yao ya kufuzu kwa
finali ya mechi za kombe la Afrika dhidi ya
Comoros katika uwanja wa taifa wa Nyayo..
Inter ina mchezaji mmoja tu kwenye kikosi cha
timu ya Italia cha kombe la dunia nchini
Brazil, naye ni mlinzi Andrea Ranocchia aliye
kwenye idadi ya wachezaji 30 ambao
watapunguzwa hadi 24..
Haijulikani kama mshambuliaji matata wa
Inter Diego Milito yuko kwenye ziara ya Kenya
kwani tayari anaondoka Inter baada ya
kukitumikia klabu hicho kwa miaka mitano.
Mashabiki wengi hawatamsahau Milito
alipofunga mabao mawili yaliyoiwezesha Inter
kuicharaza Bayern Munich mabao 2-0 katika
mechi ya fainali ya kombe la mabingwa wa
ligi ya ulaya mwaka 2010.
Msimu uliopita Milito, mwenye umri wa miaka
34, hakuonyesha mchezo mzuri kutokana na
majeraha ambayo yamemsumbua kwa miaka
ya hivi karibuni.
Miongoni mwa wachezaji wengine
wanaoondoka ambao Milito alikua nao
wakishinda Bayern ni Javier Zanetti, Esteban
Cambiasso na Walter Samuel..
Inter pamoja na Manchester United ndizo timu
mbili ambazo zimeshinda kombe la mabingwa
wa ligi ya ulaya mara tatu.



bbc
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom