JohnShaaban
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 464
- 116
Kweli ni madudu hasa pale ECK walipoamua kutangaza matokeo licha ya baadi ya sehemu kuonyesha kura za Kibaki zimezidi hata idadi ya waliojiandikisha kupiga kura. Inasikitisha sana kwa EC kama hii, licha ya witnesses waliojitolea maisha yao kusema ukweli still wameamua kutangaza matokeo ya jumla na kumwapisha Rais usikuKwa vyovyote ilivyo, uchaguzi huu wa Kenya umekuwa na madudu mengi na ya dhahiri ambayo unaweza kufanya yaliyotokea Tanzania kuwa ni ya shule ya vidudu...
Mwkjj hapo umemgonga nyoka kichwani. Tukiweza kuchukua hatua kama hiyo nadhani tutapunguza kama sio kuondoa kabisa tatizo la wizi wa kula.Lakini hofu yangu ni kwamba umasikini wetu unaweza kuwa tatizo maana fisadi watagawana 'area of concentration' na kuhakikisha wanavuruga kila sehemu wanayoiona threat! BUT Still naiona ni good option for long run.Baada ya mikoa yote kutangaza matokeo yote, tume inatangaza mshindi.
Mweshimiwa Zitto
Tanzania inafurahisha sana wametuma wabunge kwenda kujifunza Rwanda mambo ya ICT.
ICT ya Rwanda imesimamiwa na Kagame mwenyewe wakati huohuo waliokuwa wanamfundisha Kagame ni wataalamu kutoka Tanzania.
Sasa ambacho sikielewi tunashindwaje kuwatumia hao wataalamu wetu sasa wamefundisha/wamesaidia Rwanda halafu tunaenda kujifunza huko?
kwa kifupi inakatisha tamaa, halafu watu wakilikita "ughaibuni" utasikia wanalalamika ati wamekimbia rudini home!!! kufanya nini kama mambo yenyewe ndio haya??aibu gani hii? sisiemu watatumia same playbook come 2010........kaaaazi kweli.
NAIROBI.Rais Mwai Kibaki ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa Kenya, baada ya kumshinda mpinzani wake Raila Odinga wa Chama cha ODM kwa zaidi ya kura laki mbili.
Lakini wakati tume ikitangaza matokeo hayo mjumbe mmoja katika tume ya uchaguzi nchini humo ametangaza kujitoa katika tume hiyo kwa kile alichodai kukataa kujihusisha na wizi wa kura.
Mjumbe huyo Kipkemoi Arap Kirui katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi uliyopita, amesema kuwa alikataa kutia saini katika fomu za matokeo ambazo ziligushiwa na kwamba imani yake haimtumi kuendelea akubaki ndani ya tume hiyo.
Mapema Mwenyekiti wa tume hiyo Samwel Kivuitu alitangaza matokeo baada ya kupitia upya fomu zilizowasilishwa, ambapo ilionesha kuwa Rais Mwai Kibaki alikuwa mbele kwa kura chache dhidi ya hasimu wa Raila Odinga.Katika matokeo ya awali Raila alikuwa mbele.
Uhesabuji kura ulisitishwa wakati ambapo tume ya uchaguzi nchini humo ikipitia upya baadhi ya matokeo.
Raila alikuwa akiongoza kwa wingi mkubwa wa kura dhidi ya Rais Kibaki. Lakini katika matokeo yaliyotangazwa jana na tume ya uchaguzi, mwanya wa kura hizo ulipungua ambapo Raila alikuwa mbele kwa kura elfu 38 dhidi ya Rais Kibaki.
Kuchelewa kutolewa kwa matokeo hayo kumepelekea ghasia ambapo inaarifiwa ya kwamba watu wanane wameuawa katika ghasia hizo.
Mapema vyama vyote viwili kile cha Rais Kibakai cha PNU na ODM vilidai kupata ushindi katika uchaguzi huo.
naomba nichukue fursa hii kumpongeza mwai kibaki,
nilijua hili na nasikitika sana nimeshindwa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.
watanzania wengi hawajui madhara ya ODINGA Kuwa rais ila wana usalama wanajua,jiulize kwanini FORD Walimnyima uenyekiti?
kibaki asante kwa kulinda maslahi ya afrika ya mashariki,
achana na hawa wanazi waliotaka kuipeleka eac kuwa kambi ya marekani na uk.
najua demokrasia haikufuatwa ila ni kheri PNU kuliko ole ODM
Its all out war, chaos and fires everywhere, gunshots, the lights are even gone. Tuombee
Watampiga risasi Kibaki.
Hiyo hapana, isitokee maana ni mbaya zaidi. Kumbuka huyu pia ana wanaomsapoti, kwa hiyo kutakuwa na kisasi kisichoisha. La maana watumie njia yoyote nyingine kumtoa lakini si mauaji. Wampinge kortini, bungeni, wafanye maandamano na yote, lakini mtu asijaribu mauaji, effect yake ni exponentially hazardous!
Je yawezekana kuwa katika hamasa yetu ya kutaka Raila ashinde tumeshindwa kuwa fair na kutaka aliyeshinda kihalali ashinde whoever that may be? Kuongoza toka mwanzo siyo sababu ya kujitangaza mshindi. Tatizo hilo ndilo lililowakuta CUF kwenye uchaguzi.
Nadhani sheria ya Kenya ni kama ya kwetu ambapo Tume ikishamtangaza Rais hakuna pa kukimbilia ni kusubiri miaka mitano. Je watu wa Raila hawakutumia kila "mbinu" ili mgombea wao ashinde na mbinu hizo zikaitwa "mkakati"?
Kwa vyovyote ilivyo, uchaguzi huu wa Kenya umekuwa na madudu mengi na ya dhahiri ambayo unaweza kufanya yaliyotokea Tanzania kuwa ni ya shule ya vidudu. Tunapoenda mbele jukumu kubwa ni kuona jinsi gani tunaweza kutengeneza mechanism ambayo itahakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa uhuru.
Binafsi naamini jambo moja ambalo lazima lifanyike mara moja Tanzania na hata baadaye Kenya ni kuwa mtindo wa kusubiri matokeo ya Urais yatangazwe kitaifa unachochea sana wizi na uvunjaji wa taratibu. Binafsi naamini kila mkoa/jimbo utangaze matokeo yake ya mkoa na hayo yanasimama. Tume ya Taifa jukumu lake ni kukusanya matokeo yote na kuyajumuisha. Hii ina maana ya kuwa badala ya vituo kutangaza halafu matokeo yaende tume ya Taifa ni vizuri matokeo yakitangazwa vituoni yanaenda ngazi za mkoa na kila mkoa unatangaza matokeo yake period.
Baada ya mikoa yote kutangaza matokeo yote, tume inatangaza mshindi.
nawaonea huruma sana wakikuyu maana wamezungukwa na makabila mengine wakiwemo wakalenjin. Soon watu watajutia walichofanya maana hiyo nchi haitatawalika kirahisi hivi.
DU!WENZANGU,
NASHUKURU KWA KUWA PAMOJA NASI KWA KIPINDI HIKI KIGUMU.
NAWAOMBENI RUHSA NIENDE NIKAOMBOLEZE NA NCHI YANGU, TUPANGUZANE MACHOZI KWA KITENDO CHA JINAI KIMECHOFANYIKA IKULU, NAIROBI. SITAKUWA HAPA KWA MUDA LAKINI MUISHI KWA AMANI NCHI YA MAMANGU, TANZANIA.
WAMEFUNGA VITUO VYOTE VYA UTANGAZAJI NA SASA NI KBC TU NDIO INA HATI ZA KUTANGAZA. NGOJENI MUONE DAMU SASA HASA YA WANAUPINZANI NA WALIOMPIGIA RAILA IKIANZA KUMWAGWA NA SERIKALI. KBC ITAWAAMBIA MAMBO SHWARI LAKINI WATAPONDA ANY RESISTANCE NA RISASI. TUMEKWISHA SISI, VIONGOZI WETU ODM WILL BE ARRESTED WITHOUT TRIAL AND THIS IS WHAT IT MEANS TO FIGHT FOR DEMOCRACY AND THE POOR.
WE ARE MEN, WE WILL DIE LIKE MEN.
KWAHERI YA KUONANA. NIKIFA VITANI HUKO KWENYE MAANDAMANO AMBAZO ZIMEANZA TAYARI MUSINISAHAU MOYONI MWENYU. NAWAPENDA NA NINA WAHESHIMU.
AHSANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI