getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wadau sina nia mbaya ya kwenda kinyume na taratibu za ibada. Lakini naomba kujuzwa hivi kuna utaratibu upi unapaswa na makanisa yaliyo jirani na makazi ya watu wanapoendesha ibada za mikesha kwa sauti kubwa za muziki na maombi! Nadhani kuna sheria ya utulivu wa jamii wanavunja. Naomba nisaidiwe ushauri ili hata nikichukua sheria nisije kengeuka! Niko jirani na kanisa la TAG kwa kweli kwa maombi haya ya ijumaa usiku. Ni kikwazo!!