KCMC waamua kuua sasa!

Jamani, acheni kulalamika ovyo. Katika hospitali zote za rufaa Tanzania, KCMC ndio hospitali pekee ambayo ilikuwa inacharge gharama ndogo. Matokeo yake wagonjwa wote wenye uwezo na wasio na uwezo wanaenda KCMC na hospitali inajikuta inahudumia wagonjwa wengi kuliko uwezo wake. Kwa nini serikali isiboreshe hospitali ya mawenzi at least ikasaidiana na KCMC? Hapana, yenyewe imekaa tu. Imefunga THEATRE ya mawenzi tangu 2010 kisa haina ubora sasa wewe kitu kikiwa hakina ubora unakifunga au unakiboresha? Matokeo yake wagonjwa hata wanaohitaji operation, hata iwe ndogo kiasi gani wanapelekwa KCMC wakati mawenzi ipo, sasa yenyewe itajiendeshaje? Halafu bila AIBU mmeandika ma-thread mengine juzi juzi tu kuwa Hospitali ya KCMC haina huduma nzuri, wagonjwa wamerundikana mawodini na hakuna huduma bora, watawahudumiaje wakati wagonjwa wanazidi wahudumu wa hospitali? Acheni unafiki, kabla hamjaanza kulaumu watu, tumieni akili. Halafu msianze kujidai wasio na uwezo watakufa, tangu lini ukaenda hospitali ya KCMC bila hela na unaumwa sana wakakurudisha nyumbani? Na mimi ni shahidi, jirani yangu alifanyiwa operation ya tumbo vizuri kabisa na walipogundua kuwa ni kweli hana uwezo wa kulipa wakampa expemption.
 
Niwashukuru sana wote walioguswa na hili la gharama za KCMC. Hatimaye gharama zimerejea za awali kama mwanzo. Niishukuru serekali kwa kuliona hilo. Hii mifuko ya bima ya afya ya jamii ni janga lingine la Taifa.
 
Back
Top Bottom