KC Zitto Kabwe aibua Mazito kutimuliwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura

ACT Wazalendo

Verified Member
May 5, 2014
478
1,000
Hili la Mkurugenzi Mkuu wa EWURA linahusu tangazo la leseni ya Kampuni ya kifisadi ya IPTL?

Zitto Kabwe, Mb

Ni muhimu sana Rais afahamu kwamba kuna kazi kubwa ya chinichini inafanywa na wasaidizi wake ( sina hakika kama yeye Rais anajua na au ameruhusu kazi hiyo ) kuendeleza wizi huu wa watu wa PAP ya Harbinder Singh Seth na IPTL. Kwenye kesi ya Standard Chartered Bank dhidi ya TANESCO huko mahakama ya ICSID ambapo TANESCO wanatakiwa kulipa shilingi 352 bilioni kwa Benki hiyo, Wanasheria wa TANESCO na wale wa PAP/IPTL wanashirikiana kwa karibu mno. Kwenye rufaa, TANESCO wametakiwa waweke fedha hizo kwanza kwenye akaunti ya Benki ya nje kabla ya rufaa kusikilizwa.
PAP/IPTL wanalinda ufisadi wao kwa kujifanya wanashirikiana na TANESCO kwenye kesi. Kwenye Taarifa ya PAC kuhusu Tegeta Escrow Account, tuliweka wazi kuwa PAP/IPTL waliweka dhamana kuwa ikitokea madai yeyote yale dhidi ya TANESCO basi PAP/IPTL italipa.

Madai yametokea, matapeli hawa wanajifanya kushirikiana na Shirika letu na Wanasheria wa Serikali wanawasaidia matapeli hawa na sasa wanataka kuwaongezea leseni ya Biashara. Kwanini Serikali isitumie ile Indemnity kuwataka PAP kulipa hizi fedha? Kwanini Serikali inayosema inapambana na ufisadi inawakumbatia mafisadi wa PAP/IPTL? Kwanini Serikali iliyoonyesha ujasiri wa kupambana na Kampuni kubwa kama Acacia/Barrick inayumbishwa na matapeli hawa? Tena tapeli mmoja tu Harbinder Singh Seth?

Vyombo vya Serikali pia vinahusika na kuwalinda hawa matapeli. Kwa mfano, huko ICSID Shirika letu la TANESCO kupitia wanasheria wake wamepeleka hoja kwamba Maazimio ya Bunge kuhusu Tegeta Escrow hayana msingi wowote wa kisheria na kwamba Bunge linapiga porojo tu. Wanasheria hawa wameomba Ofisi ya Bunge iwape barua kuthibitisha kuwa Maamuzi ya bunge hayana msingi wowote na ni maoni tu yanaweza kudharauliwa na kutupiliwa mbali. Shirika la Umma linalosimamiwa na Bunge linapeleka barua kwenye vyombo vya kibeberu kuwa Bunge porojo tupu.

Pia kwa kudanganywa na PAP/IPTL, TANESCO wamepeleka madai kuwa PAC ilihongwa kufikia maamuzi yaliyofikiwa na Bunge. Wametengeneza barua pepe za kujaribu kushawishi madai yao hayo na hata Taasisi muhimu kama PCCB waliingia kwenye mkenge huo na kuniita kunihoji. Niliwapa ushirikiano wote na kuwapa simu na computer zangu wachunguze barua pepe zile za kuchonga wakakuta hakuna lolote. Sikuwaacha, niliwaambia kuwa wao ni mawakala wa mashetani. Wanashirikiana na matapeli kuwaibia Watanzania. Idara ya Usalama wa Taifa, inahusika moja kwa moja na kazi hii inayofanywa na PAP/IPTL ili kufanikisha mradi huu wa kitapeli. Sina hakika kama Rais aliidhinisha haya maana TISS na PCCB wanawajibika kwa Rais moja kwa moja.

Hivyo, inawezekana kabisa mpango wa kuongeza leseni ya IPTL akawajibishwa mtu wa EWURA kwa sababu ndiye alitoa tangazo la leseni, lakini huyo mtu wa EWURA anaweza kuwa ameshinikizwa na watu wa Usalama wa Taifa kufanya hivyo. Mimi naamini Rais, kwa jinsi alivyo, hawezi kuwa anahusika na haya matapeli, lakini Rais mtumbuaji anakaaje miezi 20 kwenye Kiti za Enzi bila kumaliza suala la IPTL ilhali kuna Maazimio ya Bunge yanayopaswa kutekelezwa?

Nawapa kazi ndogo Watanzania, tazameni lile Tangazo la EWURA kuhusu IPTL nililowawekea hapa siku limetoka. Tazameni umiliki na wamiliki wa IPTL hivi sasa. Kuna hisa 16% kwa kampuni mbili zenye majina ya ujanja ujanja. Kina nani hao wamegawiwa hizo hisa tena wakati wa Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,784
2,000
Mkuu, mjitahidi pia pamoja na kuripoti matukio (jambo ambalo ni zuri) muwe na innovations!

Jitahidini kuanzisha mijadala ya hoja inayofikirisha. Aidha, msimuachie kiongozi wa chama peke yake ndio awe anaibua hoja kila siku. Wengine mbona hamuanzishi hoja ?

Kukosoa wengine kosoeni, ila fanyeni zaidi ya hapo. Kama chama kuweni wabunifu, fanyeni mambo ambayo ni unique! Hayajawai kufanywa kwenye nchi hii.

Kukosoa tu haitoshi, kukosoa ni kazi rahisi isiyohitaji kutumia akili nyingi na kila mtu anaweza kuifanya. Tunataka tuone kama chama mna innovate nini?. Tunataka tuone humo kuna watu wengi wanajenga hoja madhubuti kila mara na sio kumuachia zito tu.Kuweni wabunifu. Kuongeza ufanisi, ombeni ushauri kwa jamii kwamba mfanye nini ili kuwa chama bora kuliko vyama vingine.Halafu pale mnapokwama, msione aibu kujishusha ili mpate support. Jikubalini mlivyo pamoja na udhaifu wenu na uimara wenu.

Kwa sasa ACT bado ni changa mno, wekezeni nguvu kwenye kujenga competent human resources kwenye chama. Andaeni viongozi bora na hakikisheni wanakuwa motivated. Msisubirie kugombea from no where na ishu nyingine kama hizo. Msimtegemee zitto peke yake, ninyi ni chama.
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,548
2,000
zitto nimeielewa concern yake lakini ukweli ni kwamba alishasema hafukui makaburi...halafu hajui kwa nini maazimio ya bunge yandharauliwa,hajiulizi kwenye maazimio ya yule tapeli mwakyembe mangapi yalitekelezwa?
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,809
2,000
Haya Maccm yameamua kuingia mikataba ya kiraghai ili yapate fedha za uchaguzi 2020, hivyo kuyashauri ni kupigia mbuzi jitaa. Hivi wanasheria wa nchii wanaohitwa wakili wasomi, hivi wanasoma vitabu tofauti vya sheria. au wanatumia vilivyotungwa hapa hapa ndio maana wanayumbishwa? au Nyoka wa Makengeza ashafanya yake maana alikuwa mshauri wa kampuni hii. au alishauri njia za kiwizi wizi.
 
kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,935
2,000
Toka zito alivyoanza kupepea pepea kama bendera kwenye hoja za msingi siku za karibuni huwa siamini sana maandiko yake. Ila kama alichoandika hapa ni sahihi basi vizuri, kidogo amejielewa kwa leo
 
Rubajirwa

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
474
250
Mkuu, mjitahidi pia pamoja na kuripoti matukio (jambo ambalo ni zuri) muwe na innovations!

Jitahidini kuanzisha mijadala ya hoja inayofikirisha. Aidha, msimuachie kiongozi wa chama peke yake ndio awe anaibua hoja kila siku. Wengine mbona hamuanzishi hoja ?

Kukosoa wengine kosoeni, ila fanyeni zaidi ya hapo. Kama chama kuweni wabunifu, fanyeni mambo ambayo ni unique! Hayajawai kufanywa kwenye nchi hii.

Kukosoa tu haitoshi, kukosoa ni kazi rahisi isiyohitaji kutumia akili nyingi na kila mtu anaweza kuifanya. Tunataka tuone kama chama mna innovate nini?. Tunataka tuone humo kuna watu wengi wanajenga hoja madhubuti kila mara na sio kumuachia zito tu.Kuweni wabunifu. Kuongeza ufanisi, ombeni ushauri kwa jamii kwamba mfanye nini ili kuwa chama bora kuliko vyama vingine.Halafu pale mnapokwama, msione aibu kujishusha ili mpate support. Jikubalini mlivyo pamoja na udhaifu wenu na uimara wenu.

Kwa sasa ACT bado ni changa mno, wekezeni nguvu kwenye kujenga competent human resources kwenye chama. Andaeni viongozi bora na hakikisheni wanakuwa motivated. Msisubirie kugombea from no where na ishu nyingine kama hizo. Msimtegemee zitto peke yake, ninyi ni chama.
Well said
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom