KC Zitto Kabwe aibua Mazito kutimuliwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura

Lissu wapi, CHADEMA wapi kupeleka serikali mahakani kwa kumfukuza kazi huyu CEO!!!

Lazima sheria zifuatwe.
 
zito na act sijui kama watawasikiliza naona wako bize wanaandaa sherehe ya uzinduzi wa ripoti ya pili ya madini.

hebu tuone hiki kitendawili kingine Huyo wanayemuita mzalendo no 1 atakitengua vipi?

inaonekana kama vile hili LA IPTL linataka kutibua sherehe ya j3
 
IPTL ni kisiki,hadi leo ni ngumu kujua kwanini tokea IPTL ije Tanzania imetetewa na kila serikali iliopo madarakani.
Mh Zitto IPTL ni mfupa uliomshinda fisi.
 
Hili la Mkurugenzi Mkuu wa EWURA linahusu tangazo la leseni ya Kampuni ya kifisadi ya IPTL?

Zitto Kabwe, Mb

Ni muhimu sana Rais afahamu kwamba kuna kazi kubwa ya chinichini inafanywa na wasaidizi wake ( sina hakika kama yeye Rais anajua na au ameruhusu kazi hiyo ) kuendeleza wizi huu wa watu wa PAP ya Harbinder Singh Seth na IPTL. Kwenye kesi ya Standard Chartered Bank dhidi ya TANESCO huko mahakama ya ICSID ambapo TANESCO wanatakiwa kulipa shilingi 352 bilioni kwa Benki hiyo, Wanasheria wa TANESCO na wale wa PAP/IPTL wanashirikiana kwa karibu mno. Kwenye rufaa, TANESCO wametakiwa waweke fedha hizo kwanza kwenye akaunti ya Benki ya nje kabla ya rufaa kusikilizwa.
PAP/IPTL wanalinda ufisadi wao kwa kujifanya wanashirikiana na TANESCO kwenye kesi. Kwenye Taarifa ya PAC kuhusu Tegeta Escrow Account, tuliweka wazi kuwa PAP/IPTL waliweka dhamana kuwa ikitokea madai yeyote yale dhidi ya TANESCO basi PAP/IPTL italipa. Madai yametokea, matapeli hawa wanajifanya kushirikiana na Shirika letu na Wanasheria wa Serikali wanawasaidia matapeli hawa na sasa wanataka kuwaongezea leseni ya Biashara. Kwanini Serikali isitumie ile Indemnity kuwataka PAP kulipa hizi fedha? Kwanini Serikali inayosema inapambana na ufisadi inawakumbatia mafisadi wa PAP/IPTL? Kwanini Serikali iliyoonyesha ujasiri wa kupambana na Kampuni kubwa kama Acacia/Barrick inayumbishwa na matapeli hawa? Tena tapeli mmoja tu Harbinder Singh Seth?

Vyombo vya Serikali pia vinahusika na kuwalinda hawa matapeli. Kwa mfano, huko ICSID Shirika letu la TANESCO kupitia wanasheria wake wamepeleka hoja kwamba Maazimio ya Bunge kuhusu Tegeta Escrow hayana msingi wowote wa kisheria na kwamba Bunge linapiga porojo tu. Wanasheria hawa wameomba Ofisi ya Bunge iwape barua kuthibitisha kuwa Maamuzi ya bunge hayana msingi wowote na ni maoni tu yanaweza kudharauliwa na kutupiliwa mbali. Shirika la Umma linalosimamiwa na Bunge linapeleka barua kwenye vyombo vya kibeberu kuwa Bunge porojo tupu.

Pia kwa kudanganywa na PAP/IPTL, TANESCO wamepeleka madai kuwa PAC ilihongwa kufikia maamuzi yaliyofikiwa na Bunge. Wametengeneza barua pepe za kujaribu kushawishi madai yao hayo na hata Taasisi muhimu kama PCCB waliingia kwenye mkenge huo na kuniita kunihoji. Niliwapa ushirikiano wote na kuwapa simu na computer zangu wachunguze barua pepe zile za kuchonga wakakuta hakuna lolote. Sikuwaacha, niliwaambia kuwa wao ni mawakala wa mashetani. Wanashirikiana na matapeli kuwaibia Watanzania. Idara ya Usalama wa Taifa, inahusika moja kwa moja na kazi hii inayofanywa na PAP/IPTL ili kufanikisha mradi huu wa kitapeli. Sina hakika kama Rais aliidhinisha haya maana TISS na PCCB wanawajibika kwa Rais moja kwa moja.

Hivyo, inawezekana kabisa mpango wa kuongeza leseni ya IPTL akawajibishwa mtu wa EWURA kwa sababu ndiye alitoa tangazo la leseni, lakini huyo mtu wa EWURA anaweza kuwa ameshinikizwa na watu wa Usalama wa Taifa kufanya hivyo. Mimi naamini Rais, kwa jinsi alivyo, hawezi kuwa anahusika na haya matapeli, lakini Rais mtumbuaji anakaaje miezi 20 kwenye Kiti za Enzi bila kumaliza suala la IPTL ilhali kuna Maazimio ya Bunge yanayopaswa kutekelezwa?

Nawapa kazi ndogo Watanzania, tazameni lile Tangazo la EWURA kuhusu IPTL nililowawekea hapa siku limetoka. Tazameni umiliki na wamiliki wa IPTL hivi sasa. Kuna hisa 16% kwa kampuni mbili zenye majina ya ujanja ujanja. Kina nani hao wamegawiwa hizo hisa tena wakati wa Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.
Mh Zitto, watanzania wanakujua hasa utetezi wako wa kulinda mali za umma, ila kuna muda unageukaga, una sura mbili, isingekuwa hivyo ningemwambia Rais ukupe cheo kikuu cha madini kilicho wazi, naogopa, sababu huaminiki.
 
Haya Maccm yameamua kuingia mikataba ya kiraghai ili yapate fedha za uchaguzi 2020, hivyo kuyashauri ni kupigia mbuzi jitaa. Hivi wanasheria wa nchii wanaohitwa wakili wasomi, hivi wanasoma vitabu tofauti vya sheria. au wanatumia vilivyotungwa hapa hapa ndio maana wanayumbishwa? au Nyoka wa Makengeza ashafanya yake maana alikuwa mshauri wa kampuni hii. au alishauri njia za kiwizi wizi.
Unachoongea kina mashiko.
Haiwezekani mtu akafukuzwa au kusimamishwa kazi kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu za kazi. Hapa lipo jambo. Kibaya zaidi huwa hatutangaziwi makosa ya mkosaji. Isije ikawa amefukuzwa kwa kuvujisha siri ya uongezaji wa mkataba!
Kuna kampuni mbili zimeongezwa kwenye ubia wa IPTL yaani Euroasia Holdings Limited na Hi-Tide Trade Limited Hapa kinachotakiwa ni kuchunguza ni nani walioongezwa kwenye hizo share za IPTL?

upload_2017-6-11_11-59-50.jpeg
 
Hili la Mkurugenzi Mkuu wa EWURA linahusu tangazo la leseni ya Kampuni ya kifisadi ya IPTL?

Zitto Kabwe, Mb

Ni muhimu sana Rais afahamu kwamba kuna kazi kubwa ya chinichini inafanywa na wasaidizi wake ( sina hakika kama yeye Rais anajua na au ameruhusu kazi hiyo ) kuendeleza wizi huu wa watu wa PAP ya Harbinder Singh Seth na IPTL. Kwenye kesi ya Standard Chartered Bank dhidi ya TANESCO huko mahakama ya ICSID ambapo TANESCO wanatakiwa kulipa shilingi 352 bilioni kwa Benki hiyo, Wanasheria wa TANESCO na wale wa PAP/IPTL wanashirikiana kwa karibu mno. Kwenye rufaa, TANESCO wametakiwa waweke fedha hizo kwanza kwenye akaunti ya Benki ya nje kabla ya rufaa kusikilizwa.
PAP/IPTL wanalinda ufisadi wao kwa kujifanya wanashirikiana na TANESCO kwenye kesi. Kwenye Taarifa ya PAC kuhusu Tegeta Escrow Account, tuliweka wazi kuwa PAP/IPTL waliweka dhamana kuwa ikitokea madai yeyote yale dhidi ya TANESCO basi PAP/IPTL italipa. Madai yametokea, matapeli hawa wanajifanya kushirikiana na Shirika letu na Wanasheria wa Serikali wanawasaidia matapeli hawa na sasa wanataka kuwaongezea leseni ya Biashara. Kwanini Serikali isitumie ile Indemnity kuwataka PAP kulipa hizi fedha? Kwanini Serikali inayosema inapambana na ufisadi inawakumbatia mafisadi wa PAP/IPTL? Kwanini Serikali iliyoonyesha ujasiri wa kupambana na Kampuni kubwa kama Acacia/Barrick inayumbishwa na matapeli hawa? Tena tapeli mmoja tu Harbinder Singh Seth?

Vyombo vya Serikali pia vinahusika na kuwalinda hawa matapeli. Kwa mfano, huko ICSID Shirika letu la TANESCO kupitia wanasheria wake wamepeleka hoja kwamba Maazimio ya Bunge kuhusu Tegeta Escrow hayana msingi wowote wa kisheria na kwamba Bunge linapiga porojo tu. Wanasheria hawa wameomba Ofisi ya Bunge iwape barua kuthibitisha kuwa Maamuzi ya bunge hayana msingi wowote na ni maoni tu yanaweza kudharauliwa na kutupiliwa mbali. Shirika la Umma linalosimamiwa na Bunge linapeleka barua kwenye vyombo vya kibeberu kuwa Bunge porojo tupu.

Pia kwa kudanganywa na PAP/IPTL, TANESCO wamepeleka madai kuwa PAC ilihongwa kufikia maamuzi yaliyofikiwa na Bunge. Wametengeneza barua pepe za kujaribu kushawishi madai yao hayo na hata Taasisi muhimu kama PCCB waliingia kwenye mkenge huo na kuniita kunihoji. Niliwapa ushirikiano wote na kuwapa simu na computer zangu wachunguze barua pepe zile za kuchonga wakakuta hakuna lolote. Sikuwaacha, niliwaambia kuwa wao ni mawakala wa mashetani. Wanashirikiana na matapeli kuwaibia Watanzania. Idara ya Usalama wa Taifa, inahusika moja kwa moja na kazi hii inayofanywa na PAP/IPTL ili kufanikisha mradi huu wa kitapeli. Sina hakika kama Rais aliidhinisha haya maana TISS na PCCB wanawajibika kwa Rais moja kwa moja.

Hivyo, inawezekana kabisa mpango wa kuongeza leseni ya IPTL akawajibishwa mtu wa EWURA kwa sababu ndiye alitoa tangazo la leseni, lakini huyo mtu wa EWURA anaweza kuwa ameshinikizwa na watu wa Usalama wa Taifa kufanya hivyo. Mimi naamini Rais, kwa jinsi alivyo, hawezi kuwa anahusika na haya matapeli, lakini Rais mtumbuaji anakaaje miezi 20 kwenye Kiti za Enzi bila kumaliza suala la IPTL ilhali kuna Maazimio ya Bunge yanayopaswa kutekelezwa?

Nawapa kazi ndogo Watanzania, tazameni lile Tangazo la EWURA kuhusu IPTL nililowawekea hapa siku limetoka. Tazameni umiliki na wamiliki wa IPTL hivi sasa. Kuna hisa 16% kwa kampuni mbili zenye majina ya ujanja ujanja. Kina nani hao wamegawiwa hizo hisa tena wakati wa Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli.

Niko against na zito lakini kwa hili namuunga mkono asilimia 100%
 
Lissu wapi, CHADEMA wapi kupeleka serikali mahakani kwa kumfukuza kazi huyu CEO!!!

Lazima sheria zifuatwe.

Tatizo lako akili yako imejikita kwa Lissu na Chadema siyo nje ya hapo. Wenye akili wanajiukiza kwanini afukuzwe kazi masaa machache baada ya Tangazo la EWURA?Nini kimejificha.Mawili either tuamua kufukua makaburi yote bila kuangalia sura au cheo cha MTU, vinginevyo hao wanaofukuzwa ni Mbuzi wa Kafara tu.
 
Kumbe usalama wa Taifa wanaomzunguka Rais wanashirikiana na matapeli? Ndio maana sijawahi na sitaiamini CCM milele na milele
 
Zidumu fikra za mwenyekiti...!! Tumesha apa ..!! Hata musemeje hatuelewi somo ss ndio ccm bana na mwaka huu mtaisoma namba
 
Back
Top Bottom