Shamkware
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 1,755
- 2,303
Pande zote nchi nzima tumekuwa tukisumbuka juu ya hili janga la ajira nchini! Kiukweli kabisa hili ni tatizo kubwa na wahanga wa hili tatizo ni wengi sana! Lakini tumekuwa tukisema kazi hazipo! Mi nasema kazi zipo ila ajira ndo hakuna! Tusimameni imara kuwaza mbali na kufanya kazi binafsi! Zipo nyingi kazi sema sisi tunataka ajira! Kwa mfano!. Mnaweza kujikusanya hata vijana watano mkachanga kila mtu hata laki moja mkatafuta sehemu nzuri mkalipia na mkafungua hata "tution center" Walimu ni nyinyi wenyewe mnagawana vipindi tu hii itawaweka busy na hamtakosa wanafunzi wa kufundisha mwisho wa siku mradi unajiendesha wenyewe na mtapata hela,.. Kitu kingine kilimo watu wanaamini kilimo ni shughuli ya mwisho ktk utafutaji but mi nasema no! Kwa mfano pale Morogoro kuna vijana walijiunga kama watano baada ya kumaliza masomo yao pale SUA hawa jamaa walijichanga changa wakakodi mashamba mahali wakalima tikiti maji walitoka vizuri na walipata hela nyingi sana mpaka leo hivi ni wakulima wazuri na wana hela mbaya na walishanunua mpaka zana za kilimo hiyo ni kazi yao wenyewe na mkishakuwa hivo ni rahisi kupata mkopo! Hata kufuga nyuki jamani? Tusiwaze tu kununua magari haraka haraka na kuwa mameneja kwenye maofisi ya viyoyozi hali mbaya jamani huku mitaani wasomi ndo wezi huku na matapeli makubwa wadada nao kubadilisha midume tu inajisifu mno kuwapanda wadada wasomi yaani tunaibika jamani ajira hizi daaah! Mungu atusaidie tu! "But we belief one day yes"