Kazi za Bunge ni zipi katika kulisaidia Taifa kupiga hatua zaidi?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Moja ya matumizi makubwa ya serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ni kuliendesha Bunge. Suna uhakika mpaka sasa Bunge letu lina wabunge wangapi lakini hawapungui 370.

Ni miongoni mwa wabunge hao wa kuchaguliwa majimboni, wa kuteuliwa na rais na wale wa viti maalum rais huunda serikali yake.
Kwa mijibu wa katiba yetu kazi mbili kuu za Bunge ni 1. Kutunga sheria za nchi. 2. Ni kushauri serikali katika mambo yote yanayohusu nchi.

Lakini nini maana ya kutunga sheria? Ni kile kitendo cha kusomewa miswada mara kadhaa kisha Bunge kukaa kama kamati na kuridhia sheria hiyo kupita pamoja na marekebisho yake?

Nauliza hivyo kwa sababu kuna wakati sheria zinatungwa bungeni lakini zikifika kwa umma reaction yake inakuwa kunwa kiasi cha kujiuliza ni kweli bunge kutoka na umma kwa maana ya uwakilishi?

Na vipi kama serikali ina jambo lake na inataka kulipitisha huku bunge likiwa halitaki nini Kitatokea?

Sheria ya juzi ya miamala ya fedha ya simu imeonyesha hilo.

Nini kazi ya bunge pale kiongozi kama Rais, VP na PM wanapotoa fedha hadharani ya kifanikisha mradi flani bila ridhaa ya bunge nini wajibu wa bunge kwenye hilo?

Nini kinaweza kutokea kama bunge halitakuwepo kwa muda kadhaa na serikali ikabaki inadanya kazi bila bunge?

Je, wabunge wa chama tawala wana nafasi gani katika kuikosoa serikali yw chama chao.

Je, chama huwa kinawasikiliza wabunge watokanao na chama hicho kuikosoa serikali inapofanya vibaya?

Kuna sehemu mara nyingine kama taifa huwa tunapoteza fedha nyingi sana kwa mambo ambayo hayana faida kwa umma
 
12,000,000 × 400 = Hiyo kwa mwezi wakiwa majimboni.
Ikiwa wapi bungeni kila mbunge karibia 26M analipwa.
 
Back
Top Bottom