Elections 2010 Kazi ya Vyombo Vya Habari ni nini?Kuelimisha,kujenga,kubomoa au kutumika na wachache

Kagemro

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
1,432
631
Ndugu wana Jf,

Nijambo la kujsikitisha kwa vyombo vyetu vya habari hapa Tanzania.Sijui niseme ni Vyombo vya habari au ni watu wenye taaluma zao.

taaluma hii inaelekea kupoteza mshiko kwakuwa haitumiki ipasavyo hapa Tanzania.
waandishi wengi wamekuwa wakiaandika habari kwa kuwafurahisha watu na si kuihabarisha jamii.Mambo haya tumeyaona wakati wa uchaguzi,na hata vyombo vilivyosimama na kuelimisha jamii vilitishiwa eti vitafungiwa kwa kuwa vinaandika uchochezi.

ndani ya wiki hii nimegundua kitu kipya na natumaini kitaendelea kujidhihirisha dhahiri,vyombo vya habari vimeshikilia swala la wabunge wa Chadema.

walk out ya wa bunge wa chadema si kitu kigeni hapa duniani kwa watu wanaofatilia taarifa mbalimbali za nje watakuwa wamekutana na haya,hata juzi kimetokea kwa wabunge wa urusi.

ni wajibu wa Vyombo vya habari kuielimisha jamii nini maana yake na si kupotosha watanzania ambao wamechoshwa na maisha ya kidhalimu.Tumekuwa tukiambiwa vyombo vya habari wahariri wake wananunuliwa na kupotosha ukweli juu ya taarifa mbalimbali za nchi hii,je tutafika?

kama watu wanashindwa kutumia taaluma zao kwa manufaa ya wengi Taifa letu linakwenda wapi?
tutashuhudia wiki hii jinsi vyombo vingi vitakapokuwa vinatoa taarifa zisizo sahii kama Nipashe ya leo ilimradi tu kuvuruga ukweli na si kujenga.

Wito wangu kwa waandishi wa habari tumieni taaluma zenu vizuri vinginevyo Tumechoka kusoma uwozo na uwongo.

Wala msitake kututoa katika ajenda,swala ni Tunadai mabadiliko Tanzania,Matokeo hayakutangazwa au kutolewa kwa njia iliyo wazi,Tunadai tume huru.waelimisheni watanzania ni kwanini Rais hatambuliki na si vinginevyo.

Ninyi ndiyo mtakao vuruga Amani ya nchi hii kama mtashindwa kutoa uwiano wa taarifa,kwani si kila mtu haelewi,na kwakuwa tumechoshwa na serikali inayoongozwa remotly sasa tutapambana.

zipo taarifa zimeenea kuwa vyombo vimenunuliwa nikimaanisha wahariri na wenye vyombo ili kugeuza ajenda ya Uchaguzi iliyokuwa inaendelea na kuweka ajenda ya wabunge wa Chadema,hata vile vinavyofanya vizuri wanapewa vitisho.

wananchi tumechoka sasa tunahitaji taarifa zenye maono ya kututoa hapa tulipo na kutupeleka mahali ambapo tutapumua.

SASA KAMA HIKI KITAENDELEA WENGI WETU TUTAFATILIA UKWELI HUU NDIPO MTAKAPO JUA WAPO WATANZANIA TUNAOELEWA NA KWAKUWA TUNAELEWA TUTATHUBUTU.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom