Kazi ya uteuzi ibaki kuwa Rais Ila nafasi ziombwe kupitia TAMISEMI

Mar 12, 2019
28
20
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri.

Baada ya siku chache kupita kwa mh Rais Samia Suluhu Hasani kufanya uteuzi wa waheshimiwa wakuu wa wilaya kadhaa nchini ambapo kwa asilimia kubwa ya wateuliwa wamesharipoti vituo vyao vya kazi na wengine tunasikia wamegomea uteuzi huo.

Kwanza niwapongeze wale walio ripoti pia na Hawa ambao wameshindwa kuripoti pia niwape pongezi kwa ujasiri wao huo kwa kuwa Kama binadamu lazima utambue kwenye maisha tumekuja kufanya nini huku Sheria na katiba za Nchi zikitulinda katika kutimiza Yale malengo yetu ya maisha.

Nije kwenye mada kuu lengo la kuandika hapa ni kutaka kuishauri serikali kuwa hizi nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya ziwe zinatakangazwa na wizara ya tamisemi ambapo wahitaji watume maombi yao kwa kuonyesha vipaumbele vyao nini watafanya baada ya kuteuliwa katika maeneo yao watakayo omba kupitia hayo maombi ufanyike mchako wa kupitia sifa na Mahitaji ya eneo husika na muhusika Kisha Rais kufanya uteuzi baada ya kujiridhisha.

Na hii ni kwa kuingia mkataba aidha ya miaka mitatu au mitano. ambapo Kuna kipengele Cha kuvunja mkataba pale mmoja wake anaposhindwa kutimiza wajibu wake Kama ni serikali au muhusika. Hii pia itasaidia kuepuka kuteua teua watu ambao wanakuwa wanashindwa kutatua changamoto katika jamii zetu.
 
Chawa wako wengi na mwenye chawa anataka awape ulaji. Ndo maana leo anatengua na kuteua kila leo na hamna cha maana wanachodeliver
 
Back
Top Bottom