Kazi ya Mwanadamu: Tuko Tayari ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya Mwanadamu: Tuko Tayari !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Isaac, Oct 30, 2010.

 1. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 633
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Wakuu leo tumeshuhudia kampeni zikifungwa rasmi Tanzania nzima.
  Wakati akifunga kampeni hizo wilayani Hai,mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Mbowe alitoa wito kuwa Tanzania ilikuwepo kabla ya CHADEMA na CCM. Haina maana kupigana au kusukumana kwani vyama vitapita ila Tanzania na Watanzania watabaki.
  Akihutubia wananchi wa jimbo hilo,aliwataadharisha wananchi hao juu ya ofa ya pombe iliyokuwa ikitolewa na wagombea wa ccm. Hata hivyo kwa pamoja wananchi hao walipaza sauti na kumwambia kuwa 'LEO HATUNYWI' na kumuahidi Mbowe kura zote na kumpatia madiwani wa kutosha.
  Mbowe aliweza kupitia zaidi ya maeneo 14 huku akiongozwa na vijana zaidi ya 100 wenye pikipiki na magari kadhaa.
  Kama kawaida kila alipowataja wagombea wa ccm umati ulilipuka mayowe ya kuomboleza.
  Wakuu huku kaka kashaingia mjengoni, hebu tuelezeni na huko kwenu ilikuwaje?


  My take,

  Vyama vya siasa ni kazi ya mwanadamu ila Tanzania na Watanzania ni kazi ya Mungu.
  Sasa wakati wa kumweka Mungu mbele Tanzania. Mchague Dr. Slaa awe Rais baada ya Nyerere.

  By Mbowe Freeman.
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante mkuuu.
   
Loading...