Kazi ya kilimo cha bustani

Kazi ya kilimo cha bustani

Ngwathra

Platinum Member
Joined
Jul 11, 2007
Posts
6,015
Reaction score
11,383
Heshima mbele wadau.

Naona kuna vijana wengi waliosomea kilimo na biashara wanahangaika kutafuta kazi kwa miaka mingi bila mafanikio. Nimeamua kuanzisha kazi ya kilimo mchanganyiko cha mboga mboga na natafuta vijana wa kujitolea 10 wenye taaluma ya kilimo na biashara wanaopenda kujiendeleza pamoja nami kwenye hili eneo. Watakaowahi watapewa nafasi ya kwanza hadi nafasi zitakapojaa.

Nina eka 20 za kuendelezwa zina maji ya kutosha kumwagilia, pampu zipo, umeme nk. Nitawapatia allowance ya kula na malazi, mbegu, madawa, usafiri na viwezeshi vyote vya kufanikisha kazi hii. Tutaweka malengo na kufanya teams za kufanya kazi hii kwa ushindani na baadaye wataajiriwa permanently on performance. Tuna mashamba makubwa mengine yanayoendelea sasa hivi na hili ni eneo jipya tunaloliwekeza.

Wanaofikiri wana sifa hizi na wanapenda kufanya na hatimaye kupata maisha yao kwa kilimo karibuni sana na tuma cv yako kwa bungufarm@yahoo.com
 
Kaka asante kwa wazo, chukua hata wasio na cheti ili uwape inhouse training.
 
mimi sina hivyo vyeti unavyosema ila nimo na elimu ya kutosha (namaanisha elimu ya vitendo miaka miwili) sasa sijui kama na mimi na qualify ???????????
 
Kaka asante kwa wazo, chukua hata wasio na cheti ili uwape inhouse training.

Mkuu Malila naheshimu sana michango yako ya kujenga muda wote. Nimekaa na wadau wangu tumekubaliana na wazo hili na sasa tumeamua kupanua wigo kwa maeneo mawili.

1. Tunataka vijana 10 wanye nia ya kujifunza kilimo wenye elimu ya kuanzia ya kidato cha 4 kwa ajili ya kilimo cha bustani tutandelea kuongeza kutegemeana na mafanikio ya hatua ya kwanza. Tuna eneo kubwa na kuendeleza.

2. Tunahitaji vijana wenye nguvu 60 kwa ajili ya kuvuna muhogo shambani ulipo tayari ambao tutawaendeleza ili wawe wakulima wa muhogo kwa ajili ya kulisha kiwanda. Hii ipo tayari na tunawahitaji immediately. Baadaye hawa watapewa mashamba walime kwa ajili ya kutuuzia muhogo pia watakaopenda na hii itakuwa kazi ya kudumu. Watakaoamua kuajiriwa wafanye kazi ya mshahara shambani pia watapewa nafasi hiyo. Watakuwa kambini shambani hadi hapo watakapoamua kuondoka wenyewe.

Wasiliana na mimi kupitia email hiyo hapo juu.
 
Hapo huwezi wapata wasomi uwalimishe mchicha sema kama unataka vibarua wachapakazi nikutumie vibarua 10 fasta kwa dei za 7000 kwasiku.
 
Back
Top Bottom