Kazi ya chama cha upinzani.

Kazi ya chama cha upinzani.

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
Nimeona kwenye taarifa ya habari ya ITV mwanasiasa wa ccm akilalamika kuwa wapinzani siku zote kazi yao ni kubeza kila kinachofanywa na serikali. Sishani kama yupo sahihi na labda haelewi ni majukumu yepi ya vyama vya upinzani.

Katika chama cha upinzani makini, kinachofanya majukumu yake vizuri, kazi yake mojawapo ni kuikosoa serikali pale ambapo haitimizi matakwa na malengo ya wananchi.Hata hivyo, pale ambapo serikali itakapotimiza malengo na matakwa ya wananchi, chama cha upinzani hakiliazimiki kuisifia serikali, kwani serikali itakuwa inatimiza majukumu yake. Vyama vya upinzani ni chachu katika utawala bora na maendeleo kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom