KAZI?Uchumi Supermarkets:KUUZA DUKA/KUFAGIA/STORES/ULINZI/CASHIER?

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
481
145
Ndg M TZ,Kama mpaka leo hujapata kazi hizo hapo juu na hujui kwanini nenda Quality Plaza/Pugu Road njia ya kwenda uwanja wandege,
kuna supermarket /duka la UCHUMI-kutoka kenya.
Wanasema wamekuja na wafanyakazi wao kuanzia mlinzi,mpishi,mpaka mfagiaji kwa sababu wa Tanzania ambao ni qualified hamna.?*?
Hivi ndg zetu wa Immigration mnafanya kazi kweli,maana sitaki kuamini kama hawa jamaa wanavibali vya kazi-serikali yetu ilivyo makini haiwezi kufanya kosa hilo.
Nasikia Uchumi Supermarket ni serikali ya Kenya,jamani kama ni kweli hawawezi hata kutuonea huruma -hii Afrika mashariki ikikolea tutakimbilia wapi sisi,hii sio timing bomb?
Yangu macho!
 
mi naona sawa tu.Maana hawa watakuwa waaminifu kazini, kwanza hawatatoa udhuru kama misiba,vikao vya harusi na....

Kwa sababu wako ugenini watakuwa watii vizuri.
Hata mm ningefungua kampuni kenya ningetafuta watz kufanya kazi.
 
mi naona sawa tu.Maana hawa watakuwa waaminifu kazini, kwanza hawatatoa udhuru kama misiba,vikao vya harusi na....Kwa sababu wako ugenini watakuwa watii vizuri.Hata mm ningefungua kampuni kenya ningetafuta watz kufanya kazi.
Sidhani kama umemwelewa rakeyescarl! Just read between the lines
 
wabunge wet u mko hapa.. tusaidieni kwa hili jamani..
hivi hakuna hata mbunge au kiongozi mmoja ambaye ashawahi kwenda kuishi nje ya nchi hta kwa miaka miwili??? ninauhakika labda hakuna .. watu na nchi zao wanalindana sana kwenye suala la ajira na ikija kwenye ajira ambazo hazihitaji qualification kubwa utawakubali wenyewe sasa sisi sijui nani katuloga jamani ..
 
Sijui nitapata ajira mimi na advance diploma yangu ya computer?nimeomba kazi mpaka nimechoka.poa tu
 
Sijui nitapata ajira mimi na advance diploma yangu ya computer?nimeomba kazi mpaka nimechoka.poa tu

Pole sana malizia na degree maana sasa hivi wanataka sana degree mahali pengi pa kazi ila kwenye companies utapata
JIpe moyo mkuu Mungu atakujalia
 
Ndg M TZ,Kama mpaka leo hujapata kazi hizo hapo juu na hujui kwanini nenda Quality Plaza/Pugu Road njia ya kwenda uwanja wandege, kuna supermarket /duka la UCHUMI-kutoka kenya.Wanasema wamekuja na wafanyakazi wao kuanzia mlinzi,mpishi,mpaka mfagiaji kwa sababu wa Tanzania ambao ni qualified hamna.?*?Hivi ndg zetu wa Immigration mnafanya kazi kweli,maana sitaki kuamini kama hawa jamaa wanavibali vya kazi-serikali yetu ilivyo makini haiwezi kufanya kosa hilo.Nasikia Uchumi Supermarket ni serikali ya Kenya,jamani kama ni kweli hawawezi hata kutuonea huruma -hii Afrika mashariki ikikolea tutakimbilia wapi sisi,hii sio timing bomb?Yangu macho!
mkuu mbona kuna mdada anafanya hapo ni mbongo acha hzo fanya utafiti vizuri mkuu..
 
Ndg yangu kwani ni siri?Unahitaji uchunguzi gani si nauli ya dala dala tu, sikutegema useme kuna mtanzania 1, linalonisikitisha ni kuwa inawezekanaje ulete watu wa kazi ambazo tuna watu wa TZ wenye ujuzi huo kibao na hawana kazi ulete wa KQ kuchukua nafasi hizo na wa TZ wenye ma diploma etc wanakwenda kufanya kazi ambazo hazihitaji ujuzi, mambo mengine hayahitaji kwenda kukaa nje miaka, nenda leo hii Kenya ujaribishe kazi yoyote iwe ya ujuzi au casual labor uone mziki wake, nenda India, nenda Europe etc watakupa kazi ambazo wao wanaziogopa na hawazitaki na wanajua kuwa upo.Labda Europe uombe kazi za res.etc lakini kuita wawekezaji eti wanakuja na wafanyakzi wao -sisi tunahitaji nini huo uwekezaji.

Ukiendelea kuangalia mambo haya nazidi kuwaonea huruma vizazi vijavyo,nimesikia jambo la ajabu eti wakomoro (Comoro) wanafanya kazi ya export/import live animals kutoka TZ wakati import permits zote walionazo ni wa TZ na as a result wanaenda mpaka vijini na kununua wenyewe hao wanyama huku mwenye kibali akiwa body guard wakati huko Comoro huwezi kuthubutu kufanya any biz kama sio m Comoro na wakikujua hawasubiri serikali ikufuate wananchi wenye hasira kali either watakua/kukuibia au wanakumaliza tu.Najiskia kukereketwa!Aaaaagh!

n
mkuu mbona kuna mdada anafanya hapo ni mbongo acha hzo fanya utafiti vizuri mkuu..
 
M.Ushuru,
Nilifikiri ungetoa wazo ili sisi wenye uvivu na ulaghai tuanze kuajirika,hata kama wewe mambo yako ni swafi lakini nina imani katika hao wasio ajirika kuna njia 1 au nyingine wanakukamua ,either watakuibia kioo cha gari,wata abuse watoto wako,watakuibia njiani wewe au familia yako, kama ni majambazi watakuvamia kwako hata ukiwashinda na kuwaua tayari wamekutia doa,ukikutana na ndg yao atakudhuru kwa njia moja au nyingine na njia ya mwisho itabidi uwe mkimbizi kutoka kwenu kwenda kukaa nchi za watu ambayo si permenent solution ukirudi ukawakuta hawa game inaanza upya.
Unasemaje wacha waje au una maana wacha tuendelee kuwafungulia milango?
Heri yenu mlioajirika lakini wateteeni amabao inabidi wabadirike-tuache kuwateremshia mzig wenye madaraka amabao wengi wao wakiishapata hawageuki kuangalia nyuma!

Acha waje! Wtz tumezidi uvivu na ulaghai hatuajiriki ngoja tutie akili
 
..."Wawekezaji wanasema kwamba Watanzania tuna visingizio vingi linapokuja suala la kufanya kazi, ohh nina msiba, oohh mtoto anaharisha etc" - Mizengo Kayanza Peter Pinda (PM)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom