Jodeo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2015
- 1,286
- 1,328
Luka 5
"4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama."
TAFAKARI:
Usiku uliotangulia, Petro na wenzake wanahangaika baharini pasipo kupata hata samaki mmoja, lakini baada ya kumsikiliza BWANA YESU na kukubali kumtumikia kwa kile walichonacho (Chombo/mashua zao), Mungu anawapa kibali cha kufanikiwa sana. Petro anasema: " . kwa neno lako nitazishusha nyavu". Kumbe inatuchukua neno la Mungu ili kuzitenda kazi zetu kwa mafanikio na ufanisi mkubwa, kumbe inatuchukua neno LA Mungu ili tusitumie nguvu nyingi sana kwa mafanikio kiduchu!
Kabla hawajalisikia neno lake na kumtii, yale yote waliyoyatafuta (samaki) yaliwakimbia, lakini baada ya kulisikia neno lake na kumtii, yote waliyoyatafuta yakaanza kuwatafuta! Ndiyo maana tunaona samaki wanagombania kuingia kwenye nyavu za petro!
Kumbe inatuchukua kulisikia neno LA Mungu na kulitii ili Baraka na mafanikio vitutafute na kutufuata (Zaburi 23:6).
Kwa hiyo basi;
Chagua utamtumikia nani kati ya Mungu na Mali, maana haiwezekani kuwatumikia wote kwa pamoja (Mathayo 6:24). Ni maombi yangu, Bwana awe fungu lako, maana katika yeye kuna yote uyatafutayo (YOHANA 15:7 & Matendo 17:28).
Nakutakia Neema
Nawasalimu.
~JODEO~