Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,716
- 9,051
WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema kaya 3,000 zitasambaziwa gesi jijini Dar es Salaam ndani ya miaka miwili baada ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo Aprili, mwakani.
Dk. Kalemani aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Engie ya Ufaransa, Johan Kerrebroeck, ambaye alifika wizarani, ili kueleza nia ya kampuni yake katika kuwekeza kwenye mradi huo.
Pia kampuni hiyo inatarajia kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia ukiwamo wa Somanga Fungu wa megawati 240.
Waziri Kalemani alisema mradi huo wa usambazaji gesi utatelekezwa pia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na zaidi ya kaya 1500 zinatarajiwa kufaidika.
“Hatutaishia katika mikoa hiyo tu. Baada ya hapo tutasambaza katika mikoa mingine kama Morogoro, Dodoma na Pwani na katika magari,” alisema.
Dk. Kalemani alisema usambazaji wa gesi kwenye nyumba za makazi utasaidia kutunza mazingira kwa kuwa utapunguza matumizi ya mkaa ambayo ni zaidi ya asilimia 90 nchini.
Waziri wa Nishati, aliikaribisha kampuni ya Engie kuwekeza katika mradi huo wa usambazaji gesi kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Kuhusu uzalishaji wa umeme wa gesi asilia, Dk. Kalemani alisema upembuzi yakinifu wa mradi huo utakamilika Aprili, 2018 na baada ya hapo hatua zingine za uendelezaji mradi zitakapoanza kufanyika kwa kukaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Kerrebroeck alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk. Kalemani kwa kuteuliwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya nishati nchini.
Aidha, alisema kampuni yake ina uzoefu wa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya nishati katika nchi mbalimbali duniani zikiwamo Peru na Mexico. Nchini Tanzania, kampuni hiyo imewekeza katika mradi mdogo wa umeme jua wa Kilowati 16 katika Kijiji cha Ketumbeine mkoani Arusha.