A
Anonymous
Guest
Nilichokiona Kawe kinashangaza. Hivi kweli eneo hilo bado halina stendi ya daladala?
Eneo la Kawe, maarufu pia kwa 'huduma za Mwamposa' ni kitovu cha usafiri ambacho kinahudumiwa na daladala kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Licha ya idadi kubwa ya daladala zinazohudumu katika eneo hilo, bado hakuna stendi ya kisasa yenye miundombinu rafiki kwa abiria pamoja na madereva wa daladala. Eneo linalotumika kwa sasa si rafiki kwa watumiaji abiria wanapata shida kubwa, hasa nyakati za mvua. Mvua zinaponyesha, eneo hilo hugeuka kuwa matope kila mahali, huku abiria wakikosa sehemu ya kungojea magari au kujikinga na mvua pamoja na jua.
Aidha, kando mwa eneo hilo, kuna vibanda vya mama ntilie wanaouza vyakula. Ingawa huduma zao ni muhimu kwa jamii, mazingira ya eneo hilo si salama kiafya. Magari mengi yanatoa hewa chafu inayosambaa moja kwa moja hadi kwenye maeneo ya mama ntilie, hali inayoweza kuathiri ubora wa vyakula vinavyopikwa.
Vilevile, taka zinazozalishwa na mama ntilie hukusanywa na kutupwa karibu na eneo linalotumika kama stendi, ambapo abiria husimama wakisubiri usafiri na magari huwekwa. Hili ni hatari kwa afya za wananchi.
Changamoto nyingine kubwa ni ukosefu wa huduma za vyoo katika eneo hilo. Abiria, madereva na makondakta hulazimika kujisaidia hovyo, mara nyingine kwenye mitaro ya maji au maeneo ya pembezoni mwa stendi isiyo rasmi jambo linalohatarisha afya za wengi na kuchafua mazingira.
Natoa wito kwa mamlaka husika kufuatilia kwa kina changamoto hii ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu. Ni muhimu eneo hilo lipatiwe stendi rasmi yenye miundombinu rafiki kwa watumiaji wake.
Pia, naomba Maafisa Afya pamoja na Maafisa wa Mipango Miji wafuatilie huduma za vyoo pamoja na mahali panapofanyika shughuli za mama ntilie, ili kuhakikisha zinatolewa katika mazingira salama kwa afya za walaji na wananchi kwa ujumla.