Mtoa mada hana hoja yoyote ya msingi. Tatizo la watoto wanaosoma vyuo vikuu siku hizi ni vilaza sana ndiyo maana wanalalamika bila kujua wanalalamikia nini. Ngoja niwape shule kwa ufupi kuhusu hayo maswala ya Loans board.
1. Mwanafunzi anaposaini mkataba ni kwamba unakuwa ni mkataba kati yake na board, siyo chuo anchoenda kusoma
2. Ni jukumu la mwanafunzi kuhakikisha pesa yake imelipwa kwenye chuo husika, kwa sababu huo ni mkopo anaotakiwa kulipa
3. Ili kuhakikisha kama amelipiwa anatakiwa kusaini payroll inayotoka board ambayo vilevile ni uthibitisho kwamba amepokea hizompesa
4. Mwanafunzi asiposaini payroll pesa husika inarudi board, kwa hiyo ni jukumu la mwanafunzi kufuatilia hiyo pesa kulingana na maelezo niliyotoa kwenyen namba 1
Sasa wewe kaka mtu naomba umuulize huyo mdogo wako. Je alithibitisha kulipiwa kwa kusaini payroll. Kama hakufanya hivyo wewe mlipie tu hata aende mbinguni hatafanikiwa.
Halafu mpe elimu kuhusu mkataba. Siyo anasaini tu bila kujua. Ndo hao wakipewa majukumu watakuwa wanasaini mikataba ya hovyo hovyo
1. Kwa kawaida, mwanachuo kama hajalipa/hajalipiwa ada registration yake inakua restricted na matokeo yanabanwa.
2. Hapa unaongelea watu ambao wamesoma miaka mitatu na hawakukumbwa na vizingiti tajwa hapo juu.
3. Kwa case ya Udom, kumekuwa na ukaguzi mara kwa mara kuhakikisha wanachuo HAWADAIWI. To be specific hawa wanaodai vyeti walipitia ukaguzi maalum kabla na baada ya mitihani ya mwisho (kumaliza mwaka wa tatu.)
4. Kama chuo kilikua kimegundua mapungufu kuhusu nani anadaiwa na nani hadaiwi, wangeweza kuwataarifu wale ambao wamekaa mtaani MWAKA MZIMA wakisubiri vyeti.
5. Tofauti na hapo, watu waliambiwa wakachukue vyeti alafu walipofika chuoni ndio wanapewa habari za kudaiwa.
6. Unaposema mkataba ni kati ya mwanafunzi na bodi na chuo hakihusiki mimi nitakuuliza kwa nini ada inaingia mojamoja kwenye account ya chuo? Kama chuo hakitaki kuhusika basi ada pia isiingie kwao moja kwa moja.
7. Hela ambayo inaingia moja kwa moja kwenye account ya chuo, mwanafunzi mmoja kwa wakati wake anaweza kuhakikisha kuwa ada yake imelipwa? Hapa ndipo yanapokuja makaratasi anaambiwa amelipiwa asign kuhakiki, lakini utunzaji wa hayo makaratasi pia ni tatizo na upotevu umekua ukiripotiwa mara kwa mara.
PS:
- Utunzaji wa kumbukumbu hapo Udom pia si mzuri. Ninao watu nawafahamu ambao waliambiwa wanadaiwa laki tisa kwenye ofisi ya bursar, out of curiosity wakaamua kupanga foleni kuuliza tena na kukuta deni la pili halifanani na lile la mwanzo mathalani kama ulikua unadaiwa laki 9 (kwa mujibu wao) unaweza kuambiwa unadaiwa laki tatu au milioni moja. Hii pekee inatia mashaka kama madeni ni ya kweli.
Kwahiyo mkuu wangu unapowalaumu watu hapa mi nakuona snitch maana hii ishu nimeifuatilia tangu mwanzo and I know every detail. Hapa kuna mchezo.
Kama kweli tuko serious. Udom imeshajiunga na ARIS. Watu wawe wanapewa taarifa kwenye ARIS na ku'confirm huko huko electronically ili kupunguza upotevu wa data na udanganyifu wa kiholela.