Kawambwa ni waziri mpya wa michezo?

Kawambwa ni waziri mpya wa michezo?

Inkoskazi

Member
Joined
Apr 12, 2010
Posts
34
Reaction score
17
Tumekagua hoteli, uwanja na kila aina ya utaratibu kwa ajili ya timu, tumeridhika na ndiyo maana tumeingia mkataba,” alisema. Brazil watafikia hoteli hiyo ya Movenpick.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Shukuru Kawambwa (Waziri wa Miundombinu) alisema ujio wa timu hiyo ni historia kwa Tanzania na faraja kwa mashabiki wa soka nchini.

Akizungumzia mchezo huo, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Rais ya Masoko, Teddy Mapunda alisema ujio wa Brazil si tu utakuwa burudani, bali pia utasaidia kufundisha soka Watanzania hasa timu za soka. Mchezo huo utaonyeshwa pia na televisheni mbalimbali za hapa nchini.
Source: Mwananchi

My quote: Huu ujio kwanini unahusishwa na wizara ya miundombinu badala ya wizara husika ya michezo au(mjomba) Kawambwa ana nyadhifa mbili?


"Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe"
 
Hapana, ila ni kiongozi wa kamati hiyo maalum ya kuvutia timu za nje kuja Tz katika kipindi hiki cha Woza
 
Huyu jamaa hata uwanjani kwenye mechi zetu za ndani huwa haonekani! Inafanya watu wajiulize mara mbilimbili .. ukisema ni kwa sababu ni waziri wa miundombinu .. dots hazionekani
 
Akizungumzia mchezo huo, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Rais ya Masoko, Teddy Mapunda alisema ujio wa Brazil si tu utakuwa burudani, bali pia utasaidia kufundisha soka Watanzania hasa timu za soka. Mchezo huo utaonyeshwa pia na televisheni mbalimbali za hapa nchini.
Source: Mwananchi

Hivi hawa ni wageni wa raisi? Au ndio tunafuja pesa zetu kwa kutafuta umaarufu uso na faida
 
Hawa ni wageni wa Rais, si alisema atawaletea Real Madrid sasa amewaletea Brazil. Inapitia kwa Rais ili msiweze kuuliza matumizi (mkiuliza mtaambiwa ni usalama wa taifa)... kala kabao
 
Walau yeye ameanzisha Kawambwa Cup kule Kibaha, jana Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bwana Emmanuel Nchimbi, aliiaga timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars inayokwenda Eritrea.
 
What is the connection of Serengeti Breweries, TFF, Wa Brazil na soccer ya Tanzania . Maximo features kwenye matangazo yao.
 
Kawambwa ilibidii ateuliwe kuwa mwenyekiti wa kamati hiyoo eti kwa kuwa yeye pekee ndo mwenye kusikilizwaa kirahisii na mkuu..ana ukaribuu na muungwanaa na mkuluu huwa anampendaaa..lol!!!!!!!!!!!!!

Its a shame lakini ndo aina ya mkuluu wetuuu... mawazirii wengine mkuluu huwa anawashushuaa kimipashoo kwani hawazimikii ila hakuwa na jinsi akawateuaa tuuu...jamaniii
 
Back
Top Bottom