PreGE2025 Kawaida: Nitavitaja vyama vinavyofadhili vijana kufanya vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi UVCCM, Mohamed Kawaida ameeleza kuwa anazo taarifa za baadhi ya asasi za kiraia na vyama vya siasa vinavyowapeleka Vijana wa Kitanzania kwenye mafunzo nje ya nchi ili kuwaandaa kuja kuwa sababu ya machafuko na vurugu ndani ya nchi, akieleza kuwa siku sio nyingi atawataja wahusika ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Mohamed Kawaida ameyaeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Bukombe Mkoani Geita, akieleza kuwa ni jukumu la Vijana kuzilinda tunu za Taifa ambazo ni amani, umoja na mshikamano hasa wakati huu ambapo Taifa linajiandaa na uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Ninayo orodha ya hizo asasi za kiraia, ninayo orodha ya hivyo vyama vya siasa, ninayo orodha ya hizo Ngo's zinazotuma vijana kutaka kuharibu amani ya nchi yetu. Wakiendelea nitawataja hadharani ili serikali ichukue hatua dhidi yao." Amesema Kawaida.

Kwa upande mwingine katika hotuba yake, ameeleza kuwa UVCCM imejipanga kuhamasisha vijana kuipenda nchi yao na kushiriki kikamilifu katika ushiriki wa uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu, akisisitiza umuhimu wa amani na utulivu kwa maslahi ya maendeleo ya Taifa letu
Your browser is not able to display this video.
 
Ujinga mkubwa Sana. Halafu utakuta Kuna chombo cha habari kinarusha habari hiyo.

Kwenye uandishi wa habari Kuna mambo haya huwa yanazingatiwa.

1. What?

2. Which?

3. Who?

4. Where?

5. When

6. How?

Ukizingatia kanuni hii huwezi kushabikia kuandika habari kikanjanja.
 
ASASI YA KWANZA NI CCM.
 
Huyo dogo ni kijana, lakini anatumia mbinu outdated mno! Naona kaja na version nyingine ya m-pox na ebola. Ndio maana ccm inaendelea kutegemea vyombo vya dola, kama ushawishi wenyewe wa vijana ndio huu.
 
Haka ka, jamaa huwa, kanajiona kama Isaack Newton kwa, akili, huwa, kanaamini, Sana, upuuzi kanaoongea,
 
Ninayo orodha ya hizo asasi za kiraia, ninayo orodha ya hivyo vyama vya siasa, ninayo orodha ya hizo Ngo's zinazotuma vijana kutaka kuharibu amani ya nchi yetu. Wakiendelea nitawataja hadharani ili serikali ichukue hatua dhidi yao." Amesema Kawaida.
Halafu Polisi walivyo Wapumbavu watamuamini. Ila hii video na huu wimbo utaachwa
Your browser is not able to display this video.
 
Huyo dogo ni kijana, lakini anatumia mbinu outdated mno! Naona kaja na version nyingine ya m-pox na ebola. Ndio maana ccm inaendelea kutegemea vyombo vya dola, kama ushawishi wenyewe wa vijana ndio huu.

Ujinga hauwezi kufutika maana ni mtaji kwa watawala, ukiufuta CCM haiwezi kuwepo madarakani.

CCM ni maalum kwaajili ya wajinga na wanafiki.
 
Huyo dogo ni kijana, lakini anatumia mbinu outdated mno! Naona kaja na version nyingine ya m-pox na ebola. Ndio maana ccm inaendelea kutegemea vyombo vya dola, kama ushawishi wenyewe wa vijana ndio huu.

hawana jipya, wapunguze porojo na vitisho
 
Jina lake tu......KAWAIDA....jina linaakisi uwezo wake wa kufikiri
 
Huyo dogo ni kijana, lakini anatumia mbinu outdated mno! Naona kaja na version nyingine ya m-pox na ebola. Ndio maana ccm inaendelea kutegemea vyombo vya dola, kama ushawishi wenyewe wa vijana ndio huu.
Kichwan huyo jamaa ni Mbumbumbu MNoooo
 
Yaani
Yaani watu wanahatarisha amani, eti wakiendelea zaidi atawataja, huenda hata hiyo orodha hana!? Ikiwa watu hao ni hatari why asiwataje!?
 
The problem with politicians is that they get taken by their speeches.
Sir Humphrey
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kihalifu. CCM haina tofauti na Bokoharam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…