Elections 2010 Kaulimbiu ya Chadema 'CHADEMA MWAKA 2010 HATUDANGANYIKI'.

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe jana akiwa kwenye Uwanja wa Manyema mkoani Kilimanjaro alizindua rasmi kaulimbiu ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambayo ni ‘CHADEMA MWAKA 2010 HATUDANGANYIKI.’

Je kauli hii imebeba matarajio halisi yanayotegemewa na wananchi waliochoshwa na utawala uliopo madarakani? Tuijadili.
 
Hiyo Kauli mbiu ingewafaa sana wale watanzania wengi ambao bado wamelala kwenye usingizi mzito, hao ni wale ambao hawajui tofauti ya nyakati hizi na zile zilizopita, Ni bahati mbaya sana kuwa tunajivuna kuwa tumekomaa katika medani za siasa lakini nataka nikuhakikishie kuwa watanzania wengi wamejaa ushabiki na sio hodari katika kuchukulia mambo kwa umakini na nia ya dhati. Hivi leo tunavyosema kuna idadi kubwa sana ya Watanzania makini hawakujiandikisha kwa kupiga kura, wengi hupuuzia na kuona kuwa ni upotevu wa muda kusimama kwenye mstari wa kujiandikisha kupiga kura, mbaya zaidi ni kuwa hawa ndio ambao KAULI YA HATUDANGANYIKI wanaijua fika na kusingekuwa na haja hata ya kuambiwa na Dk. Slaa, sasa hao ndilo kundi ambalo naamini halidanganyiki. Kundi kubwa lililobaki ndio WADANGANYIKA ambao hao ndiyo ambao nimesema hawana uwezo wa kujua kinachoendelea, hao ndio Bendera fuata upepo, na hao ndiyo kwa asilimia kubwa walihamasika na kushinda kwenye mistari ya Kujiandikisha kupiga kura. Hao ndio wale ambao kama sio wa dini yake au kabila lake au Chama chake hawampi kura hata kwa nini hao ndio wale ambao hawajui hata kazi ya Diwani achilia mbali huyo mbunge wao wanachojua ni kamshiko au uhusiano uliopo. Ndiyo maana sikushangaa kwenye kura za maoni zilizopigwa hivi karibuni watu wa ajabu ambao kwangu mimi najua fika hata majukumu ya mbunge hawayajui wamepigiwa kura za ndio huku watu makini ambao wanauwezo wa kuibua na kujenga hoja za maana na zenye faida kwa Taifa wamepigwa chini. Ninaikaribisha akauli mbiu ya CHADEMA ila kazi kubwa ifanyike ili hili kundi kubwa la WADANGANYIKA safari hii lijue Faida za kuchagua watu makini. Napenda sana KAULI YA TV mlimani inayosema ''ELIMU KWANZA''
 
6th August 2010


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni








Slaa2(12).jpg

Dk Wilbroad Slaa.



Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Dar es Salaam, wamejifungia jijini hapa wakipanga mkakati wa mapokezi ya mgombea urais wao, Dk Wilbroad Slaa.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Chadema zilieleza kuwa vikao kwa ajili ya maandalizi hayo vilifanyika katika nyakati tofauti, ili kufanikisha mapokezi hayo atakapowasili jijini hapa kesho.
Kuwasili kwa Dk Slaa jijini Dar es Salaam kunafuatia ziara ndefu aliyoifanya kwenye mikoa ya kanda zote nchini, akitafuta kudhaminiwa ili ashiriki kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Tayari Dk Slaa ameshafanya mikutano ya hadhara na kuomba kudhaminiwa katika mikoa ya kanda ya kaskazini, ziwa Victoria, Magharibi, Kati, Nyanda za Juu Kusini na Kusini.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Dk Slaa kuwasili jijini Dar es Salaam tangu achukue fomu ya kuomba kugombea urais kupitia Chadema.
Hafla ya kuchukua fomu hiyo ilifanyika katika jimbo la Karatu mkoani Arusha ambalo amekuwa mbunge wake kwa miaka 15 mfululizo.




CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
 
Ushindi wa Dk. Slaa kuimarisha Bunge


maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 04 August 2010

Mahasimu waweza kuwa upinzani Wakongwe waaga kwa msononeko


slaa_200.jpg



USHINDI wa Dk. Willibrod Slaa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, ndio pekee unaoweza kumaliza mivutano iliyokumba bunge lililopita, MwanaHALISI imebaini.
Kwa mujibu wa matokeo ya kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopigwa Jumapili iliyopita nchi nzima, viongozi wakuu wa makundi mawili yaliyokuwa yakinyukana, wameshinda kwa kura nyingi katika machimbo yao.
"Mvutano umedumu katika mazingira ya utawala ambao hauchukui hatua; unaolea na kubembeleza mafisadi. Dk. Slaa hawezi kulea ufisadi hata kwa miezi miwili," ameeleza kiongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Dar es Salaam.
Dk. Slaa ambaye ameteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais, ndiye mbunge wa upinzani aliyejitambulisha katika kuibua wizi na ufisadi ndani ya serikali.
"Lakini katika hali ya kuwajibika, huwezi kuacha wabunge walumbane juu ya suala linaloweza kumalizwa mara moja kwa kutema wanaonekana kuwa vikwazo," ameeleza kiongozi huyo wa CHADEMA.
Malumbano ndani ya bunge yalichipuka katika kashfa ya mkataba wa uzalishaji umeme wa dharura kati ya serikali na kampuni ya Richmond.
Kashfa ya Richmond ilichunguzwa na Kamati Teule ya Bunge na kuwataja baadhi ya wabunge na maofisa wa serikali waliohusika nayo.
Kutokana na kashfa hiyo, Edward Lowassa, aliyekuwa waziri mkuu alijiuzulu kufuatilia kushiriki kimalifu katikla mchakato wa mkataba huo.
Rais Kikwete alilazimika kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri akiwaacha nje mawaziri Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao walitajwa kushiriki kikamilifu katika kashfa hiyo.
Katika kura za maoni za Jumapili iliyopita, wanaoitwa mahasimu wakuu katika sakata hili wameshinda kwa kisindo. Majimbo ambako wabunge hao wa CCM wameibukia yameelezwa kuwa na upinzani "mdogo sana."
Wakati Spika aliyemaliza muda wake, Samweli Sitta ameshinda jimboni Urambo Mashariki, Edward Lowassa ambaye amekuwa akidai kuhujumiwa kisiasa ameibuka na ushindi jimboni Monduli.
Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Richmond, Harrison Mwakyembe ametikisa kwa kishindo jimboni Kyela na Rostam Aziz ameshinda jimboni Igunga.
Andrew Chenge wa Bariadi Mashariki ameshinda kwa kura nyingi huku Christopher ole Sendeka ameibuka kidedea huko Simanjiro.
Sitta, Mwakyembe, Sendeka, Anna Kilango wa Same Mashariki, Victor Mwambalaswa wa Lupa na wabunge wengine wamekuwa upande mmoja wa kupinga ufisadi; wakati Lowassa, Rostam na Chenge wamekuwa wakituhumiwa kuwa upande wa wanaotetea ufisadi.
Lakini malumbano na minyukano ndani ya bunge imekuwa ikiletwa kwenye ngazi ya watu binafsi badala ya wapinga ufisadi dhidi ya waungamkono mafisadi.
Katika hili Sitta na Dk. Mwakyembe wameeleweka kuongoza upande wa wapinga ufisadi, wakati Lowassa na Rostam wametajwa kupingana nao.
Majeruhi katika kambi ya Sitta na Mwakyembe ni Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii, mwenzake wa Bumbuli, William Shellukindo na James Lembeli wa Kahama ambao wamebwagwa.
Katika kambi ya Lowassa ni Nazir Karamagi wa Bukoba Vijijini aliyekumbwa na kimbunga cha kukataliwa katika kura za maoni.
Kura za maoni mwaka huu zilikuwa chungu kwa wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walishindwa vibaya na wagombea wasiotarajiwa.
Mkoa ulioongoza kwa kuachana na wakongwe wa siasa ni Iringa ambapo zaidi ya nusu ya wabunge wa zamani wamebwagwa.
Wabunge hao ni Jackson Makwetta (Njombe Kusini), Joseph Mungai (Mufindi), Benito Malangalila (Mafinga), Profesa Raphael Mwalyosi (Ludewa) na Monica Mbega (Iringa Mjini).
Wabunge hao wamekuwa bungeni kwa takribani miaka 20 bila ya kukatizwa. Mbunge mwingine wa Iringa kwa muda mrefu ni Anne Makinda (Njombe Kusini).
Makinda ameshinda kura za maoni na iwapo atashinda katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu, ndiye atakuwa mbunge wa muda mrefu kuliko wote katika bunge lijalo. Aliingia mwaka 1975 kupitia Umoja wa Vijana.
Wakongwe wengine waliodondoshwa ni John Malecela (Mtera), Juma Ngasongwa (Ulanga Magharibi) na William Shellukindo (Bumbuli).
Hata hivyo, kura za maoni za CCM zinadaiwa kutawaliwa na rushwa huku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ikitangaza kila siku waliokamatwa na kuhojiwa kwa tendo hilo.
Katika sehemu mbalimbali nchini pia, ikiwemo Dar es Salaam, uchaguzi umeahirishwa kutokana na kutofuata taratibu na vitendo vilivyodaiwa kuwa vya upendeleo.
Jijiji Dar es Salaam, wanachama wa CCM wapatao 700 walirudisha kazi zao kwa chama wakidai kuwa majina yao yaliondolewa kwenye orodha ya wapiga kura ndani ya chama.
Baadhi ya wananchi wamedai kuwa wamekuta majina yao yamewekewa alama ya "ndiyo" ikiwa na maana kuwa tayari wamepiga kura.
 
KURA YA MAONI

Mgombea yupi utampa kura yako ya Urais 2010?
Jakaya Kikwete


7%
Willbrod Slaa


88%
Ibrahim Lipumba


4%
Mutamwega Mugahywa


0%
Hashim Rungwe


1%
Paul Kyara


0%
Christopher Mtikila


1%
Peter Kuga Mziray


0%
Total votes: 339

 
KURA YA MAONI

Mgombea yupi utampa kura yako ya Urais 2010?
Jakaya Kikwete


7%
Willbrod Slaa


88%
Ibrahim Lipumba


4%
Mutamwega Mugahywa


0%
Hashim Rungwe


1%
Paul Kyara


0%
Christopher Mtikila


1%
Peter Kuga Mziray


0%
Total votes: 339


hizi statistic umepika mbona matokeo uliyo weka hapa haya landani na yaliyo mtandaoni
nilikuwa na shaka na link kama ipo ukweli poll ya mwanahalisi haisomi hivyo slaa anaongoza kwa 88%
 
Back
Top Bottom