Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,942
- 18,669
Hizi kauli za mara ooh " walitaka kunuhonga" mara " wananiomba niwateue" mimi kibinafsi zinanikera sana kwa sababu kwanza zimekaa kinafiki na pili zimekaa kimipasho kama sio taarabu.
Kwa mfano mimi kibinafsi huwa namchukia mwanamke anayekuja kwangu nakuanza kujitamba kwamba mara ooh flani anataka kunihonga gari mara hoo flani anataka nimchague yeye. Mara nyingi wanawake wa aina hii huwa ni waongo na wanapenda majivuno.
Sasa tukija kwenye upande wa siasa unakuta kiongozi anakuja kujitamba eti nilitaka kuhongwa. Huwa najiuliza, inamaana Takukuru hajui inafanya nini. Na hata hao Takukuru wapo tu wanakodoa macho hawawezi hata mchukua maelezo na kufanya kazi yao?
Kusema ukweli hii misemo haikuwepo awamu iliyopita. Mi nachoona hapa, Maigizo yanazidi kiwango cha bongo movie.
Unakuja kujitamba, "Ooh...wapo wengi wananiomba omba". Wewe Kwani umekuwa Yesu?
Mbona Nyie mnakujaga kutuomba sisi kura ila hatujitambi????
Tena ndye yulee aliye kuwa anatuombaomba kura mpaka anapiga pushup.
Alfu nilichogundua, kumbe vyeo mnaombana...Duh!!! Na mimi naombaa.... asee.