livafan
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 2,925
- 5,528
Herini ya Mwaka mpya kwetu sote tuliojaariwa pumzi tena na Mwenyezi Mungu kuwa sehemu ya watz tuliojariwa kuendelea kuishi tena.
Niende moja kwa moja kwenye hoja ya maada hapo juu na swali nililoambatanisha hapo nitaomba wajuvi wa mambo mchambue na kutoa mwongozo na majibu juu ya swali ambalo nimeuliza “ je Rais anasimama na ataendelea kusimama na wanainchi kwa kipi/lipi ?”
Kwa kurejerea hapo nyuma kidogo awamu ambayo haikukamilika iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Mhe Magufuri .Tumeshudia mambo mengi ambayo mwendazake kama anavyoitwa sasa kufanyika chini ya utawala wake na mambo hayo mengi wanainchi wengi yaligusa maisha yao hasa wa kipato chetu kidogo ikiwemo mimi hapa .
Mojawapo ya mambo ambayo Mhe Magufuri aliyafanya akimaanisha kusimama na wanainchi leo hii kila mmoja wetu anajua, swala la ghararama za kuunganishiwa umeme zilishuka, Vijana wengi waliweza kufanya biashara ndogo ndogo hizi na akawatambua kwa kuwapa vitambulisho vile tuvijuavyo , Elimu bure kwa level ya sekondary kidogo imesaidia sana, kuondoa wafanyakazi hewa jambo ambalo lilisaidia kuzuia kuliwa kwa fedha za walipa kodi kwa kisingizio cha kulipa mishara hewa, nidhamu ya watumishi serikalini iliimarika japo kiuwoga ila ilisaidia na huduna zikawa bora na mambo mengi sana ambayo yaligusa watanzania.
Kwa kipindi hichi cha mwaka mmoja chini ya Utawala wa mama yetu, Rais wetu wa JMT Mama Samia tumeshudia na pengine tutaendela kushuhudia nambo mengi yakifanyika chini ya uongozi wake. Kwa bahati nzuri SSH amefanya kazi pamoja na Mhe Magufuri na amekuwa akijinasibu kuwa yeye na Mwendazake ni kitu kimoja yaani kiatu na Mguu, ya kwamba maono yoote ya Magufuri yatafanyiwa kazi na kuendelezwa jambo ambalo kwa siku zile watz wengi walifarijika sana baada ya mama kunena hayo yote kwenye hotuba ile aliyoitoa mara ya kwanza baada tu ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa JMT.
Walakini mambo mengi sana hapa katikati yameamuriwa na mama ambayo mengi yake wanainchi ambao yeye mama anadai kusimama nao hawakufurahishwa nayo kabisa.
Baadhi ya hayo ni kama ifuatavyo
1. Kurudisha watumishi ambao waluonekana kipindi kile wanavyeti feki na yeye katika awamu ndie aliekuwa msaidizi wa Rais
2. Safisha safisha ya machinga, Vijana wengi, wamama wengi wamepoteza ajira hizo walizokuwa wamejiajiri wao baada ya kuvunjiwa vibanda vile na kudanganywa kuna sehemu maalumu pameandaliwa na watapelekwa, lkn wapi na wapi
3. Tozo, huu ni mwiba unaochoma nyayo za wengi, na mwenye mwiba huo ni serikali hii inayodai inasimama na watanzania ikidai kwamba hizo tozo zitaleta madarasa na madawati wakati kumbe madarasa hayo yanajengwa na mkopo wa trl 1.3, je kazi ya tozo kumbe ni ipi ?
4. Kurudisha Mzigo mkubwa wa garama za kuunganishia wateja huduma ya umeme wakati serikali muda huohuo inacharge % fulani mtu akiwa ananunua umeme kwa njia ya luku kwa madai kwamba hela hiyo itasaidia umeme wa rea n.k
Je , Mama anasima na Wanainchi kwa Yapi ? Maana yote yanayogusa wanainchi hasa walio wengi ni hayo ambayo kwa uchache nimeorozesha kwa apo juu.
MAMA SSH, NITASIMAMA NA WANAINCHI, JE ANASIMAMA NA WATZ KWA YAPI / LIPI ?