thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Nianze kwa kutofautiana na wale wanaopinga Kauli ya ndugu Palamagamba Kabudi, alioitoa bungeni, akihitimisha hoja ya wizara ilio chini yake ,(wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki) .
Mimi naikubali Sana tu kauli hiyo.
Kiukweli Kabudi kawa mkweli, na jumuiya ya kimataifa imesikia msimamo wa serikali ya awamu ya tano . bila kupepesa
Watanzania tuache woga wa kunyimwa misaada kisa kusema ukweli. Tuwaite Mabeberu au wema kiasi gani, wenyewe wapo kimaslahi zaidi, na si vinginevyo."they don't care the word Beberu "
Trump alituita waafrika shitholes baadhi yetu mlifurahi Sana, kwanini iwe nongwa Kabudi kuwaita Mabeberu? ,hilo jina ni size yao kabisa.
Kuhusu misaada ,nchi hii tumepata misaada mingi lakini tumeendelea kua maskini wa kutupwa, pamoja na utajiri wa raslimali nyingi tulizonazo chini ya ardhi.
Ndugu watanzania, misaada haitatuletea maendeleo, maendeleo tutayapata kwa kufanya kazi kwa bidii katika uzalishaji mali,na kutokomeza rushwa na urasimu maeneo yote yanayohusu maendeleo yetu.
Lazima tusimame Kulinda utu wetu , dhidi ya hila zozote zile dhidi ya taifa letu .
Mgawanyiko wowote ule ni kuwapa fursa na mwanya wa kutuyumbisha ,eventually kutusambaratisha.
Narudia tena kauli ya Palamagamba Kabudi, Mabeberu hawana nia njema na taifa linaloelekea kujikomboa kiuchumi, kwani, uchumi mzuri hukufanya uwe huru dhidi ya mashariti yoyote hasi. Na ikumbukwe mashariti hasi yanazitesa nchi nyingi sana zinazojaribu kujikwamua kiuchumi.
Tujiulize, China, Veatinum, Malasia,Indonesia zimeendelea kwa kupewa misaada?, jibu hapana,ni kwa kufanya kazi kwa bidii huku wakijinyima.hatimaye sasa ni nchi za kupigiwa mfano. Watanzania tulichokua tunakosa ni uadilifu wa watumishi tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha.
Rais Magufuli kaonyesha njia, ni jukumu letu sote kuungana nae kuijenga nchi.
Tulichokua watanzania tunakosa ni kiongozi jasiri wa kusimamia raslimali zetu. Leo kapatikana tunamkatisha tamaa na kumzodoa, mbaya Sana.
Lazima tubadili mindset zetu na tukiri ya kwamba tunaweza.
Lingine, Rais Magufuli hajafukuza wawekezaji wa kweli nchi hii, Kama baadhi yetu tunavyofikiri na kuaminishwa ,
Alichokifanya ni kuitoa Tanzania katika jina la shamba la bibi na kuifanya nchi inufaike na raslimali zake .huu ni msamiati mpya Tanzania, kwa slogan yake ya hamsini kwa hamsini. Umekua mwiba kwa makampuni ya kitapeli.
Hata hivyo Rais Magufuli amekua akitoa ruhusa kwa wawekezaji Kama wanaona kuna urasmi kwa wasaidizi wake, wamuone yeye Moja, kwa moja,,hii ni kuonyesha nia yake njema kwa nchi na wawekezaji pia.
Wanaojifanya mazingira magumu ni wale ambao walikua wakizoa tena bila mitaji yoyote ile,kisha kwenda zao, sasa kawabana, kilio chao kimebakia eti mazingira magumu.
Vijana nawahusia tena muda mnaoutumia kutukana mitandaoni na kulalamika, mwaka, miaka, mngeutumia kubuni mbinu za kujikomboa kiuchumi taifa lingekua mbali Sana, kwani serikali iko tayari kusaidiana nanyi katika kuiletea nchi maendeleo .
Matokeo yake mmebobea kwenye lawama na matusi. haya tuendelee na matusi na kulalamika Kama yataleta maendeleo.