Kauli ya raisi juu ya msimamo wa chama

Kauli ya raisi juu ya msimamo wa chama

Joined
Nov 30, 2013
Posts
5
Reaction score
3
RAIS WANGU NISIKILIZE

Katika kuadhimisha miaka 37 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete alitoa tamko kuwa “MSIMAMO WA CHAMA CHA MAPINDUZI NI SERIKALI MBILI”

Binafsi napenda kumpongeza Rais kikwete pamoja na washauri wake kwa kuweza kuwa mwanasiasa bora mwenye kutoa kauli kulingana na nyakati.
Hakuna asiyejua kuwa, siku ya kukabidhiwa rasimu ya pili ya katiba, Mhe Rais alisema kwa msisitizo na tahadhari kubwa kuwa “ENDAPO VYAMA VYA SIASA VITALICHUKULIA SUALA LA KATIBA KWA MASLAHI YA VYAMA , WATALIINGIZA TAIFA MATATANI”
Kwakuwa Rais Kikwete yeye akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia ni mwenyekiti wa CCM analazimika kusaliti kauli zake kutokana na majukumu aliyobebeshwa na wanaCCM nay ale ya WATANZANIA WOTE!

Nani asiyejua kuwa, wapiga kura si wote ni wanachama wa vyama vya siasa, hivyo Rais anavyotoa kauli ya msimamo wa CCM, lazima ajue kuwa kauli yake inaweza chukuliwa kama ni kauli ya Rais wa Nchi na siyo kauli ya MWENYEKITI WA CCM!
Kwa mtu asiyejali vyama, mwenye kujali taifa, anamfahamu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete kama RAIS WA Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.Inapofikia hatua ya yeye kutoa kauli kama mwenyekiti wa chama , anakuwa anawaburuza kifikra watanzania wenye utaifa mbele ya maslahi ya vyama.
Miongoni mwa vitu vilivyopigiwa kelele katika katiba ya nchi na muundo wa uongozi ni MAJUKUMU YA RAIS, Rais Kikwete alazimika kusaliti kauli aliyoitoa kwa watanzania, kauli yenye kujenga matumaini na kuwapa amani wanyonge, juu ya umuhimu wa suala la wanasiasa kuweka maslahi ya taifa mbele kwenye mchakato wa katiba.

Hakuna asiyejua kuwa Rais ni Taasisi, taasisi hiyo imeundwa na watanzania, CCM ilimchagua Mhe Jakaya Kikwete kama Mwenyekiti wa Chama na Mgombea wa Urais kupitia CCM, Baada ya hapo jukumu la kumpa mamlaka ya kuwa Rais liklikuwa ni la watanzania wote.Watanzania wote ni pamoja na wasio na vyama vya siasa.
Leo hii Rais akitoa tamko kwa vyombo vya Usalama kuwapiga wapinzani na akasema nimeongea kama MWENYEKITI WA CCM siyo kama Rais, kwa vyovyote amri hiyo itaheshimiwa kutokana na kofia ya URAIS.
IKUMBUKWE KUWA;KWA UTASHI WAKE BINAFSI, RAISI ANAWEZA SIMAMA KAMA:-
1.Mtetezi wa Watanzania wote(kwa masharti ya kuweka Uccm chini)
2.Mtetezi wa CCM (kwa masharti ya kuweka UTAIFA na UZALENDO chinki)
3.Mtetezi wa Maslahi yake (Kwa masharti ya kuweka Uccm na Utaifa/uzalendo chini)

Binafsi naamini jambo jema kwa kiongozi mkubwa kama huyu ni vema akazingatia utaifa kwanza.
Kauli ya Mhe Rais juu ya msimamo wa Chama Cha Mapinduzi, ilitolewa muda sahihi , ila haikutolewa na mtu sahihi.Kwanini kauli kama hizi zisitolewe na Makamu mwenyekiti wake, wapo Makatibu weneezi, amabao wanatoa kauli mbali mbali , kwakuwa hawana dhamana ya watanzania wasio na vyama, kauli zao zinachukuliwa kiCCM.

MAONI YANGU:
Vyama vyote vya siasa vina nia ya kushika DORA,lakini ushikaji dora ni pamoja na kuwafanya wanyonge na wasio na vyama waishi kwa matumaini.
Hivyo :
1.Viongozi wa vyama vya siasa wanapopewa maamlaka ya kuongoza nchi, wavae utaifa kwanza kuliko ukada.Hili si tatizo la CCM pekee, vyama vyote hili ni tatizo.
2.Endapo uzalendo utakuwa mbele, itakuwa si vigumu kuona waziri wa chama cha upinzani, maana mteuaji hatohofu , pia mteule hatatumia mamlaka kwa maslahi ya chama chake.
3.Endapo Rais atazidi kuwa ni Mwenyekiti au kiongozi mkuu wa chama cha Siasa, ni raisi kuamini kuwa vyombo vya dora (JESHI LA POLISI) vikifanya makosa watu watasema kiongozi wa chama ambaye pia ni amri jeshi mkuu ndiye aliyetoa amri hizo ,maana vyombo hivyo vimefunzwa kutii kauli za amri jeshi mkuu.

TAMATI
Viongozi wa siasa hawawezi kusimamia zoezi la katiba mpya kwa maslahi ya taifa bila kuingiza maslahi ya kuzidi kushika dora au kupata dora. HIVYO watanzania, tusiwape ridhaa wanasiasa kutuamulia mambo yote.Kauli za wanasiasa wote, toka vyama vyote zichujwe sana ndipo zifuatwe.

REJEA: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IBARA YA 18(a)

Nawatakia maandalizi mema ya kuelekea kwenye mchakato wa katiba mpya
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu libaliki Bunge la Katiba mpya.
 
^^
Mfumo wa vyama vingi wa Rais anapochaguliwa akabaki na mamlaka ya juu kichama, ndio unawafanya baadhi ya watu wasielewe Rais alisema wapi na katika wadhifa upi.
Na hiyo ni athari ya Presidential democracy
^^
 
Jei kei ni dhaifi, na mimi nilishampuuza kwa kila alifanyalo.
 
Samwel Luhanga ni kiongozi dhaifu kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania!
 
Nakubaliana nawe100%. Utaifa kwanza vyama baadae. Ilitakiwa kiwekwe kipengele kitakachopiga marufuku misimamo ya vyama kwa wajumbe wa Bunge la Katiba
 
Kweli si mara moja ama mbili Rais anazungumza kwa sura mbili (double standard) kama unakumbuka sakata la kupandishwa bei mafuta ya taa mswaada ukapata baraka za mwenyekiti wa baraza la mawaziri..rais ukawa sheria. Baadae suala hilo likatolewa msimamo na NEC ya CCM wakililaani mwenyekiti akiwa ni Rais huyo huyo.

Katika hotuba ile ya tarehe 2/2/2014 mwenyekiti alitoa msimamo wa chama juu ya serikali mbili kipengele kidogo tu katika rasimu ya katiba.hiyo hotuba ikasindikizwa na uteuzi wa bunge la katiba ukionyesha wengi ni wanan-CCM kwa ajili ya kulipitisha tamko la mwenyekiti. Kumbuka wapo CCM kama mimi tunaotaka Tanganyika irudi ukimjumlisha na Sita, kina bomani, Warioba na wale wa G55 waliokuwa hai. Hivyo hata uteuzi umewaangalia wale wanaoona sawa nmwenyekiti..hususaniviongozi wa sekreteriati yaya Chama vijana na wajumbe wa NEC kupitia makundi ya ajabu ajabu yaliyowekwa na sheria ya mabadiliko ya katiba imiyovita hisia kipindi cha bunge. Anyway tuangalie mwisho wa move japo imani imenitoka kama katiba itakuwa ni ya Chama ama Wananchi kwa mtindo huu
 
Hoja yako naiunga mkono asilimia 100. Hata kwenye hotuba yake kwa viongozi wa vyama na dini hivi karibuni,amerudia tena kauli ya chama chake kuwa na sera ya serikali mbili. Hata hivyo, Mungu atakuwa kwenye upande wa wananchi wengi tusio na vyama!
 
Back
Top Bottom