Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Mhariri wa HabariLeo amekuja na mpya baada ya kuacha kazi yake ya kuutumikia umma wa Watanzania (wanaolipa mshahara wake) na kujivika ukada wa CCM kumtetea JK. Mimi niliisikiliza kwa ufasaha hotuba ya Kikwete na alikuwa wazi kabisa kuwa wafanyakazi na Tucta hawambabaishi na alienda mbali zaidi kwa kuwatishia uhai wao wale wote ambao wangevunja amri ya serikali ya kutogoma akitoa mifano ya jinsi serikali ilivyoweza kuwaua wale waliojihusisha na migomo ambayo serikali iliita haramu.. vipi leo hii anaanza kuyameza maneno yake? Anatumia vyombo vya habari vya serikali kumtetea ili kuwalaghai wafanyakazi? tunasema mwaka huu ng'o! Mlitulaghai na vyombo vyenu fake mwaka 2005 safari hii tafuteni mbinu nyingine
repetitive... JK alivyokuwa fawning,sycophantic,obsequious
Hata kama ningetaka kuwafurahisha akina mzee Mgaya, kwa jambo hili haiwezekani. Na, kama wanavyodai kwamba watampigia kura kiongozi na chama atakayewapa fedha hizo, kura hizo sisi tunahesabu tumeshazikosa. Ni afadhali kuzikosa kura za akina Mgaya kuliko kuwaumiza wananchi walio wengi kwa kutumia fedha zote za nchi kuwapa akina Mgaya wagawane na kuwakosesha wananchi huduma muhimu. Jambo hili sitalifanya.
Mbali zaidi alikwenda kama Amiri Jeshi Mkuu alikuwepo Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,Mwamunyange,Mkuu wa jeshi La Polisi Saidi Mwema na Mkuu wa Jeshi La Magereza,alikuwa anatangaza vita na wafanyakazi,lazima aadhibiwe kwa Kitendo hatarishi kama hicho huwezi kutishia watu na kutaka wafyate midomo wanapoidai haki zao wakiwa hawajavunja sheria yeyote ya nchi na wakiwa wakitimiza waajibu wao kikatiba,TUCTA tuko nyuma yenu kwa lolote mtakalosemaHuyu Mhariri wa Habari Leo,sometimes I think he is lacking in profound meditation. Ile hotuba aliyotoa JK Diamond Jubilee Hall kwa wazee wa Dar es Salaam ilikuwa speech kali ingawa hakusema kwamba anataka kumuua mtu yoyote. Lakin kama nilivyoandika pale kwanza,kwamba ''it was a Stalinistic speech'' na kwamba wafanyakazi wangegoma,wakuu wao wangeitwa Cenrtal Police Station to sign a confession that they were instigated by Foreign Counter-Revolutionary powers.
What I did not like about that speech ni jinsi yule Mkuu wa Mkoa,William Lukuvi alivyokuwa anashabikia wakati JK anazungumza,kama vile yeye ndiye aliyemchochea JK kusema maneno yale yote. Halafu what was surprising about that speech ni jinsi ambavyo kesho yake,baada ya kutoa ile hotuba kuwafokea wafanyakazi,jinsi JK alivyokuwa fawning,sycophantic,obsequious,alipokuwa anaongea na dignitaries waliokuja katika World Economic Forum for Africa. Imekuwa kama vile JK ana dual personality,vigumu kuamini huyu anaongea hivi leo,ndiye aliyeongea vile jana.
Lakini yale mambo yameongewa zamani na sasa I think the bitterness has passed,na ule mgomo,I don't know what happenned to it,naona kama vile ule mgomo umeyayuka. Lakini wafanyakazi wanaweza kuelezwa maneno yale yale John the Baptist aliyowaambia askari,kwamba waridhike na mshahara wao,wasiwe na tamaa.