EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,709
- 35,712
Akiwa bungeni dodoma kama spika wa Bunge ndugu Job Ndugai ameshauri kuwa tungeanza kujenga bandari ya Bagamoyo kuliko reli ya SGR. Kiuchumi hii imekuja kukiwa na maswali mengi kwa nini mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo umesitishwa. Faida za kiuchumi ni kubwa lakini inaonekana hazina yetu haina kitu. Pesa hakuna. Nimesoma uchambuzi wa ndugu Zitto kuhusu hali ya uchumi kwa ujumla nikapata walau picha ya kwa nini mkataba umevunjwa. Ni matrion mengi ya madafu yanahitajika ili kujenga hiyo bandari. Mkataba umevunjwa!
Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa: hivi ni huyuhuyu Ndugai aliyeonekana kushindwa kuongoza bunge anahoji hivi? Nani kamwamsha usingizini? Hivi hajui bunge linapaswa kusimamia serikali hivyo? Ni mawazo hayo anayosema yaliyowafukuzisha wapinzani bungeni. Kwa nini hatupendi kuchukua mawazo mazuri ya wapinzani na kuyaingiza kwenye utekelezaji? Walio upande wa pili hufanya utafiti, husoma vitabu, hisikiliza na huchambua. Hata uwasilishaji wa hoja zao ni tofauti na ndugu zetu wa chama cha mapinduzi. Wabunge kama Hussein Bashe aliwahi kuhoji juu ya SGR wakaishia kuhojiwa uraia!
Leo hii Ndugai kainukia sijui wapi na kuja na mawazo yaleyale. Kwangu naona ukombozi wa kifikra kwa spika wetu. Endapo ataendelea hivi basi neno "dhaifu" litakufa.
Ujenzi wa reli inaitwa Standard Gauge...ulifanywa kwa mihemko, hisia na ushabiki pasipo kufanya costs benefit analysis! Kama tuna barabara nzuri ya lami kwenda morogoro tulihitaji treni ya mwendo kasi? Itahudumia watu wangapi ambao magari yameshindwa kuhudumia? Ni nani aliyetufanyia uchambuzi? Tatizo kuna mambo yanaamliwa bila kuwashirikisha wachumi kisa wengine ni wapinzani. Akili zote za nchi hii zinapaswa kutumiwa na rais wetu kujenga nchi yetu. Hakuna haja ya kubaguana, vyama vitakufa lakini nchi yetu itabaki.
Sasa kutokana na kukurupuka tumebomoa jengo la TANESCO pale Ubungo, tumebomoa nyumba nyingi sana kimara mpaka mbezi tukiwa tunapanua ili tujenge njia nane, halafu eti Leo namsikia Eng. Kamwelwe akitangaza bila hata hofu ya Mungu kuwa ujenzi umesimamishwa mpaka lini sijui. Tumewafilisi watanzania, wengine walifunga biashara na kufa, wengine wakakimbia jiji, wengine ikawa ndio mwisho wao. Hayo ndio maamuzi ya kukurupuka sana na madhara take ndio hayo. Tuache kujinasibu kana kwamba tunaweza kila kitu. Kama taifa lazima tuwe na vipaombele na mifumo imara. Tunajenga watu badala ya mifumo imara. Watu wanakufa na kupotea lakini mifumo imara itawanyoosha wote watakaingia. Marekani na nchi nyingine ziliendelea zimejenga mifumo. Hata akija chizi au mhuni mfumo unamwongoza. Tuwe na dira tuache mbwembwe.
Kwa chama changu cha mapinduzi (CCM) lazima sasa tubadilike. Tuandae mfumo bora na tuache tantalila nyingi kwenye masuala ya kitaifa. Tanzania siyo yetu ni ya Watanzania. Hatutaongoza milele, maisha na zama hubadilika. Kwa maisha na mwenendo wetu ni ngumu kujinasibu kama mfano bora.
Wabunge wetu wajifunze kujenga hoja na kutetea maslahi ya wanaowawakilisha.
Mungu ibariki Tanzania!
Selgius Ntechi
+255712124912