Dada Jane ameandika mambo mazito.Nape hujui wala hutaki kujua watu wameumia na kuhuzunika kwa kiasi gani kufuatia hukumu ya jana dhidi ya Lema.Wananachama,mashabiki, wafuasi ,viongozi CHADEMA na Watanzania wengine wengi wameumia sana..Binafsi uamuzi wa jana umeniumiza sana..umeniumiza sana.Je, kama wana CHADEMA wa ARUSHA MJINI wakiyapa uzito maneno yako hapa Jf na wakaamua kuanzisha vurugu utawalaumu?Hapana! utabeba lawama maana utakuwa umekuwa perpetrator wa violence.
Mwanasiasa makini na anayejitambua hujua aseme nini, wakati gani,kwa nini,ili iweje, kwa namna gani na kwa nani!watu wanakuona si mtu makini.Laiti ungekuwani mtu makini ungechagua kukaa kimya kaka.
Kwa mara ya mwisho,mwanzoni mwa miaka ya 2000, nilikufamu kama mtu mlokole,mwenye hofu ya Mungu na uliyependa kumtumikia Mungu..siasa ikakuvutia, ukaweka biblia chini!Mimi ni miongoni mwa watu ambao wewe Nape umepata kuwalea kiroho mahali fulani..Sasa humu JF unashutumiwa,mara kwa mara, kwa kusema uongo wa wazi wazi mchana kweupe, eti nyie ndani ya CCM mnauita propaganda!!wewe unaendekeza mizaha!wala huangalii hisia za wasomaji wako.Ninayo mengi ya kuandika,panapo majaliwa kesho saa nane mchana,kwa kuwa umenikera sana, nitaandaa thread mahususi kuhusu wewe ili watu wapate kukuelewa vyema.