Kauli ya mzee Mwinyi kwa CHADEMA imetimia

Kauli ya mzee Mwinyi kwa CHADEMA imetimia

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Igwe wanaJF,

Ajizi nyumba ya njaa, CHADEMA ikiongozwa na Kamanda wa anga kila kukicha wameendelea kuuthibitisha ulimwengu kuwa wao ni CCM B kwani sasa wameamua kutoipinga CCM katika chaguzi za marudio, sasa sio siri tena, kauli ya mzee Mwinyi kuwa CHADEMA ni CCM B imetimia.

Karibuni tujadili kwa hoja.
 
CHADEMA sasa inapumulia masikio badala ya pua. Tetesi za kuhama zimezagaa mahala mahala. Nasikia wanatafutana hawajui kesho anaondoka nani. Ufipa hakukaliki ni hofu tupu; watu hawaongei kila mtu anamuona mwenzake ni msaliti. Nasikia Wana mpango wa kulishana Yamini.
 
CHADEMA sasa inapumulia masikio badala ya pua. Tetesi za kuhama zimezagaa mahala mahala. Nasikia wanatafutana hawajui kesho anaondoka nani. Ufipa hakukaliki ni hofu tupu; watu hawaongei kila mtu anamuona mwenzake ni msaliti. Nasikia Wana mpango wa kulishana Yamini.
Duh, hali ndio imekuwa hivi?
 
tumefika pabaya sasa lakini kipo wanachokijua lakini hawako wazi kusema ukweli
Mku huyo mmoja aliyeomba kuchaguliwa na wenye Itikadi ya Chadema nao wamehama kuja kwetu ccm au ndo huyo mmoja ndo tunajisifu.Siasa ni Itikadi na itikadi ni imani iliyokamili inayoishi rohoni mwa watu.Kwa hiyo ni Imani kama zilivyo imani zingine hapa duniani hivyo basi wanachadema wa Siha bado wapo kama alivyowakuta na wataendelea kuwepo.
 
Tanesco kuna tatizo gani kwani amenipigia Mpangaji wangu ya kuwa leo ni siku ya tatu Yombo hakuna umeme .
 
Kususia uchaguzi si kuwa ccm b.badala yake ni kuuonyesha umma na dunia nzima jinsi siasa ya tz ilivyo
 
huu uamuzi wa kugombea kushiriki chaguzi wamewashirikisha wanachama wao au ndio mtindo wa kubadili gia angani.
Ni vyema maamuzi mazito kama hayo yakapata baraka za wanachama ambao kila siku wanawekwa ndani na sio kikundi cha watu wachache ingawa kipo kisheria
 
Ukiwa mbunge kupitia tiketi ya chadema unalazimishwa kukilipa chama nusu ya mshahara na posho zako kila mwezi. Pia kuna michango na harambee zingine kibao hadi unaona haina maana ya kuendelea kuwa mbunge, afadhali ukatafute kazi zingine. Mbaya zaidi pesa zinazoingia kwenye chama zinaliwa na wachache, zimeshindwa hata kujenga jengo la makao makuu lenye hadhi na badala yake kinapanga kwa gharama kubwa sana kwa kajengo ka mtu fulani. Lazima watahama wengi tu kuonesha disatification.
 
Mwanzilishi wa Chadema ameamua kurejea ccm ingawa mkwewe anamuomba asifanye hivyo.
 
Tena kama kuna mtu aliepokea rushwa basi ni mbowe aliamua kuuza majimbo na kata wala si wale waliojiuzulu!
 
Igwe WanaJF!

Ajizi nyumba ya njaa, Chadema ikiongozwa na Kamanda wa anga kila kukicha wameendelea kuuthibitisha ulimwengu kuwa wao ni CCM B kwani sasa wameamua kutoipinga CCM katika chaguzi za marudio, Sasa sio Siri tena , kauli ya Mzee Mwinyi kuwa Chadema ni CCM B imetimia.

Karibuni tujadili kwa hoja.
Mkuu kuna hoja gani tena, wakati mwenyewe umepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza, wengine tutasemaje?
Mfano wa timu mbili hasimu, moja inajiondoa kwenye mashindano dakika za mwisho!
Kitendo hicho huashiria nini?
Tena huyo master mind anayesababisha kugawa ushindi wa bwerere kwa timu hasimu, asilimia kubwa ni mamluki, ama anakuwa kahongeka.
Hivi hakuna wasomi "wazuri" kuweza kuanzisha ama kubuni chama cha upinzani chenye mrengo wa upinzani wa kweli na si aina hii ya vyama vya siasa za maigizo na kugawana ruzuku vilivyopo sasa, vinavyojiita vyama vya upinzani?
 
Tanesco kuna tatizo gani kwani amenipigia Mpangaji wangu ya kuwa leo ni siku ya tatu Yombo hakuna umeme .
Jaribu kucheki nao mkuu. Unajua Mtera mvua hazijanyesha. Bwawa kina kipo chini, ufuaji umeme bado chini. Kama unavyojua nchi yetu imepata uhuru miaka 56 iliyopita lakini sisi bado wachanga. Hata akili zetu unaziona. Hatuna lingine zaidi ya kupiga "sihasa" ambayo tunapoelekea itakuwa "sihaba"!
Na kumbuka, vijana tulio nao ndiyo hawa. Wametumbua mimacho kuangalia nani anadowea finyango nzuri kwa jirani. Pole ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom