Kauli ya Mbunge ‘yabezwa’

nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
a
bread_end.gif

KITAIFA
[h=1]
ico_plus.png
SHARE[/h]

nyambari.jpg

Na Diana Maningo

Posted Jumatano,Novemba28 2012 saa 10:11 AM

KWA UFUPI

“Kama imefikia hatua mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi tena wa chama tawala akitaka kuandamana na wananchi kuchoma mgodi maana yake, Serikali imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi” alisema Ngoto.KAULI ya Mbunge wa Jimbo la Tarime ya hivi karibuni katika mkutano na wananchi mjini Tarime, Nyambari Nyangwine kuwa ataandamana na wananchi wake kutoka Tarime hadi Nyamongo kwenda kuchoma moto mgodi wa Africa Barrick Gold Mine, endapo mgodi huo utashindwa kuwalipa fidia wananchi waliofanyiwa tathmini ili kuhama maeneo yaliyojirani na mgodi yaibua mapya.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Tarime, Lucas Ngoto amemtaka Mbunge wa Jimbo hilo la Tarime, Nyambari Nyangwine awaongoze wananchi wakiwa na mapanga kwenda hadi Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kudai X-Ray ambayo imekosekana katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa muda wa miezi 8 hali inayowalazimu wagonjwa kwenda mikoa ya jirani na nchini Kenya kupata huduma hiyo.

Ngoto alisema kuwa hashangai kusikia Mbunge Nyangwine akitaka kuandamana na wananchi kwenda kuchoma moto mgodi kwa madai kuwa huenda mbunge huyo kafanya hivyo baada ya kugundua kuwa Serikali imeshindwa kutatua kero zinazowakabili wananchi hususani wa Nyamongo ambao walifanyiwa tathmini na mgodi kuyahama maeneo ambayo mpaka sasa hawajalipwa fidia.Ngoto alisema kuwa kama kauli ya Mbunge Nyangwine ilikuwa ni ya uchochezi na kuhatarisha amani, kwani kama kiongozi alipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa aliongea mbele ya mkutano wa wananchi wa hadhara ambao ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali huku walinzi wa mkutano huo wakiwa ni Polisi.

“Kama imefikia hatua mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi tena wa chama tawala akitaka kuandamana na wananchi kuchoma mgodi maana yake, Serikali imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi” alisema Ngoto.

Ngoto alimtaka mbunge huyo kabla ya kwenda kuuchoma mgodi, yeye kama mbunge awaongoze wananchi wakiwa na mapanga hadi Wizara ya Afya kudai X-Ray kwa madai kuwa kukosekana kwa huduma ya X-Ray Hospitali ya Wilaya ambayo imesababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma,huku wagongwa wengine wakitumia gharama kubwa kwenda kupata huduma ya X-Ray mikoa jirani na nchi ya Kenya.

“Tunamtaka mbunge kabla ya kwenda mgodini atuongoze wananchi tukiwa na mapanga yetu hadi Wizara ya Afya kudai X-Ray, miezi 8 sasa hakuna huduma hiyo, mimi kama kiongozi wa Chadema nimefuatilia hospitalini tunaambiwa X-Ray ni mbovu na wahusika wa matengenezo ni wizara ambayo inadaiwa na kampuni inayotengeza X-Ray zilizoko katika hospitali za Serikali,” alisema Ngoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, Justus kamugisha alisema kuwa kwa upande wao kauli ya Mbunge Nyangine ya kuchoma moto mgodi haiwezi kuwaathiri kwa madai kuwa mbunge akifanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
6,691
Likes
17
Points
135
POMPO

POMPO

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
6,691 17 135
Hana lolote ni mnafiki sana Nyambali danganya toto
 
M

mwimbule

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Messages
500
Likes
51
Points
45
M

mwimbule

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2009
500 51 45
Asichome Mgodi dawa ajiuzulu ubunge na kuhama hilo lichama lake la CCM. Kwani matatizo yote ya nyamongo hayataisha bila kuwang'oa hawa wavaa nguo za kijani.
 
zema21

zema21

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
619
Likes
53
Points
45
zema21

zema21

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
619 53 45
a
bread_end.gif

KITAIFA
ico_plus.png
SHARE
nyambari.jpg

Na Diana Maningo

Posted Jumatano,Novemba28 2012 saa 10:11 AM

KWA UFUPI

"Kama imefikia hatua mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi tena wa chama tawala akitaka kuandamana na wananchi kuchoma mgodi maana yake, Serikali imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi" alisema Ngoto.KAULI ya Mbunge wa Jimbo la Tarime ya hivi karibuni katika mkutano na wananchi mjini Tarime, Nyambari Nyangwine kuwa ataandamana na wananchi wake kutoka Tarime hadi Nyamongo kwenda kuchoma moto mgodi wa Africa Barrick Gold Mine, endapo mgodi huo utashindwa kuwalipa fidia wananchi waliofanyiwa tathmini ili kuhama maeneo yaliyojirani na mgodi yaibua mapya.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Tarime, Lucas Ngoto amemtaka Mbunge wa Jimbo hilo la Tarime, Nyambari Nyangwine awaongoze wananchi wakiwa na mapanga kwenda hadi Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kudai X-Ray ambayo imekosekana katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa muda wa miezi 8 hali inayowalazimu wagonjwa kwenda mikoa ya jirani na nchini Kenya kupata huduma hiyo.

Ngoto alisema kuwa hashangai kusikia Mbunge Nyangwine akitaka kuandamana na wananchi kwenda kuchoma moto mgodi kwa madai kuwa huenda mbunge huyo kafanya hivyo baada ya kugundua kuwa Serikali imeshindwa kutatua kero zinazowakabili wananchi hususani wa Nyamongo ambao walifanyiwa tathmini na mgodi kuyahama maeneo ambayo mpaka sasa hawajalipwa fidia.Ngoto alisema kuwa kama kauli ya Mbunge Nyangwine ilikuwa ni ya uchochezi na kuhatarisha amani, kwani kama kiongozi alipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa aliongea mbele ya mkutano wa wananchi wa hadhara ambao ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali huku walinzi wa mkutano huo wakiwa ni Polisi.

"Kama imefikia hatua mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi tena wa chama tawala akitaka kuandamana na wananchi kuchoma mgodi maana yake, Serikali imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi" alisema Ngoto.

Ngoto alimtaka mbunge huyo kabla ya kwenda kuuchoma mgodi, yeye kama mbunge awaongoze wananchi wakiwa na mapanga hadi Wizara ya Afya kudai X-Ray kwa madai kuwa kukosekana kwa huduma ya X-Ray Hospitali ya Wilaya ambayo imesababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma,huku wagongwa wengine wakitumia gharama kubwa kwenda kupata huduma ya X-Ray mikoa jirani na nchi ya Kenya.

"Tunamtaka mbunge kabla ya kwenda mgodini atuongoze wananchi tukiwa na mapanga yetu hadi Wizara ya Afya kudai X-Ray, miezi 8 sasa hakuna huduma hiyo, mimi kama kiongozi wa Chadema nimefuatilia hospitalini tunaambiwa X-Ray ni mbovu na wahusika wa matengenezo ni wizara ambayo inadaiwa na kampuni inayotengeza X-Ray zilizoko katika hospitali za Serikali," alisema Ngoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, Justus kamugisha alisema kuwa kwa upande wao kauli ya Mbunge Nyangine ya kuchoma moto mgodi haiwezi kuwaathiri kwa madai kuwa mbunge akifanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Nasari alipotishia kujitenga alionekana ni mchochezi akaitwa polisi kuhojiwa lakini nyangwine alipotishia kuchoma moto anatetewa si mchochezi.........Hv hamjui kauli yake inahamasisha na kuhalalisha fujo?
 
N-handsome

N-handsome

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,337
Likes
141
Points
160
N-handsome

N-handsome

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,337 141 160
Serikali Sikivu Bwana
 
N

nemasisi

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2012
Messages
1,898
Likes
116
Points
160
N

nemasisi

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2012
1,898 116 160
Zamani wakati nasoma vitabu vyake kwenye literature nilidhani huyu mtu ni bonge la mwanamapinduzi, kumbe aaaah! Mweupeeee
 
K

Kichuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
320
Likes
0
Points
0
K

Kichuli

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
320 0 0
Kauli ya nasri ilikua ni ya cdm na kauli ya nyambari ni yake kama mkazi wa tarime anahaki ya kutoa kwa wapiga kura wake hivyo hajafanya kosa lolote la kuhojiwa polisi,
 
nashy

nashy

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Messages
679
Likes
2
Points
35
nashy

nashy

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2011
679 2 35
Police weakness, eti wanasubiri mgodi uchomwe moto ndo wachukue hatua, huu ni ukosefu wa akili na kutokua independent katika kufanya kazi
 
kizaizai

kizaizai

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Messages
2,979
Likes
1,555
Points
280
kizaizai

kizaizai

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2010
2,979 1,555 280
Zamani wakati nasoma vitabu vyake kwenye literature nilidhani huyu mtu ni bonge la mwanamapinduzi, kumbe aaaah! Mweupeeee
Vitabu vingi wanaandika Wasomi wengine ila wanatumia Jina lake Kibiashara.
 
B

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Messages
230
Likes
0
Points
33
B

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2012
230 0 33
Kauli ya nasri ilikua ni ya cdm na kauli ya nyambari ni yake kama mkazi wa tarime anahaki ya kutoa kwa wapiga kura wake hivyo hajafanya kosa lolote la kuhojiwa polisi,
we ni kichuli kwel, kauli ya NASARI haikuwa ya chama-cdm na ndio maana alipomaliza kuongea na mbowe ilpofika nafasi yake ya kuongea aliifuta ile kaul na kusema hiyo sio kauli ya chama kwani cdm kitawaunganisha watanzania wote kutoka kusin-kazikazin, kutoka magharibi - mashariki kwani ukombozi wa kweli ni lazima kuwausisha watu wote....na kwa nini ahojiwe nasari kama ilikuwa ni kauli ya chama.... na kitu kingine uwezi kutoa kauli za uchochezi eti useme ni kauli yake kama mkazi wa tarime, kama ndiyo hivyo kila mbunge angeenda jimboni kwake na kutoa kauli za uchochezi.....just think about that
 
Mwitongo

Mwitongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2009
Messages
311
Likes
49
Points
0
Mwitongo

Mwitongo

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2009
311 49 0
we ni kichuli kwel, kauli ya NASARI haikuwa ya chama-cdm na ndio maana alipomaliza kuongea na mbowe ilpofika nafasi yake ya kuongea aliifuta ile kaul na kusema hiyo sio kauli ya chama kwani cdm kitawaunganisha watanzania wote kutoka kusin-kazikazin, kutoka magharibi - mashariki kwani ukombozi wa kweli ni lazima kuwausisha watu wote....na kwa nini ahojiwe nasari kama ilikuwa ni kauli ya chama.... na kitu kingine uwezi kutoa kauli za uchochezi eti useme ni kauli yake kama mkazi wa tarime, kama ndiyo hivyo kila mbunge angeenda jimboni kwake na kutoa kauli za uchochezi.....just think about that

Hapo ktk wekendu, msiharibu lugha za watu. Hiyo kitu inaitwa KICHURI
 
B

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Messages
230
Likes
0
Points
33
B

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2012
230 0 33
Hapo ktk wekendu, msiharibu lugha za watu. Hiyo kitu inaitwa KICHURI

mkuu ilo ni jina na mimi quote jina kama lilivyo (kichuli) kama yeye mwenyewe anakosea jina analotumia mm nitamrekebisha vp
 
Forum statistics

Threads 1,238,390
Members 475,954
Posts 29,318,999