Kauli ya JK urais 2015 yazua mtafaruku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya JK urais 2015 yazua mtafaruku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima wa Kuku, Mar 2, 2012.

 1. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  * Yadaiwa inawazibia wenye uwezo, kusababisha mpasuko CCM
  Na Reuben Kagaruki
  Mwandishi Wetu

  SIKU chache baada ya gazeti moja la kila siku (sio Majira) kumnukuu Rais Jakaya Kikwete, akihadharisha watu wa umri wake kuachana na ndoto za urais mwaka 2015, kauli hiyo imepokewa kwa hisia tofauti na kuzua mtafaruku mkubwa miongoni mwa wanachama na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Rais Kikwete aliyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Kamati Kuu (CC), jijini Dar es Salaam na kusema kuwa, muda wake wa uongozi ukiisha, angependa nafasi hiyo ishikwe na vijana.

  Chanzo chetu kinasema kuwa, Rais Kikwete alisema watu wenye umri kama wake ambao wanataka urais, si wakati wao bali wa vijana kauli ambayo inadaiwa kuwanyong'onyeza baadhi ya makada wanaotajwa kutaka nafasi hiyo wakati umri wao umeenda.

  Rais Kikwete ametoa kauli hiyo wakati makundi mbalimbali ndani ya chama hicho, yakijipanga kwa ajili ya kusaka nafasi katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

  Akizungumza na gazeti hili mmoja wa makada wa chama hicho ambaye pia ni mjumbe wa CC, alidai kusikitishwa na kauli hiyo na kuhoji mantiki ya kuwabagua watu wenye umri kama wake katika nafasi hiyo ya juu.

  Kada huyo ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alisema haoni sababu ya Rais Kikwete kuwakatisha tama viongozi wa umri wake bila kuzingatia kigezo cha uwezo na sifa zao.

  Alisema kimantiki, hata yeye Rais Kikwete kwa umri atakaostaafu mwaka 2015, hatakuwa mzee na asingechaguliwa mwaka 2005, bado alikuwa na nguvu na uwezo wa kuwania nafasi hiyo pia asingejisikia vizuri kama angesikia kauli hiyo.

  Aliongeza kuwa, urais si kazi ya umri, kinachoangaliwa ni uwezo ambapo kauli ya Rais Kikwete, imeongeza mpasuko ndani ya chama hicho katika kinyang'anyoro cha urais na kama CCM haitakuwa makini, unaweza kutokea mgawanyiko mkubwa.

  "Karibu asilimia 100 ya watu wanaohusishwa na urais 2015 wana umri kama wa rais, hawa si watu wa hivi hivi tu, wana uwezo na rekodi kubwa kiuongozi ndani na nje ya chama.

  "Umri wao utakapotumika kama kigezo cha kuwahukumu wasipate nafasi hiyo, Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama chetu anakosea," alidai kada huyo ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.

  Kada mwingine wa CCM kutoka Kanda ya Ziwa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, alidai kusikitishwa na kauli hiyo kwa madai kuwa, inakigawa chama na kudhoofisha mshikamo uliopo.

  "Hii kauli inanipa hofu, kumbuka wale wenye umri kama wake wako wengi na wengine waligombea naye, sasa wakiamua waungane wawe kundi moja, waanzishe mtandao wao itakuwa ni hatari kwa chama chetu, kauli hii inaweza kufifisha chama na kukiweka pabaya kwa kuleta mgawanyiko," alisema kada huyo.

  Akithibitisha kuwa urais si suala la umri, aliwataja baadhi ya viongozi wa nchi za Zambia, Malawi, Afrika Kusini, Zimbabwe , Uganda, Sudani na zingine za Afrika kuwa zinaongozwa na watu wenye umri wa kutosha kabisa.

  Aliwataka wana CCM kujenga mshikamano zaidi na kutoruhusu mitazamo ya kuleta mgawanyiko ndani ya chama hicho.

  "Kama CCM itafanya mchezo huu, ikumbuke kuwa wapo wenzetu wanaotazama mtu kwa uwezo wake na si kwa umri kama CHADEMA, watatuadhiri hivi hivi, tuache mchezo," alionya kada huyo.

  MY TAKE:
  Naona vita vyake na Lowassa vimeshika kasi kwa upya. Je ataweza? Naona hatari ya Mkuu wa nchi kujiweka kwenye siasa za makundi namna hii hasa akijua kuwa hawezi kufanikiwa. Mmemsikia Zitto na Januari. Walitumwa, au waliamua wenyewe? Je, Rais anafahamu consequesncies za matamshi yake?
   
 2. assa von micky

  assa von micky Senior Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ccm hawana mtu anayeweza kusimama na kutoa uamuzi ambao kila mmoja akakubaliana nao.Watatapatapa hadi uchaguzi mkuu ufike ,watanzania tungekuwa na busara tungewapumzisha hawa wanaotapatapa....KIONGOZI SAFI HAWEZI KUTOKA CCM.Hata vijana wao wanamawazo ya kizee hivyo basi ujana anaousema jk ni upi ?
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ni maoni yake
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Aendelee tuu kuipasua CCM kwa kauli zake ili Anguko rasmi la magamba litimie!
   
 5. N

  Ntuya Senior Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja tuone mwisho wa haya mambo, mana mwisho u karibu sana.
   
 6. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tusijidanganye CCM ni zaidi ya uwajuavyo wewe subiri uone!
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ansayemsikiliza Kikwete na kutilia maanani kauli zake lazima hayupo sawa kichwani. Kwani kikwete anasema mangapi ambayo huwa anayageuka kabisa hadi kutia aibu? Kwani hamkumbuki pale alipotenga dk 45 za hotuba ya mwisho wa mwezi kueleza mpango wa kutenganisha biashara na siasa? Je 2010 alifanya nini? Si ndo akaingiza wafanyabiashara zaidi na kuwatosa wengine? Kikwete ni kiongozi wa aina yake, huwa haoni shida kutafuna matapishi yake upya na kuyameza.
   
 8. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tatizo CCM imejaa Minafiki mingi, na JK analijua hilo. Sasa kama hakuna wa kumkosoa anatamka ***** wao wanampigia makofi. Na kwa unafiki huo huo, yeyote miongoni mwao atakayejifanya kuchukua fomu ya kugombea urais atakuwa anampinga rais wao na atakuwa Msaliti! Itulie hivyo hivyo kama inanyolewa kama ilivyotulia sasa kwa kumwogopa binadamu mwenzao
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  URAIS WA KI-UDALALI, MBELEKO MBELEKO, UANAMTANDAO NA VIGEZO VINGINE UCHWARA VINAVYOZUIA DEMOKRASIA KUFANYA KAZI KATIKA UHALISIA WAKE NA KWA KUZINGATIA TAMADUNI ZA TAIFA LETU JUU YA HILO KAMWE HAYANA NAFASI 2015

  Mara nyingi mtatizo ya ki-utawala kwa Rais Kikwete ama ndani ya chama chake au ndani ya serikali yake yanatokea mra nyingi kuwa ni ya kujitakia mwenyewe hasa kwa kuokota mawazo ya barabarani na kuyarasmisha kinyume na matarajio ya watu na vyombo sahihi vyenye dhamana, mamlaka na madaraka kamili kuyafikia maamuzi ya kisera kama hayo.

  Ndio, nasema hiviii, hili la 'Urais kwa Majaribio kwa Umri wa Vijitoto' ni mfano hai wa matatizo ya kujitakia mwenyewe Rais wetu maana jambo hili wala si kitu rahisi kukublika kama anavyodhani ndani ya taifa lililofifishiwa matumaini kama hili la kwetu kwa mambo mengi kwenda kombo ki-uongozi. Hakika haya yote ni matatizo ya kujitakia kuzua mtafaruku baada ya mtafaruku na kuendeleza mipasuko ya ajabu ndani ya chama chake CCM.

  Baya zaidi, kitendo cha mwana-CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe kugeuka Chief Decision-Maker on all unpopular policy issues within Chama Cha Mapinduzi fraternity na makada wa chama hicho wakiwemo wabunge kujikuta hawajui hili wala lile bali tu hulazimika kufuata maamuzi yake hayo kwa Rais Kikwete, hili nalo huenda likawafanya Wana-CCM wenye dhamana ya kufanya maamuzi kama hayo ya kisera (Policy Decisions) sio tu kumchukia zaidi kada huyo wa CHADEMA bali zaidi huenda wakamgomea ki-aina Mwenyekiti wao CCM taifa pamoja na DHANA POTOFU WA 'KUFANYIA MAJARIBIO YA WATANZANIA ZAIDI YA MILIONI 48 KWA KUWEKA 'URAIS WA TAIFA HILI MIKONONI MWAO VIJITOTO'. Na kwamba hayo yote yafanyike kwa hisani na maelekeze ya akina Zitto Kabwe na Januari Makamba.

  Kiukweli maisha ya WaTanzania kufanyiwa nayo majaribio zaidi tena baada ya lile jaribio la dhana ya USPIKA KWA MISINGI YA JINSIA YA MTU kutuangukia vibaya mno kule bungeni, Umma wa Tanzania tunasema kwa kauli moja kwamba HAKIPITI KITU HAPA mpaka kupigiwa kura ya maoni kitaifa tena chini ya Tume Huru ya Uchaguzi ili sisi wenyewe wananchi wenye nchi hii tukayatolee maamuzi ya mwisho Contencious Constitutional issue kama hiyo na wala si vinginevyo.

  Hakuna kuburuzwa mtu tena kwa mawazo ya kutoka kwenye ndoto ya mtu mmoja usingizini kwake kutwishwa kwenye mabega ya WTanzania karibia milioni 50 kulifuata tu kama kondoo bila kuhoji juu ya malengo yake na faida na hasara zitakazotokana na mambo kama hayo.

  Binafsi naamini kwamba nchi yetu imekua ya amani wa kuigwa si ki-ajali tu bali ni kufuatia ukweli kwamba kuna baadhi ya mambo TULIJIZUIA KUJIINGIZA KAMA TAIFA, kama vile kuendekeza Urais KWA MISINGI WA UMRI WA 'VIJITOTO, Urais kwa misingi ya Dini ya mtu, Urais Kwa kufunuana nguo kuangalia kwanza JINSIA WALIZOUMBWA NAZO WATU, na vile vile hivi sasa tunaongeza kwenye orodha hiyo kujikatalia Urais wa Mbeleko kule kubebew tu mtu ndani ya gunia na watu kujistukia tu tumebwagiwa hata yule tusiemdhania kabisa ikulu Magogoni.

  Rais wa JMT wa vipindi vijavyo watapatikana kwa kura ya wananchi moja kwa moja bila udalali wa ki-mbeleko mbeleko cha 'mwenzetu mara mwanamtandao' na kupitishwa kwa zengwe na ghiliba nyingi, urais wa aina hiyo haina nafasi tena katika Tanzania tunayoitaka mara baada ya Rais Kikwete; rais ajaye safari hii atapatikana kwa misingi yaUADILIFU, USHINDANI WA KUFA MTU, MHUSIKA MWENYEWE KUJINADI ANACHOKIFUATA IKULU na wla si mtu kutuletea tu vijivigezo mara usikie ooh safari hii KIGEZO ni mpaka mtu atoke mkoa wa Mwanza au Zanzibar ndio agombee urais.

  Nasema hiviiiii, tuache kabisa mizaha katika taasisi hii kubwa aajabu na yenye kubeba matumaini ya mamilioni ya watu katika nchi na sasa kuanza kuliangalia sawa tu na cheo cha U-Katibu Kata vile.
   
 10. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh! mwishowe tutamwita Slaa kwa mazungumzo ya faragha kama Karume

  Usitake nnncheke mie...
   
 11. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
 12. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  yeye alichaguliwa akiwa na umri mdogo kwa mtazamo wa watanzania mwaka 2005.nikipi alichokifanya kizuri kwa umri huo? Mbona anajiingiza kwenye marumbano ya uraisi na ilihali alikataza wana magamba kusaka uraisi kwani ni mapema mno?
   
 13. C

  Chintu JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
   
 14. m

  matawi JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja 100%
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Jk anapima kina cha maji kwa Lowassa? Atalijua jiji.
   
 16. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
   
 17. M

  MYISANZU Senior Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeye anawataka H.Mwinyi au Nahodha urais 2015.JK NI MDINI SANA.
   
 18. MZEE WA ROCK

  MZEE WA ROCK JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 623
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  myisanzu; umeona hee!!!!!!! JK bwana ana mamboooo, mm nadhani jk tutamkumbuka tu kwa sababu lazima iandikwe kulikua na awamu ya nne ya urais and not els
   
 19. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Magamba hata waweke kijana hamna kitu hapo. 2015 ni Slaa tu!
   
 20. k

  kamaudoulton Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  • Ben Mkapa alipata Urais akiwa mzee wa zaidi ya miaka 60: PERFORMANCE yake ilikuwa nzuri na ya kukumbukwa na Watanzania (uchumi ulikua, mfumuko wa bei ulidhibitiwa nk)


  • Jakaya Kikwete alipata Urais akiwa "kijana" wa miaka 49: PERFORMANCE yake inajulikana na kila Mtanzania (uchumi umedorora, mfumuko wa bei juu toka 7% mpaka zaidi ya 20% nk). JAZA MWENYEWE!
   Tunachotaka ni uwezo wa mtu kuongoza ili tutoke kwenye janga hili na siyo umbile, jinsia au umri wa mtu. CCM ifanye kosa hilo kama la kumteua Makinda kuwa Spika kwa msingi wa jinsia na siyo uwezo; idiriki kumteua ati alimradi kijana (Nahodha, Mwinyi, Ridhiwani, Nchimbi nk), basi SLAA (na uzee wake) NI RAIS 2015 bila upinzani mkubwa. CCM mpo hapo?
   
Loading...