Wakuu habari za jioni
Hivi kauli ya jiwe kuwa yule mfanyabiashara mwenye mtaji usiozidi million 4 asibugudhiwe na mamlaka husika, mimi naona haijakaa vizuri. Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa katika mazingira haya ya utitiri wa kodi na tozo zisizo kuwa na kichwa wala mkia mfanyabiashara anaweza kutumia mwanya huo kuweka dukani bidhaa ambazo thamani yake isizidi million nne kadiri ya jiwe na hivyo kukwepa kodi na akaamua bidhaa zake kuficha stooni ambako ni yeye na mkewe tu wanajua.
Alichopaswa jiwe kuwaambia wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na mamlaka zinazohusika na ukusaji kodi ni kutengeneza mfumo ambao utawatambua wafanyabiashara wadogo ambapo ingekadiriwa kuwa kwa mfanyabiashara mdogo ambaye kipato chake kwa mwezi/mwaka ni kiasi fulani basi hatawajibika kulipa kodi au tozo fulani kwa mamlaka husika, hii ingeleta uwazi fulani katika mfumo mzima wa ulipaji kodi, lakini kwa kutumia kigezo cha Capital inayoonekana dukani kuwa huyu mfanyabiashara mdogo asibugudhiwe basi serikali ijiandae kukosa mapato. stand to be corrected.
Nawasilisha