Kauli ya Godbless Lema na CHADEMA ni kuwadharau wahanga wa bomu Arusha.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Akizungumza katika maadhimisho ya "siku ya kumbukumbu" ya mauaji ya watu wanne na wengine kujeruhiwa yaliyosababishwa na bomu Juni 15, 2013 yaliyofanyika mkoani Arusha, Godbless Lema alidai kitendo hicho lilitekelezwa na polisi na ushahidi wanao na inazidi kuthibitishwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kukataa kuunda tume huru ya kimahakama walikoahidi kukabidhi ushahidi wa picha za mnato na video.

“Kwa kipindi cha mwaka mzima sasa tunaimba iundwe tume huru ya kimahakama, lakini haiundwi. Rais na viongozi wa serikali wako kimya kama vile wale waliokufa na kujeruhiwa pale Soweto si Watanzania,” alisema Lema.

ANGALIZO:
Kuna angalizo moja lisemalo, "mtu yeyote akikueleza jambo la kijinga na akafahamu kabisa jambo analokueleza ni la kijinga nawe pia ukalikubali jambo hilo, basi atakudharau sana".

Baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA wanawadharau sana wananchi.

Viongozi wakuu wa CHADEMA wanapoenda mbele ya familia, ndugu, jamaa na marafiki wa wahanga wa mlipuko wa bomu na kuanza kuwaeleza kuwa wana picha za video na mnato lakini hawawezi kuwaonyesha mpaka tume iundwe, ni dharau na kejeli isiyohesabika na kukubalika katika jamii endelevu.

Hii ni sawa na mtu aliyempa hifadhi mtu anayemfahamu ni muuwaji lakini badala yake anaenda kuwaambia wafiwa kuwa hawezi kuwaonyesha picha ya muuwaji mpaka vyombo vya sheria vimuulize.

Ni huyu huyu Godbless Lema aliyeweza kutoa photocopy nyingi za picha mnato zilizokuwa zinamuonyesha mtu mwenye sura inayofanana na yake akilawitiwa na akazipeleka kwenye mkutano wa hadhara huku akiambatana na mke wake na kufikia hatua ya kumpandisha Jukwaani Mke wake [Neema] ili azigawe picha hizo bila ya kutaka tume au taasisi ya serikali ifanye kwanza uchunguzi kama ilivyotangazwa kwenye thread hii,
Kwa nini kwa sasa asifanye hivyo pia kwenye video na picha mnato anazodai anazo na zinazowaonyesha watu wabaya waliofanya mauwaji ili jamii itoe hukumu kwa kutumia court of public opinion?.

As we all know, to know the offender would give affected community the opportunity to locate and bring the offender to justice. CHADEMA is denying justice to the family affected by bomb blast. CHADEMA is playing politics to peoples life for gullible political gain.

Kuna nini nyuma ya pazia au ndiyo mwendelezo wa siasa za kilaghai kwa faida ya siasa za muda mfupi.

Kila siku tunasema, CHADEMA kimejengwa katika misingi ya kilaghai. Maneno na matendo yao ya kitapeli ni zaidi ya dharau kwa wananchi.

Historia ya matendo ya Godbless Lema na CHADEMA kama nilivyoelezea hapo juu yanaonyesha kama kweli wangekuwa na video na picha mnato wasingesubiri uundwaji wa hiyo tume wanayodai ili wazitoa picha wanazodai wanazo.
 
Video itatatowa rais atakapounda tume.

Umefurahiiiii mwenyewe washirika wenu wa CCM kina Mwanadiwani kuinanga CHADEMA...Acha umalaya wa kisiasa kijana..............By the way CHADEMA inajua kuucheza huu mchezo...mtasubiri sana
 
mimi naona mwanadiwani rais angeunda hiyo tume ya kimahakama ili chadema waumbuke kama ilivyokuwa katika Hati ya muungano ilivyoletwa Baraza la katiba. Kukaa kimya ndiyo yote hii inatokea.
 
Haya ni mojawapo ya majambo ya kijinga kutoka kwa watawala:

- Pigeni tu.
- Nyie mnaweza kutengeza juice tu.
- Hata mkila majani
- Hakuna division zero
- ...............
- ...............
 
Sikiliza MwanaDiwani

Hii ni dalili ya wazi kuwa CCM mnawindwa na hatia. The guilty are always afraid. Na kadri mnavyotoa maneno kama haya mnazidi kuichokonoa damu ile mliyoimwaga kwa ukatili wa hali ya juu.

Wananchi wanajua...uoga na hofu waliyonayo viongozi wa CCM iwapo ukweli wa tukio lile ukijulikana. Serikali ya CCM itaanguka kwa mambo mengi sana.

Wananchi wanajua kwamba CCM na baadhi ya watendaji wake, wakiwemo wa Vyombo vya dola wangekuwa hawahusiki, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM angeshaunda Tume ya Kimahakama/ Kijaji ili ukweli ujulikane na haki itendeke.

Wananchi wanajua kuwa Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ameshindwa kutumia mamlaka ya kikatiba aliyoapa kuilinda, kwa sababu tu anajaribu kusogeza aibu na anguko la CCM kutokana na umwagaji wa damu ambayo sasa mmeamua kuifanya kama ndiyo sera yenu mbadala ya kusukuma siku zenu madarakani.

Kila mtu makini anajua kuwa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiunda Tume ya Kimahakama/ Kijaji itakayofanya kazi ya kuweka ukweli hadharani na kusaidia haki kutendeka, aibu atakayolazimika kuikabili kama kiongozi mkuu itakuwa haina mfanowe!

Itakuwa ni aibu kubwa kuliko waliyoipata Serikali ya CCM kwa kuhusika na mauaji ya Daudi Mwangosi kama ambavyo Ripoti tatu za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (chombo cha serikali), Kamati ya Nchimbi, na Kamati ya Jukwaa la Wahariri na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT) zilivyothibitisha kwa ushahidi wahusika wa mauaji hayo!

Rais Kikwete ameshindwa kutumia mamlaka ya kikatiba aliyonayo kwa niaba ya wananchi kuunda Tume ya Kijaji/Kimahakama kuhusu tukio mlipuko wa bomu la kivita pale Soweto, kwa sababu anajua aibu watakayoipata Serikali ya CCM itakuwa ni kubwa kuliko ile inayowakabili hadi leo kwa mauaji ya Januari 5 pale Arusha kama ambavyo Ripoti ya THUT (chombo cha serikali) imeonesha kwa ushahidi uhusika wa Serikali ya CCM na watendaji wake kukatili maisha ya watanzania kadhaa kwa risasi za moto!

Umwagaji wa damu mnaoendelea kuufanya kama mlivyofanya siku ya Juni 15 mwaka jana, utaendelea kuwatafuna. Damu ya watoto wale waliokuwa wametoka madrasa kujifunza ilimu ahera haitawaacha mkiwa huru asilani abadani.

Damu ya mwanamke yule iliyomwagika bila hatia yoyote bali kwa mapenzi ya watesi wa CHADEMA, itaendelea kuwawinda na itawakamata tu inshallah.

Machozi ya wazazi wa watoto wale, machozi ya wategemezi wa mwanamama yule, machozi ya ndugu, jamaa na wote waliolia kwa ajili ya tukio lile, yanatembea na viongozi wenu waliopanga hila ya jambo lile la ukatili.

Machozi ya wote wanaolia hadi leo, wakikumbuka marehemu wale, wakikumbuka pengo walilonalo kutokana na ukatili ule, wakikumbuka namna walivyobaki na ulemavu wa kudumu maishani mwao, hayatawaacha mkiiwa salama!

Jasho la wote walionusurika kwa kukimbia, jasho la wote waliojitolea kukimbiza majeruhi hospitalini, jasho la wote waliojihimu kwenda kutoa msaada wa hali na mali kwa majeruhi na wafiwa, limeshawapatia alama ya kudumu mnayotembea nayo mioyoni, rohoni, akilini na mwilini. Damu ya mtu si maji ya kifuu cha nazi unayoweza kuyamwaga tu upendavyo!

Mna hofu ya nini kuunda Tume ya Kijaji/Kimahakama? Kama mmejiaminisha kuwa CHADEMA hawana ushahidi si ndiyo wataumbuka?

Katika hili tambueni, mkifikiri mnapmabana na majina ya watu kama ulivyoyataja au mkifikiri mnapambana na CHADEMA na kujitia uhayawani wa kuendelea kuandika maneno ya kukejeli kama haya, kwanza mnazidi kudhihirisha kuwa ninyi ni INTARAHAMWE kweli...sasa baada ya kuzoea 'kula' damu za watu, mmeshazoea. Mmeamua kufuga mzinga kabisa! Lakini pia mnaongeza hasira zinazotokana na ukatili mlioufanya.

Wala msifikiri kuwa si katika tukio hilo pekee CHADEMA wameomba Rais atumie mamlaka yake ya kikatiba kuhakikisha ukweli unajulikana na haki inatendeka na hatua stahiki za kinidhamu na kisheria zinatolewa. Yako matukio mengine kadhaa.

Mnaogopa nini kuunda Tume ya Kimahakama/Kijaji hata kwenye tukio lile la Ndago, Iramba Magharibi, Singida ambako aliyefariki alikuwa ni Kiongozi wa UVCCM? Mnaogopa yule kiongozi wenu aliyetuma vijana kwenda kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe mkutano wa CHADEMA ataumbuka? Mbona tayari Watanzania wanamjua kama mmoja wa wapanga njama za kigaidi! Mnajulikana kwa kauli na matendo yenu!

Mnaogopa nini kuhakikisha ukweli unajulikana na haki inatendeka kwenye tukio la kuuwawa kwa Mbwana Masoud pale Igunga, Tabora. Au kwa sababu mnaogopa mtajulikana namna mlivyomteka, kumtesa na kumuua kikatili ikiwemo kwa kile kinachoonekana kunyongwa na kutobolewa macho!

Mnaogopa nini kuchunguza kifo cha Ally Singano Zona pale Morogoro? Au mnajua mlichokifanya kwake, hadi mkaleta msamiati wa 'kitu kizito chenye ncha kali'. Haya yote yana muda tu! Woga wenu unatoa uthibitisho uso shaka namna mlivyoamua kuwa majahili na malipo ya majahili kama ninyi yanajulikana!

Hapo hatujakumbushia mliyofanya Januri 2000 kule Zanzibar, hapo hatujasema mliyofanya kwenye Operesheni Tokomeza jinsi mlivyotokomeza uhai na maisha ya watu!

Viongozi wa CCM, chama hicho na serikali yake, will always be hunted and haunted and you will never get out of this mercilessness
. That is principle. Kama mlishaingia ndiyo hamtoki tena.

Unataka tuongezee?

Makene
 
ushaingiza siku, watoto wataenda chooni
Ndugu, nieleze pia jinsi ya kutoa siku!.

Haya masuala ya kuingiza siku wala hayahitaji mjadala katika jukwaa la siasa. Kuna jukwaa la Ujasiliamali linachambua masuala kama haya.
 
Umefurahiiiii mwenyewe washirika wenu wa CCM kina Mwanadiwani kuinanga CHADEMA...Acha umalaya wa kisiasa kijana..............By the way CHADEMA inajua kuucheza huu mchezo...mtasubiri sana

Mkuu nilichosema ni sahihi au si sahihi? Pengine ungeanzia hapo badala ya kunilaumu bure.
 
Ndugu, nieleze pia jinsi ya kutoa siku!.

Haya masuala ya kuingiza siku wala hayahitaji mjadala katika jukwaa la siasa. Kuna jukwaa la Ujasiliamali linachambua masuala kama haya.

Usanii wa Ccm hauna tena Nafasi hasa Arusha.

Mtela Mwampamba ni kiroboto anayejaribu kuingiza senti kupitia propaganda dhidi ya Upinzani ila hawezi.

Akumbuke alipo SHAIBU AKWILOMBE kisiasa na uchumi.
 
mimi naona mwanadiwani rais angeunda hiyo tume ya kimahakama ili chadema waumbuke kama ilivyokuwa katika Hati ya muungano ilivyoletwa Baraza la katiba. Kukaa kimya ndiyo yote hii inatokea.
Ndugu, hoja hapa siyo kuumbuka kwa chama chochote cha siasa. Maisha ya binadamu hayapimwi kwa kigezo cha chama ndiyo maana hata jukumu la kuangalia maisha ya binadamu liko kwa binadamu wenyewe wakisaidiana na taaisisi iliyopewa mwanvuli wa kisheria.
 
Ndugu, hoja hapa siyo kuumbuka kwa chama chochote cha siasa. Maisha ya binadamu hayapimwi kwa kigezo cha chama ndiyo maana hata jukumu la kuangalia maisha ya binadamu liko kwa binadamu wenyewe wakisaidiana na taaisisi iliyopewa mwanvuli wa kisheria.

Mwamvuli wa Kisheria ndo huo huo unaovuja damu..

Ccm wameutoboa toboa.

Ccm wamefikia hatua mbaya

Ngoja nijiandikishe kupiga kura upya kwani mmechakachua daftari.

Wassira na Lukuvi ..watetezi wa Serikali hawana jipya tena.
 
Mwaka huu ni wa shetani ........mna hali mbaya sana sana ......
Ndugu, tunaongelea psychological torture ya ndugu, jamaa na marafiki ambao wanasubiri hata kuziona picha tu za watu waliotenda maovu kwa loved one wakati viongozi wa CHADEMA kama Godbless Lema wameziweka video na picha kwenye kabati la mafaili yao kama souvenir.

Rudi kwenye hoja ya msingi na kama unadhani hakuna hoja, basi hata kusoma na kuondoa nayo kimantiki ni kuchangia hoja.
 
MwanaDiwani, hebu tupe wanaukumbi sababu moja tu kwa nini Kikwete anasita kuunda tume! Anaogopa nini? Hapa mwenye dharau kwa wafiwa ni nani? Huo ushahidi wewe unataka utolewe kwa nani? Wale wake watuhumiwa? Siku zote mimi najua ushahidi unatolewa makamani...sasa wewe watakaje? Eti muuaji apewe ushahidi? Ili iweje?
 
Last edited by a moderator:
Hamuwezi kuleta jambo jipya? Can't you be a little bit creative? You are disgusting MwanaDiwani. Kutwa kucha ni Chadema tu?


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Last edited by a moderator:
Umefurahiiiii mwenyewe washirika wenu wa CCM kina Mwanadiwani kuinanga CHADEMA...Acha umalaya wa kisiasa kijana..............By the way CHADEMA inajua kuucheza huu mchezo...mtasubiri sana
Ndugu, hakuna anayekinanga CHADEMA.

Mimi ninausema ukweli ndani ya mantiki ya maneno na matendo kama yanavyoakisi historia ya baadhi ya maneno na matendo ya viongozi wa CHADEMA.

Kama Mbunge anaweza kutoa picha zinazoonyesha mtu mwenye sura inayofanana na yake akilawitiwa bila hata ya kutaka uchunguzi kwanza ufanyike, kwa nini asiweze pia kutoa photocopy ya picha zinazowaonyesha wauwaji wa raia wasio na makosa bila ya kutaka pia uchunguzi.

Hii ndiyo mantiki ya hoja yangu.
 
Hamuwezi kuleta jambo jipya? Can't you be a little bit creative? You are disgusting MwanaDiwani. Kutwa kucha ni Chadema tu?


Sent from my iPhone using JamiiForums app
genekai

You are giving them a test of the time!

They stopped being creative long time a go for good will kuwatumikia wananchi rather than creating ufisadi, ufisadi and ufisadi from one to another, na sasa mauaji kama haya ambayo wanakuja kuyaandikia maneno ya kejeli kama hizi wanazofanya akina Nape Nnauye na Kinana.

They can't stretch their brains little bit more for the wananchi!

All they do nowadays...is exposing themselves how much insensitive they are to the issues and interests of the wananchi.

Hofu ya kuuona mlango wa kutokea....kutoka madarakani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom