Kauli ya CUF dhidi ya suluhu ya Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MPANGO WA KATIBU MKUU WA CUF MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD WA KUTAFUTA SULUHU YA MGOGORO WA KISIASA WA ZANZIBAR ALIOUTANGAZA JUZI HUKO MAREKANI INAYOTOLEWA LEO JUNI 17, 2016 NA MNADHIMU WA KAMBI YA CUF KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALLY SALEH (MB)

Ndugu Waandishi wa Habari,
Hivi sasa Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye ni Rais wa Nyonyo za Wazanzibari aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana huko Zanzibar yupo katika ziara ya kimataifa nchini Marekani na Canada.
Ziara hiyo imefanywa kwa makusudi ili chama chetu kipaze sauti katika juhudi yetu ya kupaza sauti mbele ya jumuia ya kimataifa kuwaelezea yaliojiri Zanzibar na yanayoendelea kujiri ikiwa ni sehemu ya kupigania haki yetu ambayo tunaamini inshallah itarudi mikononi mwetu.
Maalim Seif pamoja na sehemu nyengine mbali mbali na kuonana na viongozi wa kiserikali wa nchi hizo, basi pia amefika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York ili kupaza sauti yetu juu ya dhulma iliyofanyiwa CUF na kuishitaki Serikali ya Rais John Pombe Magufuli ambayo imepuuza kilio cha CUF.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete ndio iliyoiweka madarakani Serikali haramu ya Dk Ali Muhammed Shein na Dr. Magufuli ndie anayeilinda hivi sasa kwa kisingizio cha kufungwa mikono kikatiba.
Ndugu Waandishi
CUF inazidi kusisitiza kuwa dhulma inayoendelea hadi sasa kwa Polisi kukamata watu ovyo na kupiga mabomu ya machozi hata juzi usiku, kukamata watu ovyo, lawama yote ya haya anabeba Rais Magufuli na tunaunga mkono hatua ya Maalim Seif kuuelezea ulimwengu juu ya hilo pale alipohojiwa na kipindi cha Televisheni cha Voice of America kupitia mtangazani Shaka Ssali.

Ndugu Waandishi

Wabunge wa CUF kwa kipekee kabisa wanaunga mkono tamko la Malaim Seif kuelekeza kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa ulipo Zanzibar hivi sasa ambapo CUF inaigomea Serikali ya Dr. Shein.
Wabunge wa CUF wanampongeza Maalim Seif kwa kufungua milango ya kuwezesha kuanzwa kwa mchakato wa kutufuta suluhu huko Zanzibar yote akiwa na mapenzi na nchi yake na tunataraji kuwa watawala wa Zanzibar na wa Serikali ya Muungano watapokea hatua hiyo ya Maalim Seif.
Maalim Seif ameelezea juu ya Mpango wa Hatua 6 (Six Point Plan) wa kuitoa Zanzibar katika jinamizi liloinamia hivi sasa ambao ni kama huu ufuatao:
1. Kuundwa kwa Serikali ya pamoja ya muda
2. Serikali hiyo kuwa ni ya kitambo cha miezi 6
3. Serikali hiyo kuongozwa na Mzanzibari asiye na muelemeo wa kisiasa na anayekubali na pande kuu za kisiasa Zanzibar
4. Kuandaliwa uchaguzi mwengine Zanzibar ndani ya kipindi hicho cha miezi 6
5. Uchaguzi huo usimamiwe na jumuia za kimataifa
6. Kuheshimika kwa matokeo ya Uchaguzi huo kwa mujibu wa sauti ya umma
Ndugu Waandishi

Hatua hii ya Maalim Seif inadhihirisha umahiri wake katika siasa, moyo wake wa kuipenda Zanzibar na ujasiri wake wa kufanya maamuzi magumu na ndio maana tukaona haja ya kumuunga mkono ili kuipaza sauti yake hiyo ya kusaka suluhu ya Zanzibar isikike na Watanzania wote.
Tunaamini kuwa Wazanzibari na Watanzania walikuwa wakisubiri kwa hamu hatua hii ya Maalim Seif ya Chama cha CUF kutoa pendekezo la kuitisha mazungumzo ili kuanza kulikabili suala hilo la Zanzibar kwa maslahi ya Wazanzibari na amani na utulivu wa Watanzania.
Ni imani yetu kuwa karibuni tu tutasikia kauli ya Serikali ya Muungano na watawala wa Zanzibar juu ya pendekezo hili la Maalim Seif kwa sababu hakuna njia yoyote ya kupata suluhu ya Zanzibar bila mazungumzo ya kukaa mezani na CUF imefungua mlango kama ilivyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa 1995 na pia baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2000 na kupatikana muwafaka kwa faida kubwa ya Wazanzibari.

ALLY SALEH (MB)
MNADHIMU WA KAMBI YA CUF
Bunge la Jamhuri ya Muungano

Ally Saleh +255 777 4300 22
BBC Correspondent 1984-2011
 
Duuu...rais wa NYONYO za wazanzibari....hii kali
 
Please, hebu jaribu kupanga vizuri taarifa yako ili isomeke na kueleweka kwa ufasaha.

Sina hakika kama taarifa hii inasomeka na kueleweka. Labda ni kwa sababu imewasilishwa kwa kiswahili cha kizanzibari!
 
Hongera sana Maalim Seiff kwa jitihada zako za kisiasa tokea ukiwa Waziri kiongozi na hata pale ulipotofautiana na Mwalimu Nyerere kipindi kile mpaka ukawekwa korokoroni miaka mitatu ,Dunia ikapiga kelele ukaachiwa na kisha ukaanza siasa za upinzani na akina James Mapalala , kwa hakika historia yako ni ndefu katika siasa za Zanzibar

Swala gumu na fikra ngumu ni je Zanzibar hakuna mwanasiasa anayeweza kuvaa viatu vyako kuendeleza azma ya chama chako...? muda umefika sasa wa kumpata atakayerithi mikoba yako ya kisiasa.
 
Hapa ndipo tunapopotelea,yaani kila kitu tunasubiri ccm ituamulie,what is ccm by the way?
CCM ndiyo chama tawala mind you! wamarekani lazima wafanye tafiti zao wenyewe kama kweli cuf ni chama kinachostahili kutawala bila kuleta madhara kwa taifa na dunia in general. Kumbuka wamarekani walimuamini saaana Morsi aliyekuwa rais was ma Pharaoh kumbe alikuwa na siasa hatari,know that once bitten twice shy! Hamas walishinda kura through the ballot box na wakapata sifa sana but alas, kumbe Hamas wa siasa kali, Fatah ndiyo CCM kule Zenj na CUF ndiyo Hamas, from this logic get your own conclusion as to why CCM should continue ruling Zenj so as to avert the Egyptian and Hamas Muslim Brotherhood ideologies, I stand to be corrected for the betterment of Tanzanian tranquility.
 
Katiba yenu inasemaje? Sababu sioni sioni taasisi wala taifa la kuingilia maamuzi haya wameshindwa Burundi sembuse Bongo? Marudio ya trh 25 tuliambiwa ni ufujaji Wa pesa za walipa kodi marudio yanayodaiwa sasa hela atatoa Nani?
 
CCM ndiyo chama tawala mind you! wamarekani lazima wafanye tafiti zao wenyewe kama kweli cuf ni chama kinachostahili kutawala bila kuleta madhara kwa taifa na dunia in general. Kumbuka wamarekani walimuamini saaana Morsi aliyekuwa rais was ma Pharaoh kumbe alikuwa na siasa hatari,know that once bitten twice shy! Hamas walishinda kura through the ballot box na wakapata sifa sana but alas, kumbe Hamas wa siasa kali, Fatah ndiyo CCM kule Zenj na CUF ndiyo Hamas, from this logic get your own conclusion as to why CCM should continue ruling Zenj so as to avert the Egyptian and Hamas Muslim Brotherhood ideologies, I stand to be corrected for the betterment of Tanzanian tranquility.
Naamini wameshafanya tafiti za kutosha kuliko tunavyofikiria kuhusu chaguzi za Zanzibar toka zilipoanza. Ukifuatilia zaidi utaliona hilo. Changamoto hapa zaidi itakua je CCM watakubaki wakati wanajua kua wakiingia kwenye uchaguzi watashindwa tu. Muamuzi wa mwisho hapa kwa faida ya Tanzania ni Raisi wa Muungano. Hii ni changamoto kwake kutambulika zaidi kimataifa na kuirudishia Tanzania sifa yake kimataifa.
 
Mbona wameshajibiwa tangu juzi!Naona wanahangaika tu. wasubiri 2020. Zanzibar hakuna mgogoro naona wanapiga ngoma na kuicheza wenyewe
 
Mambo ya muungano CUF siku zote wamekuwa wakidai yapunguzwe na wangependa zaidi muungano uwe wa mkataba au serikali tatu.

Katiba yetu ya sasa kwa shinikizo la Seif na CUF yake iliondoa masuala ya uchaguzi wa serikali ya Zanzibar kwenye mambo ya muungano, hivyo Zanzibar ikaanzisha ZEC ambacho si chombo cha muungano. ZEC inatawaliwa na katiba ya serikali ya Zanzibar. Serikali ya Muungano haina mamlaka nayo.

Sasa kipi hapo hamkielewi rais wa serikali ya Muungano akisema mikono yake imefungwa na katiba wakati nyie wenyewe ndiyo mliomfunga?
Mwache tu maalim aendelee kuwa rais wa NYONYO kama ulivyoandika hapo juu, na huyo shein sijui mnamuita rais wa kitu gani?
 
Viongozi wa upinzani wanatakiwa nao waamini kwamba wapo wanachama wa upinzani wanaofaa kuongoza vizuri tena zaidi ya waliopo! Imekuwa maalim Seif, Mbatia, SijuiLipumba..( sorry sijui nani anapewa hii nafasi) kila wakigombea hawapati..lakini CCM imeshabadilisha wagombea wapya awamu Tano.. kama kweli wana nia ya kuleta demokrasia ya kweli kwenye vyama vyao.. waliopoo wastahafu na kuwapisha wengine vingine ni Kuendelea kukonga 'Nyoyo" za wananchi na matumbo yao badala ya "nchi". Tunaona kwenye demokrasi zilizoendelea mgombea akijaribu mara moja au mbili akashindwa anajiuzulu na wanachaguliwa wengine wenye mawazo na mikakati mipya. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
 
Kama CCM kweli wanafikiria maslahi mapana ya Taifa kuliko maslahi binafsi ya chama Chao, hawawezi kupuuza mapendekezo haya mapya aliyoyatoa Maalim Seif kama njia ya kuikwamua Zanzibar kutokana na mkwamo ilionao hivi sasa.

Kwa kuwa siyo siri tena kuwa Shein ni Rais aliyewekwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama na Maalim Seif ndiye Rais wa wazanzibari aliyechaguliwa kwenye sanduku la kura October 25 mwaka jana na matokeo yake 'kupinduliwa' na Jecha kwa maagizo ya viongozi wahafidhina ndani ya CCM.

CCM kuendelea kufanya kiburi kwa kuamini tu kuwa wao wana vifaru vya kijeshi na magari ya washawasha, nao pia wanapaswa wajikumbushe historia ya dunia ambapo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa dunia ambapo nguvu yoyote ya dola imewahi kuishinda nguvu ya Umma iliyojizatiti.
 
Mambo ya muungano CUF siku zote wamekuwa wakidai yapunguzwe na wangependa zaidi muungano uwe wa mkataba au serikali tatu.

Katiba yetu ya sasa kwa shinikizo la Seif na CUF yake iliondoa masuala ya uchaguzi wa serikali ya Zanzibar kwenye mambo ya muungano, hivyo Zanzibar ikaanzisha ZEC ambacho si chombo cha muungano. ZEC inatawaliwa na katiba ya serikali ya Zanzibar. Serikali ya Muungano haina mamlaka nayo.

Sasa kipi hapo hamkielewi rais wa serikali ya Muungano akisema mikono yake imefungwa na katiba wakati nyie wenyewe ndiyo mliomfunga?
Mwache tu maalim aendelee kuwa rais wa NYONYO kama ulivyoandika hapo juu, na huyo shein sijui mnamuita rais wa kitu gani?
Maalim Sef na SUK kwenye bunge(baraza la wawakillishe) walitunga wenyewe katiba ya Zenj na kumfunga mikoni rais wa Muungano, sasa kelele za CUF huko Marekani na hapa za nini? imekula kwao mpaka 2020!!! Dr Magufuli, you better keep away from what Maalim Seif is trying to force you into, you are dawn right for having washed your hands just as Pilate did before the crucifixion of Jesus Christ.
 
Back
Top Bottom