Kibajaj, sheikh wangu. Si kwamba Chiligati ametoa kauli ya kupinga wazo la kupunguzwa kwa posho kwa nguvu kubwa ki-hivyo kwa bahati mbaya.
Kumbuka, Wabunge wengi wa CCM wana madeni makubwa sana wanayodaiwa kutokana na pesa waliyokopa wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi. Maana wengi walitumia pesa nyingi sana kutoa rushwa ili waweze kupata ubunge. Mategemeo yao makuu yapo kwenye hizo posho wanazolipwa ndizo zinazowasaidia kulipia madeni yao pamoja na mali waliyoweka dhamana wakati wanakopa.
Kwa hiyo kumtegemea Mbunge wa CCM eti aunge mkono hilo wazo ni Ndoto ya Mchana.
Hawa jamaa hawana ubinaadamu hata kidogo! Hata hali ya maisha ya Mtanzania iwe mbaya kivipi hawako tayari kujitoa ili kuokoa jahazi
Lakini ndio watu mliowapigia kura hao!!
Chiligati ana roho mbaya kama sura yake! Hana tofauti na Chenge!
Nampongenza Chiligati amekua muwazi kabisa! Tumeshudia unafiki wa Wabunge wa Upinzani kama aliofanya Dr Slaa aliwahi kusema mshahara ni mkubwa kwa wabunge lakini kaenda mtaani anataka alipwe vile vile! Pia wakati bunge hili lina anza kulikua na habari ya milioni 90 ya magari Wabunge wa upinzani walichukua hela hiyo! Naona ni kujitafutia umaarufu tu hakuna lolote ni unafiki!
Hawa wabunge wa ccm sijui wako kwa mslahi y a nani?:smow:
Vyombo mbalimbali vimekuwa vikiripoti vipaumbele vya bajeti ya mwaka mpya wa fedha.Suala ambalo limekuwa na mvutozaidi ni kukatwa kwa posho za vikao kwa wabunge ambapo ni sehemu ya bajeti ya upinzani. Hapa hakika tumeona jinsi baadhi ya wanasiasa katika nchii walivyo walafi na ni namna gani wanasiasa hawa hawana utu kwa raia ambao ndiyo waliowaweka madarakani.Naibu katibu mkuu wa chama cha MAPINDUZI bwana JOHN CHILIGATI ametoa kauli inayoonyesha jinsi asivyo na utu na pia jinsi asivyo mzalendo. Kauli ya kwamba Zitto anataka umaarufu kwa vile sitting allowance zimepunguzwa na kusema wazi kuwa CCM watachukua posho hizo na kama wapinzani hawataki waache ni kauli mbovu sana kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama yeye. Ikumbukwe kwamba mshahara wao uko palepale! posho nyingine ziko palepale na wakiwa bungeni wanalipiwa gharama zote muhimu. Kauli hii imedhihirisha wazi kuwa hata hii kampeni ya kujivua gamba ni danganya toto. Wenzetu ulaya wanapunguza matumizi sisi tunaongeza kwa mambo yasiyo na msingi? mtu alipwe milioni saba gari ya zaidi ya milioni sitini marupurupu kibao bado ashindwe kuwa na utu hata chembe oja?
Jeuri ya pesa hizi ndiyo imewahamisha majimboni wako hapa mjini wakijivinjari.
Jamani tembeeni tanzania kuna umaskini mkubwa sana.
Mbunge akilipwamilioni saba adundulize ajinununlie gari lake mwenyewe kwanza atakuwa na uchungu nalo na atalitunza.
Kwa kauli hii ya chiligati anazidi kuiweka ccm matatani.
"AFRICA POLITICS IS AN INVESTIMENT JUSTFY"
Nampongenza Chiligati amekua muwazi kabisa! Tumeshudia unafiki wa Wabunge wa Upinzani kama aliofanya Dr Slaa aliwahi kusema mshahara ni mkubwa kwa wabunge lakini kaenda mtaani anataka alipwe vile vile! Pia wakati bunge hili lina anza kulikua na habari ya milioni 90 ya magari Wabunge wa upinzani walichukua hela hiyo! Naona ni kujitafutia umaarufu tu hakuna lolote ni unafiki!
Hapa tunataka tuone wabunge wa chadema wakisusia hizo posho au wakidirect katika miradi ya maendeleo.
Wasitupige changa la macho kama kwenye mishahara ya wabunge.
Hatakama magamba watakaa hilo pendekezo, magwanda waonyeshe mfano!
Wabunge wengi wa CCM wana madeni makubwa sana wanayodaiwa kutokana na pesa waliyokopa wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi. Mategemeo yao makuu yapo kwenye hizo posho wanazolipwa ndizo zinazowasaidia kulipia madeni yao pamoja na mali waliyoweka dhamana wakati wanakopa.
Kwa hiyo kumtegemea Mbunge wa CCM eti aunge mkono hilo wazo ni Ndoto ya Mchana.
Hawa jamaa hawana ubinaadamu hata kidogo! Hata hali ya maisha ya Mtanzania iwe mbaya kivipi hawako tayari kujitoa ili kuokoa jahazi
Lakini ndio watu mliowapigia kura hao!!
Chiligati ana roho mbaya kama sura yake! Hana tofauti na Chenge!
Hawa wabunge wa ccm sijui wako kwa mslahi y a nani?:smow:
Wakuu.Salaam.
Kimsingi Bunge limeweka Utaratibu ili kumsaidia Mbunge afanye vizuri kazi zake za Kibunge
Mkumbuke vile vile siku hizi hela imeshuka sana thamani, hizi Milioni 90 zinaisha ndani ya wiki moja tu na unaweza ukajikuta hakuna la maana ulilolifanya.
Aluta Continua
Kutoka Miti Mirefu Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu.
Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.
Soma maoni yetu ukurasa wa sita