Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,741
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA
KAULI YA AWALI YA KAMATI KUU KUHUSU NJAMA UCHAGUZI WA MEYA JIJI LA DARE ES SALAAM NA VITISHO KWA WAWAKILISHI WA WANANCHI
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo imelaani vitendo vya njama za kisiasa zinazofanywa kupora haki ya wananchi katika uchaguzi wa Meya Jiji la Dar es Salaam na kuwa ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea nchini huku ukionekana kuwa na ‘baraka’ za viongozi wakubwa wa nchi, hautavumilika.
Akitoa kauli hiyo ya awali mbele ya waandishi wa habari leo wakati Kamati Kuu ikianza kikao chake jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa CHADEMA haitakubali kuona Serikali ya awamu ya tano ikitawala kwa kutegemea udhalimu wa kutumia vyombo vya dola huku ikivunja sheria na taratibu nchi.
Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa ni ajabu kuwa watawala wa awamu ya tano ambao wanataka kujinasibu kuwa wanakubalika, wanalazimika kuendesha nchi kwa kuvunja misingi ya demokrasia na kutumia njia za kunyanyasa wapinzani kwa nia ya kuwanyamazisha badala ya kuwa tayari kukosolewa kwa mstakabali sahihi wa maslahi na matakwa ya nchi kwa ujumla.
Amesema kuwa hali hiyo ya sheria kuvunjwa kwa ajili ya kuwashughulikia wapinzani ikiendelea bila kukomeshwa ikiwemo kuwapora wananchi haki yao ya wazi kama inavyotaka kufanyika kwenye umeya wa Dar es Salaam, watawala watachochea moto ambao watashindwa kuuzima.
“Tumelazimika kuzungumza nanyi waandishi wa habari kutoa kauli hii ya awali wakati tunaelekea kuanza kikao cha Kamati Kuu kwa sababu ya matukio ya hila, njama na mipango ovu ya kisiasa inayopangwa na Serikali ya CCM ili kujihalalishia mambo kinyume na sheria za nchi.
“Ipo mikakati ya siri ambayo imeanza kutekelezwa kwa vitendo vya kuwakamata na kuwashushia hadhi na kuwadhalilisha wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge na madiwani ambao kama inavyoendelea kufanyika Jiji la Dar es Salaam,” amesema Mwenyekiti Mbowe.
Ameongeza kusema kuwa njama zinazoendelea za kuwakamata, kuwaweka chini ya ulinzi na kuwanyima dhamana wabunge na madiwani wa CHADEMA katika Jiji la Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati mkubwa wa Serikali ya CCM kutaka kupora uchaguzi wa meya na kulinda ufisadi mkubwa katika jiji hilo.
“Uchaguzi wa Meya Dar es Salaam unasuasua kwa miezi minne na siku tano hadi leo. Wananchi walifanya maamuzi ya kuchagua madiwani wengi wa UKAWA wakaikataa CCM. Chama chochote makini kilipaswa kuheshimu maamuzi hayo ya wananchi.
“Temeke ambako CCM wana madiwani wengi hakukuwa na tatizo katika kumpata meya ambaye anatokana na CCM. Lakini katika maeneo yote ambako CHADEMA au Ukawa tumeshinda wenzetu hawa wamekataa kukubali, kila mahali imekuwa ni shida kweli kweli…”
“Huko Kyerwa ambako tulikuwa na madiwani wengi, madiwani wetu walikamatwa siku ya kupiga kura na kubambikiwa kesi, huko Kilombero hata leo tu mbunge wa jimbo amekamatwa na kudhalilishwa asiingie ukumbi wa kupiga kura.
“Tunapozungumza hapa Mbunge Mdee anashikiliwa na polisi, wanamshikilia Mbunge Waitara, wanamtafuta Kubenea, wanawashikilia madiwani wetu na wanachama bila sababu zote za msingi, lakini lengo ni kuhujumu uchaguzi wa meya,” amesema Mwenyekiti na kuongeza;
“Wakati watu wetu wanakamatwa, yule RAS aliyesoma zuio la mahakama la kughushi na kuharibu uchaguzi na kusababisha vurugu yuko huru. Haya yote yanafanyika Rais Magufuli ambaye ndiye Waziri wa TAMISEMI anajua, Waziri Mkuu anajua, Sefue anajua, CCM wanasheherekea na wote hawa ni sehemu ya uchakachuaji huu unaofanyika.
Mwenyekiti pia amezungumzia wito wa barua walizoandikiwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA, wakiwemo Godbless Lema, Pauline Gekul na Ester Bulaya kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa madai ya kumvunjia heshima Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge siku ya mjadala wa Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja vikao vya bunge kupitia TBC.
Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa taarifa hiyo ya awali itafuatiwa na tamko la Kamati Kuu ambayo inakutana jijini Dar es Salaam kujadili na kuamua juu ya masuala mbalimbali ikiwemo kuhusu hali ya kisiasa nchini.
Imetolewa leo Jumanne, Machi 1, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano