ideal safarimate
Member
- Mar 17, 2016
- 71
- 91
Kwa mara ya kwanza uchaguzi wa marekani umevuta hisia za watanzania wengi hasa kutokana na urahisi wa kupata habari kupitia huduma za "internet" na mitandao ya kijamii.
Mgombea maarufu ni Donald Trump(R) ambaye amenukuliwa sana kwa kauli zake tata hasa kuhusu uhamiaji na sera za nje.
Pamoja na ukweli kwamba Trump amekua mtu mwenye kauli tata na msimamo mkali lakini kuna baadhi ya watu wamekua wakipotosha na kutunga kauli na kuzinasibisha na Trump.
Moja ya nukuu zilizosambaa sana ni kuhusu kauli yake ya kejeli kwa waafrika na viongozi wake kwamba ni wavivu, wezi na wanastahili kutawaliwa tena.Pili ni kuhusu mgombea mwingine Mama Hilary Clinton (D) kwamba kama hakuweza kumridhisha mume wake Bill Clinton atawezaje kuwaridhisha wamarekani.
Kauli hizi na nyingine nyingi zimesambaa sana na zimezua mjadala kwa watu wengi hata watu ambao ninawahesabu kama makini mfano Bw.Humphrey Polepole na waandishi wa magazeti wameingia mtego wa kuziamini.
Ukweli ni kwamba pamoja cnn , fox, bbc n.k kuripoti kauli nyingine tata za Trump hakuna rekodi yoyote ya Trump kuziongea kauli hizi na hakuna chombo chochote cha habari cha marekani au kimataifa kilichoripoti wala wapinzani wake kama Ted Cruz, John Kasich hata Hilary mwenyewe hawajawahi kuzizungumzia popote.
Katika election with most scrutinization surely he wouldn't survive this controversial claims IF they existed in first place!
GET YOUR FACTS STRAIGHT BEFORE YOU PUBLISH ANYTHING.