Kauli tata mtaani kwenu

BONNIE GOLD

JF-Expert Member
Jan 27, 2021
330
612
Upo zako mgahawani, utasikia kauli hizi zenye utata mtupu:

Mhudumu: Vipi umeshawashughulikia wateja?"

Wateja: Aah! Sema kuhudumiwa, siyo kushughulikiwa.

Mhudumu: Karibu Masta, za mzunguko?

Mteja 1 wa kiume: Mzunguko gani, acha ufala wewe.

Mteje 2: Oya shika hela yako (anatoa 10,000).

Mhudumu 2: Mzee hauna ndogo? Tupe ndogo bhana, hii hatuna chenji.

Mteja 3: Oyyyyyyy naomba kitumbua na maziwa. Jana kitumbua chako kilikuwa kitamu kweli kweli.

Mhudumu: Weka kauli sawa, sio kitumbua changu, mi siyo mpishi.

Mteja 4: Ahaaaaaa, shee mkuuu ndugu yangu! Za siku zako, unaendeleaje na hali?

Mhudumu: Wewe, kauli gani hizo, za siku zipi yani, dadavua?

Mteja: Oyy acha leo sina hela, nitakupitishia.

Mhudumu: Weka kauli sawa, sema ntakupitia hela yako baadae, sio ntakuptishia!!Utanipitishia nini sasa, mti au? Acha ujinga.


KWENYE DALADALA

Konda: Makumbusho makumbusho, vipi unaenda?

Abiria: Hamna siendi, ila ukitaka nikupeleke nakupeleka chaap moja.

Konda: Naomba nauli mzee.

Abiria: Ngoja ikisimama nakupa.

Konda: Acha ujinga weweeee!

Huku mtaani ukiambiwa kauli yeyote na vijana hawa, itafakari mara mbili kwanza!
255753123747_status_0d69e957c99f4a67b011b327be36999b.jpg

JamiiForums1924898438.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom