Kauli na ahadi za mastaa zilizoishia hewani

explicity

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
207
140
Mastaa wengi wa Bongo wamekuwa wakiahidi vitu vingi kwa mashabiki wao lakini vitu hivyo vinakuwa vinapotea hewani bila ya kutekelezeka.
d023c3d5b16bd1249a08b80ce366a1a7.jpg
‘Ahadi ni deni’, watu wengi wanakuwa wanasahau maneno ambayo mwanzo waliyasema wenyewe na bila hata ya kurudisha tena mrejesho kwa mashabiki wao juu ya kauli zao za mwanzo walizozisema.
Baadhi ya mastaa wameshaanza kupoteza uaminifu kwa mashabiki wao kutokana na kuahidi kuja na vitu vingi lakini muda umezidi kwenda na mambo yanazidi kubadilika huku kauli zao zikiwa hazitekelezwi.
Hawa ni baadhi ya mastaa walioshindwa kutekeleza ahadi zao kwa mashabiki wao.

1:Wema Sepetu
9f6aebf9ffe7d02b90eb229dd02f3fd3.jpg

Nimwaka mmoja takribani Madam atoe ahadi ya kuachia movie aliyofanya na staa wa movie kutoka Ghana, Van Vicker.
Ni kweli kuna kipindi Sepetunga hakuwepo nchini kwa muda kidogo na alidai kuwa anaenda kushoot movie yake na staa huyo wa Ghana. Aliwahi kusema alifanya connection na Van Vicker kupitia Instagram. Movie hiyo hadi leo haijatoka.
Naamini hiyo movie siku ikitoka inaweza ikaweka rekodi ya kuwa movie ya kwanza kuuza kwa soko la ndani kutokana na umaarufu waliokuwa nao Madam Wema na Van Vicker, lakini pia itamfanya Wema kutanua soko lake nchi za Afrika Magharibi.
Muda bado upo ngoja tuendelee kusubiri japo wengi wamechoka kuisubiria na tayari wameshakata tamaa juu ya ujio wa hiyo movie.

2:Alikiba
74e54803449f946c3200e5debf9ca03a.jpg

Unakumbuka kauli ya kuwa kuna nyimbo ya Alikiba na Davido inakuja? Ni muda mrefu tangu hilo limezungumzwa lakini bado mpaka leo halijatimia.
‘Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja’ lakini pia waswahili wanasema kuwa ‘ngoja ngoja yaumiza matumbo’, tutasubiri mpaka lini?
Alikiba amezidi kuachia nyimbo nyingine kama ‘Nagharamia’ na ‘Lupela’ huku mashabiki wakiwa na hamu ya kuisikiliza nyimbo aliyoimba na Davido ambayo tunategemea utakuwa ni muziki mzuri ambao utazidi kuutangaza muziki wa Bongo Fleva nje ya mipaka ya Tanzania.

3:Idriss sultan
78ecc16ddda3926040ac1beb0859cd31.jpg

Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan anaingia kwenye orodha ya mastaa walioshindwa kutekeleza ahadi zao.
Ni takribani miaka miwili tangu atangazwe kuwa mshindi wa BBA, baada ya muda Idris aliahidi kuja na reality TV show ambayo alisema amepanga itakuwa inaonyeshwa kwenye kituo cha BET.
Haijulikani iwapo ndoto hizo za kuja na Reality Show zimepotea au bado mipango ipo vile vile. Ni kitu kizuri ambacho alikifikiria Idris na kingeweza kumuongezea umaarufu zaidi na kumpa deals kibao za kuingiza pesa kwa kuwa kingeweza kuonekana dunia nzima.

4:Barnaba
0f2ab4d10a69dd0af391abfba26aeee8.jpg

Barnaba ni mmoja kati ya wasanii wa Bongo Fleva waliobarikiwa kuwa na vipaji vingi kwenye muziki.
Mwaka jana mwishoni Barnaba aliachia wimbo aliomshirikisha staa kutoka nchini Uganda, Chameleone. Baada ya kuachia wimbo huo ‘Nakutunza’ Barnaba alitoa ahadi ya kuachia video ya wimbo huo baada ya miezi miwili lakini mpaka sasa imepita miezi mitano na siku kadhaa tangu ameachia wimbo huo na bado video yake haijaonekana.
‘Nakutunza’ ni wimbo ambao umewakutanisha mafundi wa muziki na hakika huwezi kuchoka kuusikiliza. Mpaka sasa mashabiki wameshatengeneza script zao vichwani kwa ajili ya video yake.

5:Nikki wa pili
2971d3c4342ea094daab9432e2fdb744.jpg

Ukiwataja wasanii wasomi kwenye Bongo Fleva, hutaacha kulitaja jina la Nick wa Pili lakini pia ni miongoni kati ya wasanii wachache wanao hit na nyimbo zao kadhaa bila kuwa na video kama ‘Safari’ na ‘Baba Swalehe’.
‘Baba Swalehe’ ni wimbo wa Nick ambao bado unafanya vizuri tangu siku ya kwanza ilipoachiwa kwenye redio. Ingawa ni miezi mingi imepita tangu wimbo huo utoke Novemba mwaka jana, bado Nick hajaachia video yake.
Aliwahi kudai kuwa angeachia video yake baada ya G-Nako kuachia wimbo wake mpya na sasa ni miezi kadhaa tayari imeshapita tangu G-Nako aachie Original lakini video ya Baba Swalehe haipo.
Bongo5.com
 
Idriss milioni 500 zimeisha kaamua kuajiriwa kama mtangazaji
Kiba no MTU aliefeli siku nyiingi ila ni kama anaswagwa na wasiomtakia mema Diamond
Wema hajitambui,anaamini atabakia kua na miaka 20,milele
 
Prof Jay alihaidi atapeleka wanafunzi mwezini wakafanye huko practiko
 
Idriss milioni 500 zimeisha kaamua kuajiriwa kama mtangazaji
Kiba no MTU aliefeli siku nyiingi ila ni kama anaswagwa na wasiomtakia mema Diamond
Wema hajitambui,anaamini atabakia kua na miaka 20,milele
Akuna aijuae kesho
 
DIAMOND
-Chibu beats na bidhaa nyingine za WCB
-Ngoma na Psquare
-Ngoma na A-list artist marekani n.k
Huyu wangemuweka namba moja, anaongoza kwa ahadi hewa. Japo najuwa zitatimizwa, ila naona kama huwa anaongea mapema sana kiasi kwamba kama ni nyimbo zinakuwa nyingi afu wanaishia kusema tunazipa muda, mfano ya psquare walitangaza tokea may 2015 wakasema soon ila bado mwezi kutimiza mwaka sasa..

SHILOLE
-Ngoma na Jennifer Lopez
 
Back
Top Bottom