Kauli mbiu za ccm ni kejeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli mbiu za ccm ni kejeli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwinukai, Jun 25, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kauli mbiu zinzotumiwa na CCM kwa hakika ni kejeli hii inaamanisha kauli mbiu zimekuwa kinyume na matarajio yake, mfano umo kwa baadhi ya Kauli mbiu zifuatazo :-
  UKWELI NA UWAZI hii ni kauli ilitumiwa na CCM enzi za mkapa cha kushangaza ni katika utawala huu waandishi wa habari waligandamizwa na mikataba mingi ikiwemo ya Rada ilifanywa kwa siri na taifa likiambulia hasara,ubinafsishaji haukuwa wa ukweli na uwazi,uuzaji wa nyumba za taifa kwa maslahi ya kifisadi yalimaanisha kwenda kinyume kabisa na kauli mbiu.

  ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI, MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA
  , hii ndiyo kauli aliyoingia nayo JK mwaka 2005,kwa bahati mbaya ari mpya na kasi pamoja nguvu vilikuwa ya kudidimiza maendeleo kwa ufisadi na uongozi wa kishkaji na baada yakawa Maisha Bora kwa Kila Fisadi,na Mtanzania akiwa anagugumia maisha magumu.

  ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI
  , hii ilikuwa kauli ya mwaka 2010 katika kipindi hiki watu maisha yaemekuwa magumu zaidi,

  VUA GAMBA kauli ililenga kuwafukuza wanachama wanaojihusisha na Ufisadi lakini cha kustaajabisha hao Magamba wamekuwa wakipewa nyadhifa muhimu katika nchi kuziongoza na hata kupata nafasi ya kuwania na kushinda uongozi ndani ya CCM.

  Kwa ujumla ukiangalia sana kauli mbiu za CCM zimekuwa zikimaanisha kinyume
   
Loading...