Kauli hii ya Mh. James Lembeli, Ni kweli au?

Kauli hii ya Mh. James Lembeli, Ni kweli au?

labda na mimi niongezeee HAKUNA TAASISI HATA MOJA!! lembeli kazidisha
 
Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli amesema kuwa Tanzania kama nchi sasa iko njiapanda. Lembeli alikuwa akichangia katika Mjadala ulioitishwa na Naibu Spika Job Ndugai jana kuona uhalali wa Bunge kujadili Ripoti za CAG na TAKUKURU kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow. Lembeli amesema kuwa kwa hali ilivyo Tanznia itapaswa ichague ka ya kuenelea kudumisha amani au kutumbukia kwenye machafuko.

Pia Lembeli alihoji kusitasita kwa Serikali katika kujadiliwa kwa suala la Escrow wakati masuala mengine kama Operesheni Tokomeza yalijadiliwa kwa haraka. Alimtolea mfano Balozi Hamis Kagasheki ambaye aliachia ngazi kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza.

Binafsi nakubaliana na Lembeli. Mjadala wa Escrow haufunikiki,hauzuiliki na hauepukiki
 
Wakati jana, akichangia hoja ya inayoendelea bungeni alisema hivi.

"Nchi hii kuna Taasisi mbili tu au tatu zinazoaminika sasa na wananchi, ambazo ni bunge la JMT na JWTZ tu" nilipata mshangao sana wa kauli, hivi ni kweli hakuna taasisi nyingine zinazoaminika na wananchi.....

Kama zipo tuzitaje......

kwani inshu ya melemeta si ilikuwa kuhusiana na jeshi japo wengine hatukuambulia ilitetewa na pinda mtoto wa mkulima isijadiliwe eti kiusalama zaidi.
 
Kwamba JWTZ bado inaaminika! Kwani yule Shimbo alikuwa mwanajeshi wa wapi?
 
Nyie waheshimiwa wabunge wetu leo ndio mnajua mahakama zetu ni tatizo?

Naungana na Mb. Lembeli kuwa wananchi hawana imani na mahakama

Mahakama zetu zimepewa uhuru wa kupindukia hivyo wanajifanyia wanavyotaka

Mahakamani pale majaji,mahakimu,makarani na mawakili akiwemo Tindu Lissu ni balaa na majanga

Mahakamani pale kuna miji mingine hapa Tz majaji,mahakimu,mawakili na matajiri wametengeneza mitandao na makampuni ya kununua nyumba wanazodhulumiwa masikini kwa kuinject migogoro,ikifika mahakamani tu mchezo umeisha.

Wabunge kwa nini hamuhoji na kupeleka hoja binafsi ya kuidhibiti mahamakama?

Mahakimu na Majaji kwa ushirikiano na mawakili na makarani wanafanya mambo ya hovyo tu hakuna hatua inayochukuliwa

Ni kwa vipi Jaji au Hakimu akae na kesi hadi miaka kumi hajatoa ruling huku wakuu wa mahakama wakimuangalia tu.

Ni ajabu sana kuona fisadi anafikwishwa Mahakamani akicheeka kwa dharau kama vile anapelekwa kwenye starehe

Sasa limewafika ni muda muafaka kuifunga gavana na sio kwa yanayowakumba nyie tu hata huku uswazi ni sheeedah

UHURU UMEPINDUKIA SASA MPAKA BUNGENI WAMEFIKA BILA AIBU
 
mimi nathani,hakuna zaidi ya jeshi kwani hata bunge, hakuna kitu japo nakiri kuna wabunge smart,ila itikadi za vyama zinafanya tupunguze imani,hasa spika kuwa na chama ndo imani inakwisha kabisa.

Yale ya Meremeta na siri za jeshi na usalma wa nchi vipi? Mimi sioni huko kuaminika kwa JWTZ. Hivi mnajua jeshi linatuibia sana watz. hasa madini na rasilimali nyingine? Hamkuona maofisa wa juu wa jeshi waliwahi kuburuzwa mahakamni mahakama ikaamu kuwasafisha kuondoa soo? Hii nchi imeoza kwa sababu ya uongozi dahifu wa MR Dhaifu aka Mzee wa Tezi Dume.
 
Ni kweli, sijui kwa nini JWTZ wapo kama kobe?

Nadhani bado mahakama inaaminika kwa unafuu kuliko hz taasisi zingne sema tu imepitiwa na upepo.Bunge ndo ovyo kabisa sawa na police.Na kama kuna taasisi wanatafuna hela ya nchi hii ni JWTZ sema ishu zao hazimulikwi.KIUKWELI MAHAKAMA NDO AFADHALI HATA TUKATAE.
 
Wakati jana, akichangia hoja ya inayoendelea bungeni alisema hivi.

"Nchi hii kuna Taasisi mbili tu au tatu zinazoaminika sasa na wananchi, ambazo ni bunge la JMT na JWTZ tu" nilipata mshangao sana wa kauli, hivi ni kweli hakuna taasisi nyingine zinazoaminika na wananchi.....

Kama zipo tuzitaje......
Binafsi bunge pia siliamini, kwa hiyo ninabakiza JWTZ tu.
 
lembeli nae mwizi mkubwa

lijizi likubwa nani kamdanganya watanganyika tunaliamini bunge sisi tunaamini ukawa tu si zaidi ya hapo hawo wachumia tumbo wataangaika sana kujipendekeza kwetu 2015 hawana chao kwetu
 
kama wapo wabunge waadilifu kutoka chama tawala; wanaofahamu ufisadi Wa wenzao lakini wakakaa kimya; nao pia ni mafisadi Wa kisiasa
 
Kwamba JWTZ bado inaaminika! Kwani yule Shimbo alikuwa mwanajeshi wa wapi?

Shimbo alipiga billions of fedha, na sasa china anaendelea kula......plus madawa + ndovu business.
 
Aic wtz mpaka mnyongwe ndo muone mnaonwa au mtu ajiite yesu ndo muone ana watetea!!!!!!!
 
hata yeye sio mkweli JWTZ wana usafi gani? hawa si ndo walihusika na mereremeta sijui deep green ya EPA? (forgive me if not true, maana hizi habari tunaokota tu). Ila One thing I know for sure vijana wa JWTZ wamekuwa wakiwapiga vijana kwa kuvaa nguo zinazofanana na jezi zao, badala ya kuwafikisha mahakamani. Hawa pia walihusika katika kashfa ya tokomeza ujangili. sasa usafi wao upo wapi kama taasisi. Huku sio vijana wanatumia vyeti vya kufoji? nafikiri aliwaogopa tu. Na wabunge si ndio hao kina chenge, Lowasa, Sitta, tibaijuka, Komba sasa kama taasisi usafi wao upo wapi?. Taasisi isiyo na longolongo Tanzania ni shirikisho la watoto wa chekechea tu, maana hao ukiuliza mmekunywa uji na sukari au bila sukari watakwambia ukweli.
 
Ki msingi bunge haliaminiki. Ni taasisi moja tu inyoaminika, JWT basi. Tumuombe Mungu jeshi letu liendelee hivi,ndiyo tegemeo letu wote.
 
Back
Top Bottom