Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,292
- 11,071
Nanukuu "Nawashukuru wapinzani kwa ujasiri wao mkubwa wa kujitokeza kushindana na chama cha Mapinduzi. Uchaguzi sasa umekwisha. Kauli ya wananchi imedhihirika. Tuungane, tuwe kitu kimoja; tujenge na kuendeleza nchi yetu." mwisho wa kunukuu.
Rais Kikwete aliitoa kauli hii mnamo tarehe 30 Desemba 2005, katika hotuba yake ya kwanza kabisa kulihutubia bunge na Watanzania kwa ujumla, tangu achaguliwe kuwa raisi wa nne wa nchi hii.
Katika makala hii nitaongelea kwa ufupi suala kauli moja kutoka katika nukuu hapo juu "Tuungane, tuwe kitu kimoja, tujenge na kuendeleza nchi yetu".
Kimsingi hii ni kauli nzito sana kutolewa na kiongozi wa nchi, na iliwalenga wananchi wenye mtazamo tofauti na chama tawala, wapinzani na wasio na vyama (huenda na wanachama wenzao ndani ya chama chao wenye mawazo tofauti na wanachama wengine). Kwani bila kuungana hatuwezi kufanikiwa, kwa vile Umoja ni nguvu.
Swali linakuja kwamba, " Je chama tawala wana utashi wa kisiasa wa kuungana na watu wenye mawazo, itikadi, malengo na mitazamo tofauti na wao?" Wako tayari kupokea changamoto mpya na chungu kuzimeza toka kwa watu hao wanaowaomba kuungana nao? Wako tayari kusaidina nao katika kupambana na rushwa na umaskini unaotafuna nchi ila leo? Wako tayari kushirikiana nao kupunguza bajeti za safari za nje na ndani ili tuweze kujitegemea katika bajeti yetu kila mwaka? Je chama tawala kipo tayari kushirikiana na watu hawa katika kupitisha bajeti mbadala kutoka katika upande pinzani zenye maslahi kwa wananchi? Wako tayari kuchangia mawazo ya wapinzani katika kusisitiza kuwekeza katika kilimo bora?
Wameungana na watu hawa katika kushughulikia kero sugu ya rushwa inayoendelea kuongelewa sasa nchini mwetu?
Kama majibu yatakuwa na 'ndiyo' nyingi kuliko 'hapana' basi lazima kauli hiyo kutoka kwa mheshimiwa raisi itakuwa na hitilafu, na wala itakuwa haikutolewa kwa dhati ya moyo wake.
Mungu Ibariki Tanzania