Kauli hii ya Kikwete ni thabiti?

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,963
10,457
Nanukuu "Nawashukuru wapinzani kwa ujasiri wao mkubwa wa kujitokeza kushindana na chama cha Mapinduzi. Uchaguzi sasa umekwisha. Kauli ya wananchi imedhihirika. Tuungane, tuwe kitu kimoja; tujenge na kuendeleza nchi yetu." mwisho wa kunukuu.

Rais Kikwete aliitoa kauli hii mnamo tarehe 30 Desemba 2005, katika hotuba yake ya kwanza kabisa kulihutubia bunge na Watanzania kwa ujumla, tangu achaguliwe kuwa raisi wa nne wa nchi hii.

Katika makala hii nitaongelea kwa ufupi suala kauli moja kutoka katika nukuu hapo juu "Tuungane, tuwe kitu kimoja, tujenge na kuendeleza nchi yetu".

Kimsingi hii ni kauli nzito sana kutolewa na kiongozi wa nchi, na iliwalenga wananchi wenye mtazamo tofauti na chama tawala, wapinzani na wasio na vyama (huenda na wanachama wenzao ndani ya chama chao wenye mawazo tofauti na wanachama wengine). Kwani bila kuungana hatuwezi kufanikiwa, kwa vile Umoja ni nguvu.

Swali linakuja kwamba, " Je chama tawala wana utashi wa kisiasa wa kuungana na watu wenye mawazo, itikadi, malengo na mitazamo tofauti na wao?" Wako tayari kupokea changamoto mpya na chungu kuzimeza toka kwa watu hao wanaowaomba kuungana nao? Wako tayari kusaidina nao katika kupambana na rushwa na umaskini unaotafuna nchi ila leo? Wako tayari kushirikiana nao kupunguza bajeti za safari za nje na ndani ili tuweze kujitegemea katika bajeti yetu kila mwaka? Je chama tawala kipo tayari kushirikiana na watu hawa katika kupitisha bajeti mbadala kutoka katika upande pinzani zenye maslahi kwa wananchi? Wako tayari kuchangia mawazo ya wapinzani katika kusisitiza kuwekeza katika kilimo bora?

Wameungana na watu hawa katika kushughulikia kero sugu ya rushwa inayoendelea kuongelewa sasa nchini mwetu?

Kama majibu yatakuwa na 'ndiyo' nyingi kuliko 'hapana' basi lazima kauli hiyo kutoka kwa mheshimiwa raisi itakuwa na hitilafu, na wala itakuwa haikutolewa kwa dhati ya moyo wake.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Sasa tupo na mvunja umoja na amani ya nchi
Ambae pamoja na mambo mengine, amedhihirisha anaweza kukusamehe hata kama utaripua bandari kuliko kumsemanga Daudi Albert Bashite!!!

Ambae amedhihirisha ni heri upite makanisani na misikitini ukawa unamwaga vinyesi humo bado na anaweza kukuombea kuliko kumjulia hali mpinzani na hasa mpinzani mwenyewe akiwa aina ya Godbless Lema na Tundu Lissu!!!
 
Yaani hajui hata anafanya nini, yule mama maria sarungi anasema ametoka kwenye hero to zero very sad
 
Huo ndo ukweli wenyewe... from Hero to Zero!!!
Kiongozi mzuri sio lazima afanye yale yatakayofurahiwa na wananchi tu,huyo sio kiingozi bora angeuza icecream,kiongozi lazima aonyeshe misimamo thabiti hata kama maelfu ya mapunguani hayatamuelewa kwa wakati huo
 
Kwa mfano msimamo upi thabiti alioonyesha?!

Wa kuendelea kumlinda Daudi Albert Bashite pamoja na kashifa kadhaa zinazomkabili?!
 
Kwa mfano msimamo upi thabiti alioonyesha?!

Wa kuendelea kumlinda Daudi Albert Bashite pamoja na kashifa kadhaa zinazomkabili?!
Angalia hapo nimeandika hata kama mapunguani elfu hayatamuelewa nadhani unaweza jua upo fungu gani?
 
Angalia hapo nimeandika hata kama mapunguani elfu hayatamuelewa nadhani unaweza jua upo fungu gani?
Hakuna cha maana ulichoandika zaidi ya porojo na kuonesha kwamba ni porojo ndo maana umeshindwa kujibu na kuishia kutoa lugha chafu...!!
 
Back
Top Bottom