Kauli hii ya JK itafanya kila kitu kipande BEI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hii ya JK itafanya kila kitu kipande BEI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vakwavwe, Jan 4, 2011.

 1. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bei ya Umeme


  Ndugu Wananchi;


  Natambua kuwepo kwa mazungumzo, katika jamii kuhusu uamuzi wa EWURA wa kukubali ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) kuongeza bei ya umeme. Wakati mwingine mazungumzo yamekuwa na hisia kali na hata jazba kutawala. Wizara, TANESCO na EWURA wameeleza kwa ufasaha misingi iliyotumika mpaka kufikia uamuzi huo. Sina maelezo mazuri zaidi ya hayo. Ninachotaka kusema mimi ni kuwaomba Watanzania wenzangu kutokukubali suala hili la kibiashara na kiuchumi kugeuzwa kuwa la kisiasa na kutafutiwa majawabu ya kisiasa.


  Naomba tuamini na kukubali maelezo ya TANESCO na EWURA kwamba katika miaka minne hii gharama za uendeshaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme zimepanda kama zilivyopanda katika shughuli nyingine. Hivyo basi, kutaka bei ya umeme ibaki kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita hautokuwa uamuzi sahihi kiuchumi na kibiashara kwa TANESCO. EWURA imefanya kazi nzuri ya kuchambua maombi ya TANESCO na kuyakubali yanayostahili na kuyakataa yasiyostahili kuwa sehemu ya bei. Kwa kufanya hivyo, watumiaji wa umeme wamelindwa wasibebeshwe mzigo usiostahili na Shirila la Umeme limewezeshwa ili lisiendeshe shughuli zake kwa hasara.

  nimesikia wamiliki wa Mabasi wanapandisha nauli soon!DAWASCO wameunga tela,bei ya maji itaongezeka soon,soda zimepanda bei katikati ya mwaka wa budget,products za viwandani zinapanda bila notifications!!!!!!!!!!
  teh teh teh tih tih. maisha bora kwa kila MDANGANYIKA kwa kasi zaidi na nguvu zaidi na pia ari zaidi. kama Rais anabariki upandaji huu wa UMEME kwa sababu kila kitu kimepanda ni dhahiri hata ambao hawakuwa na nia hiyo watapandisha tu.

  TANZANIA YANGU MWEEEEE! mishahara ndo haipandi na haitapanda.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mjomba Vakwavwe,

  Tulikuwa tumeanza kusahau kauli-nyundo hiyo ya JK, wewe umetukumbusha na kuamsha maumivu makali!

  Hakika kauli yake hiyo imetoa consent kwa wafanyabiashara wote kupandisha bei za bidhaa zao kwa kuangalia 'muda' tu ambao bei zimekuwa stagnant...
  Hivi serikali hii yenye uwezo wa kuwalipa Dowans bil185 haiwezi kusubscribe hiyo 18.5 % ya ongezeko la bei kwa mlaji?...
  Jibu ni moja kwamba serikali ina vipaumbele vyake, na si kumlinda mwana-wa-nchi!...Wanajua kuwa wao na jamaa zao ongezeko halitawahusu wala kuwaathiri!
   
 3. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Amini msiamini JK hana wasaidizi wa maana au yeye mwenyewe ndio bila bila. Ktk hiyo hutuba alisema bei umeme haijapanda toka 2007 na kwamba hicho ni kitu hatari kwa uchumi!!! Kazi kweli kweli.
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  JK hajui madhara ya kupanda kwa umeme, yeye umeme anaupata masaa 32 kwa siku, siku 9 kwa wiki, wiki 72 kwa mwaka na siku 565 kwa mwaka. Kupanda bei kwa vit kwamhusu nnini? Yeye analetewa kila kitu hata hajui nyanya inauzwaje Kariakoo, labda katika magazeti. Tusimwonee JK, hajui alitendalo. Ameshafika Ikulu anategemea wasalama wake kumletea habari, ambao wanachakachua habari kabla hazijamfikia. Hata wewe ungekuwa rais huenda ungefanya yayo hayo.
   
 5. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hapana ndugu nisingefanya hayo.....kuna vipaumbele ambavyo serikali ikivitilia mkazo maisha yangelegeza ugumu kidogo. kama JK alitoa some trillions kwa wanunuzi wa Pamba wakati kuna uliosemekana mtikisiko wa uchumi anashindwaje kusubsidize mambo ya umeme!!!?
  ni upuuzi tu,hakuna lolote, badala ya kusubsdize yeye anatutwanga na Dowans tena....
  na akina rweye.. ambao mi nawaheshimu sana watu wa nyumbani nao wako brainwashed wanapinga kuwa rais hamiliki Dowans si waseme mmiliki sahihi?wana PCCB,Usalama wa CCM maana ule uliokuwa usalama wa taifa sasa ni wa CCM,polisi na majeshi ya ulinzi wanashindwaje kumtaja mmiliki wa dowans???! eti Slaa(Phd) ni kichaa! wao ndio vichaa na infact wanahitaji matibabu veri serious.
   
 6. m

  mzambia JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mwacheni baba yangu kikwete apumzike mbona mnamuandama baba?

  Tokea mjue uwezo wake ni mdogo basi tena kila kitu ni kumsingizia tu baba ziba masikio?
   
 7. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  kuna rafiki wa kaka yangu ambaye alisoma na JK kipindi hicho yaani baada ya jamaa kupata urais tu akasema Tz tumeumia nilikuwa sijui kwanini jamaa alisema hivyo ila sasa nimejua kuumbe ndio hivi. alisema jamaa JK si kiongozi mzuri nilikuwa sielewi kipindi kiile sasa naelewa.
   
Loading...