Kauli 5 za mwisho alizoandika Kalihose kuhusu Maisha na Kifo

Magoiga SN

Member
Oct 15, 2016
15
61
Peter Alijua Muda Wake Hapa Duniani Umetimia

Magoiga SN-Mwanza

i) Tarehe 31 Dec/Tanuru la Fikra : Aliandika 'Maisha haya ni mafupi sana na hatupaswi kufanya chuki kuwa sehemu kuu ya maisha yetu...TUSAMEHEANE kila wakati (matendo na maneno), leo 2016 na kesho 2017. Walionikwaza nimewasamehe WOTE'

ii) Tarehe 31Dec 2016 : Aliandika 'Maisha....Baada ya KUISHI (maisha) nini hufuata? (Kuna aliekwishafikiria kwamba maisha aliyoishi yanatosha)?'

iii) Tarehe 30 Dec/Tanuru la Fikra : Aliandika 'Tunapomaliza mwaka 2016...Tujiulize.....Je, tunaipenda TANZANIA au tunavipenda zaidi VYAMA VYETU?? Je, muhimu kwako ni UTANZANIA au ni UNYUMBU/UFISI/USIMBA wako? Mwaka 2017....Tuanze/tuendelee KUIPIGANIA [HASHTAG]#TANZANIA[/HASHTAG] au unyumbu/ufisi/usimba kama kawaida?? [HASHTAG]#TANZANIA[/HASHTAG], [HASHTAG]#MTANZANIA[/HASHTAG]. TIMIZA WAJIBU WAKO, toa maoni kisha tuamue kama Taifa....!!
(KUMBUKA KILA MAISHA YANA THAMANI YAKE KWA WAKATI WAKE NA BAADAE HUPISHA MAISHA MENGINE.....)'

iv) Tarehe 28 Dec 2016/Facebook : Aliandika 'Nobody is saying 2017 is my year...2016 humbled everyone. (Kwa tafsiri isiyo rasmi sana, Hakuna asemaye 2017 ni mwaka wangu, angalau 2016 ulimfaa kila mtu)'

v) Tarehe 11 Dec/Tanuru la Fikra: Aliandika 'Unapokuwa umekufa hujui chochote wala husikii maumivu, wale walio hai ndio hubeba maumivu ya kifo chako.'

#My_Take Ukizitafakari kauli hizo za Marehemu Peter Kalihose, utagundua kuwa wanaotumia kifo chake kama silaha ya kumhukumu au kumuadhibu kwa shughuli zake za kisiasa alizowahi kuzifanya akiwa hai hawajui wafanyalo. Kauli hizi ukizitafakari kwa makini utagundua kuwa, japo amelala mauti lakini bado kuna watu ambao kupitia kauli hizi tunaouona utoto wao.

R.I.P PETER KALIHOSE ~~Daima Tutakukumbuka

Magoiga SN
Mwenyekiti wa Muda-CCM Tawi la Mitandaoni
 
Wanadam kabla ya kusamehe yatufaa kuomba kusamehewa kwanza,ili uliowakosea wakupe afadhari ya moyo wako.
Hapo kwenye unyumbu na ufisi nadhani kiburi cha uzima kilikuwa bado kimetamalaki.

Hata hivyo RIP uhifadhiwe unapostahili Mimi ni mwanadam kama wewe siwezi kuchagulia Mungu pahala pa kukuhifadhi.
 
Wanadam kabla ya kusamehe yatufaa kuomba kusamehewa kwanza,ili uliowakosea wakupe afadhari ya moyo wako.
Hapo kwenye unyumbu na ufisi nadhani kiburi cha uzima kilikuwa bado kimetamalaki.

Hata hivyo RIP uhifadhiwe unapostahili Mimi ni mwanadam kama wewe siwezi kuchagulia Mungu pahala pa kukuhifadhi.
Muungwana huwa anaanza kuomba asamehewe yeye kwanza. Mbona hapa JF kuna sisiemu kindakindaki lakini si watovu wa adabu kiasi hicho? Nimemsamehe.
 
Back
Top Bottom