TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,747
Jana 6 machi 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli alimteua aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini India, Mhandisi John Willium Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Ombeni Sefue ambaye kwa mujibu wa Rais, atapangiwa kazi nyingine.
Ikumbukwe kuwa Ombeni Sefue alikuwa mteule wa Pili wa rais tangu aingie Madarakani hapo Movemba mwaka jana. Uteuzi wa Ombeni Sefue ulitanguliwa na ule wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche Masaju.
Mara tu baada ya operation Tumbua majipu ulipoanza maneno Mengi sana yalisemwa. Wapo waliosema rais anatumbua vijipu upele, wengine wakasema ni nguvu za soda na wengine wakasema rais anatumbua majipu huku akiishi na majipu mengine ikulu. Kwa wale waliozoea kufanyakazi kwa mazoea wataendelea kuamini anachokifanya Magufuli ni nguvu za soda, lakini kwa wenye kujitambua , hili la Ombeni Sefue ni la kututia hofu zaidi kuwa rais amedhamiria. Kama Katibu Mkuu Kiongozi aliyemteua yeye mwenyewe ameonekana kutojaa vizuri kwenye nafasi hiyo, MIMI, WEWE NA YULE TU AKINA NANI mpaka tufanye kazi kwa mazoea? Tuwe na ujanjaujanja katika kutekeleza majukumu yetu? Tubeze kazi inayofanywa na rais?.
Nilikuwa namuogopa sana rais na hii kasi yake. Kauli yake mbele ya Wakuu wenzake wa nchi za maziwa makuu kuwa atatumbua hata majipu yaliyoko nchi wa washirika wa Jumuiya ya Afrika mashariki na hili la Katibu Mkuu Kiongozi ni matukio ambayo pasi shaka yanatudhihirishia kuwa amedhamiria. Ni wakati wa Watendaji wa Umma na hata wasio wa Umma kujitathmini na kubadilika na kutanguliza uzalendo, uadilifu na uchapakazi ili kuendana na kasi ya mheshimiwa rais la sivyo huko mbeleni kuna kulia na kusaga meno. Ni wazi huyu rais hana rafiki, hakika yeye ni Kazi tu.