Katoliki kuwekeza zaidi katika elimu

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Kanisa katoliki nchini,limesema kamwe halitarudi nyuma kutumia rasilimali zake katika kuwekeza kwenye elimu kwa kujenga shule nyingi za sekondari ili kulisaidia taifa kuwa na vijana wengi wasomi.

Kauli hiyo ilimetolewa juzi jijini mwanza na rais wa baraza la maaskofu nchini(TEC)Jude Thadaeus Ruwaichi wakati alipo kuwa akizungumza kwenye mahafali ya 50 ya shule ya msingi Nyakahoja ya jijini mwanza. Kwa mujibu wa askofu Ruwaichi kanisa hilo lipo mstari wa mbele kupigania maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla,hivyo litaendelea kuwekeza kwa kujenga sekondari za wavulana na wasichana nchini.

Kanisa litatumia rasilimali zake kuwekeza sana kwenye sekta ya elimu kwa kujenga shule nyingi za sekondari,miaka 20 iliyopita tumejenga sana sekondari kwa wasichana.Kazi hii tutaendelea nayo kwa lengo moja tu la kusaidia nchi na vijana wetu katika kuwa na wasomi wenye elimu bora.

Ruwaichi ambaye pia ni askofu wa jimbo kuu la Mwanza ,alisema mwaka huu kanisa hilo litaanza kujenga shule ya sekondari ya wavulana jijini Mwanza.Hata hivyo Ruwaichi aliagiza mchakato wa ujenzi huo ufanyike haraka ikiwa ni pamoja na kuandaa mchoro wa shule hiyo.
 
Big up Askofu...... {utaona mabango tutaongozwa na ukatoliki hadi lini} Jibu ni mizizi imara wanayo itengeneza wenyewe
 
Hayo always ndiyo maono ya kanisa lolote!...Kupeleka mbinguni watu walioerevuka na kuachana na ujinga!...Lawama na maandamano ni kupoteza muda...

Imagine, watu wanaandamana kugombea eneo la ibada shuleni, while wengine wanawaza kujenga mashule na Long term Dev. plans zingine.
Hapa pana Dead-Line iliyo Clear kabisa, sijui kwanini inakuwa ngumu kuelewa!!...

Mkuu unataka kuniambia hata yesu hiyo nafasi hatokuwanayo! Yeye hajaenda shule ati!
 
hata kama wamesikia wataamua kuamini kuwa askofu ameipa amri serikali iongeze fungu la mou ili kanisa lijenge hizo shule! Subirini waje subscribers wa dhana fikirika ya mfumo kristo!
nimefurahi sana kuona kanisa linawekeza katika elimu tena kwa maendeleo ya vijana hapo hakuna kubagua lakini ngoja mpuuzi mmoja anaitwa malaria sugu aje kuchafua hali ya hewa twamsubiri kwa hamu ms
 
tunasonga mbele,huko kwetu bukoba kila mwaka matoke ya form 4 yanaanza hivi. 1.katoke seminary 2.Rubya seminary 3.HEKIMA Secondary(shule ya wasichana). Baada ya hizo shule katoriki zinafuata shule binafsi kama 4.peace secondary 5.karagwe secondary 6.kaisho secondary n.k mwisho shule chovu za serikali.. Kama mumwani,mugeza,bukoba sec.wanalitia aibu ata jina la kadlinari rugambwa iliyoko pale bukoba mjini.
 
Ingawa ni muislaam lakini nawapongeza kwa uamuzi huo. Lakin kwa ushauri tu kuliko kuongeza taasisi nyingine kwa nini wasizi improve existing ones. Quality ya education ya taasisi za kanisa zimekuwa quastionable. Muwe mnajali quality kuliko quantity.
 
Hapana...nilichokuwa namuelewesha rafiki yako MS ni kwamba... siyo swala tano wote wasafi...! Ni hicho tu!

Angalia ulivyokuwa na upeo mdogo kwa hiyo wewe MS ni adui yako sababu ni Muislam.

JF bana kuna mambwiga wengi sana mtu akiwa dini tofauti na wewe ni adui..kazi kweli kweli.
 
Angalia ulivyokuwa na upeo mdogo kwa hiyo wewe MS ni adui yako sababu ni Muislam.

JF bana kuna mambwiga wengi sana mtu akiwa dini tofauti na wewe ni adui..kazi kweli kweli.
Sijui kati yangu mimi na wewe ni nani ana upeo mdogo. Msingi wa mafundisho yetu ni UPENDO na siyo UADUI. Binafsi ninao ndugu wa damu wengi tu Waislam na wanaongezeka kila uchao. Unaweza kuniambia ni wapi nimesema MS ni adui yangu kwa sababu ni Muislam?
 
Thibitisha haya maneno yako kwanza.
Huu sasa ni utoto ... Hivi kwa kukuambia Malaria Sugu ni rafiki yako ndiko kunakokufanya uone mimi ni adui yake? Crap..! Kwaninini hujayahoji mabandiko yake(MS) yanayoonyesha chuki kubwa na uadui kwa ukristo ? Mimi simchukulii muislam kama ni adui yangu lakini wewe pamoja na wenzako mnawaona wakristo ni adui zenu...! Tuendelee na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom