Katika vita hii hakuna atakayepona ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika vita hii hakuna atakayepona ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jul 14, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimezunguka jana na leo karibu kila nilipotembelea nimesikiliza watu katika makundi kwa furaha au huzuni wakizungumza kuhusu dhana ya kujivua gamba kwa wanachama na viongozi wa CCM. Katika hili hakuna asiye na upande, wapo ambao wanashangilia kuwa kundi pinzani ndani ya chama limepoteza shina na mhimili wake kwa maana ya nguvu ya kifedha aliyonayo Bw. Rostam Aziz. Wapo wanaohuzunika kwa kuondokewa na msamaria mwema wa chama na wanachama wake. Wako wanaosema CCM kwisha habari yake. Wako wanaosema kuwa sasa chama kimeanza kufanikisha ajenda yake ya kujivua gamba na kwa hiyo tutarajie kuona umaarufu wa chama ukirejea kwa haraka kwa sababu waharibifu wake wataondoka mmoja baada mmoja.

  Si nia yangu kuunga mkono au kupingana na kundi lolote katika hayo ambayo maoni yake nimeyatoa kwa kifupi hapo juu, bali nataka kutoa tahadhari kwa wote na misimamo yao. Kwa maoni yangu vumbi ndiyo limeanza kutimka, bado tuna njia ndefu sana kuona kile ambacho tunakitegemea sasa.


  Kwa kifupi na kwa kurejerea maneno ya RA jana ni kwamba anahasira na watu ndani ya chama chake, anahasira na uongozi wa chama na anahasira na maoni ya watu kuwa yeye ni fisadi. Wananchi wa Igunga wanahasira na chama chao, wanahasira na uongozi wa juu wa chama chao, wanahasira na msimamo hasi wa watu wengine juu ya aliyekuwa Mbunge wao.

  Mimi siami na sifikirii kuwa ipo siku Rostam atakiasi chama chake, lakini pia siamini kuwa atakuwa na nafasi ya kuwazuia wanachama wa ccm jimboni kwake wenye mapenzi nae wasiasi na pengine huu ndio utashi wake ingawa ameahidi kuwa mwanachama mtiifu. CCM iliyopokea ajenda CDM kumchafua RA haiwezi kuthubutu kuimba wimbo wa utakatifu wa Rostam mbele ya wananchi wa Igunga, swali je Nnauye na timu yake ya kampeni watabeba ujumbe gani kwenda kumwombea mgombea wao kura kwa wananch wa Igunga. Kiungwana itabidi waimbe wimbo wa Jembe ni jembe maana yake waendelee kuwambia wananchi wa Igunga uchafu wa RA na pia wawe tayari kujibu maswali ya Wanaigunga kwa kile wananachodhani kuhusu Mbunge wao. Maswali yenyewe ni madogo lakini yatakuwa yamebeba ujumbe mzito nayo baadhi nahisi yatakuwa kama ifuatavyo nini hasa dhambi ya RA, kuhusu Richmond watauliza hivi yeye kwenda kuomba kazi serikalini kuna ubaya gani wakati serikali ilikuwa na nafasi ya kumjibu kuwa hatoshi kufanya kazi hiyo badala yake ikampa kwa nini kosa hili la serikali kushindwa kufanya maamuzi sahihi atupiwe RA? Mbona tunasikia hela za Kagoda zilifanya kazi ya kampeni ya Chama iweje leo kosa liwe na RA na mengineyo mengi.


  Kisiasa RA amejeruhiwa sana, lakini sasa kutoka kwake katika siasa ni mlima mkubwa kwa chama chake kuepuka kupata jeraha tena sehemu nyeti na ngumu kutibika hata kama daktari ni bingwa kwa sababu kuna uwezekano mwili kushindwa kuhimili tiba hiyo.

  Je huu ndio mwanzo wa kuporomoka kwa Chama Tawala, Je turufu ya CCM kuendelea kuwa chama chenye nguvu iko mikononi mwa watu ambao wanaitwa magamba na chama chenyewe? Je Rostam ataendelea kuwa adui wa watanzania na kuhesabika kama mkosaji au kujiondoa kwake katika siasa na majukumu nya kisiasa ni nafasi nzuri ya kuwafanya watanzania watafakari upya ili wamjue na pengine kumtetea kuwa yeye ni mwanakondoo tu katika siasa za ndani ya chama chao?


  CCM MNAYO KAZI NA PENGINE HUO MWELEKEO NDIO MUGUMU KULIKO MISUKOSUKO AMBAYO MUMEWAHI KUPATA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MIAKA ZAIDI YA 60 YA UHAI WA CHAMA.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,585
  Likes Received: 4,693
  Trophy Points: 280
  We waache tu wajishebedue kuwa sasa kazi imeanza, itakula kwao, kwani ni usanii tu unaendelea,vinginevyo ikifanyika hiyo kazi kama inavyopasa kufanyika mbona CCM ndiyo mwisho, ugali umwagwe kweli kuna mtu atapona? Majeruhi wa kwanza ni Jakaya Mrisho Kikwete (GAMBA KUU)
   
 3. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,570
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Daah, asante sna mtoa hoja unadeserve jins ulvoufafanua hoja ya rostam!I'm satisfied enough, ki ukwel mim cna ugomv na hao mapacha wa3 kama weng wanavotaka kuamin hvo!Kama ni swala la gamba basi niseme typically CCM as whole must caryout zic BURDEN!
   
 4. N

  Ngolengosha New Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubali kabisa, lakini kilichonishangaza hawa ndugu zetu wa Igunga kwa kumwaga Mashozi hadharani, kwa kweli nimesikitika sana pale watu wanapoamini hakuna mtu mwingine atakayeleta mambo mapya hii ni hatari sana, huruma yetu ndiyo inafanya maisha ya MTz yanazidi kuwa magumu kwa kuwakumbatia wezi wa mali za umma, lazima sasa wanainchi wachukue maamuzi magumu ya kuwatosa kabsa mafisadi wote. Mungu Ibariki TZ
   
 5. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Duh!! Hii Game ndo inaanza kuwa tamu vile!!!!!! Tatizo magamba yamekuwa magumu kiasi cha kuziba masikio na ubongo. Ndo maana ukaambiwa Mbunge mmoja wa CHADEM ni sawa na wa CCM 70 kwa fikra, sasa hivi kila wakifanya hiki, hawana pa kutokea. Kazi ni Kwao sisi yetu macho
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Acha CCM life tu .Wanafiki sana wanasema pembeni lakini wakiwa katikati hata JK hawezi kutamka fulani fisani pamoja na kumiliki vyombo vyote ya intel .Acha waumizane wake pembeni tukuchue nchi yetu .
   
 7. WANALIZOMBE

  WANALIZOMBE Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi nashangaa wana igunga kwa kuanguankilio kwakumlilia GAMBA, washindwe, chamsingi huyu gamba akomaliwe alrudishe pesa ya inchi yetu aliyo kwiba
   
 8. c

  chimwaga Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Arafu isitoshe wana igunga now wata kuwa na imani na kambi ya upinzani coz ndio walio sababisha Rostam aji uzuru nyasifa zote so through this imani kwa upizani ime ongezeka. kwa kweli kazi ime anza.
   
Loading...