Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Katika siku za karibuni kumetokea sintofahamu kubwa kuhusu POSHO za madiwani Jiji la Arusha.Na kwamba zimeuziwa wakati sio kweli....
Huu ndio ukweli...
Posho ya kikao kimoja katika Halimashauri ya Jiji la Arusha ni laki moja kwa kikao,posho hii imeanza kulipwa 2008(nilikuwa shuleni)enzi hizo Halimashauri ilikuwa chini ya ccm,kabla ya hapo posho ilikuwa 80,000.Kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za Halimashauri posho hii ilipitishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu. Posho ya laki imelipwa kwa miaka nane mfufulizo na kamwe haijawahi kuwa hoja licha ya Halimashauri kufanyiwa special audit.
Mimi Ephata Nanyaro nimechaguliwa rasmi 2010 na kukuta kiwango hiki na kipindi hiki tangu 2010 hadi 2015 CHADEMA tulikuwa na mgogoro wa umeya,hivyo hatukuingia vikao vingi binafsi nilishiriki vikao 22 tu kwa miaka mitano kati ya hivo nililipwa vikao 10 tu yaani 100,000x10=1,000,000(milion moja ya kitanzania)
2015 nimechaguliwa tena na this time ni mjumbe wa kamati ya fedha na utawala kamati ambayo hukutana kila mwezi.Tangu tumechaguliwa na halimashauri imekuwa ya CHADEMA tuna miezi nane na vikao vya baraza (full council) vimekaa mara nne
1.Baraza la kuapishwa(Kikao cha kwanza)
2.Baraza maalum la bajeti 2016/17
3.Baraza la kawaida
4.Baraza la kujibu hoja za CAG
Kuna vikao vya kamati mbalimbali na binafsi nimekaa mara 7 kwenye kamati ya fedha ambayo inakutana kila mwezi ndio kusema 100,000x7=700,000 pamoja na baraza 100,000x4=400,000
400,000+700,000=1100,000(milioni moja na laki moja)
Kwa kuwa hii posho ambayo tumeikuta imekuwa NONGWA kwa makada wa ccm na watu wengine wenye umbumbu wa sheria na kanuni,na kwa kuwa CHADEMA kwenye ilani zake zote 2010 na 2015 imekuwa ikiitaka serikali kuondoa posho ya kitako na kwa kuwa Tangu 2008 kuna waliolipwa na kwa kuwa Katibu mkuu Tamisemi ameandika barua akitaka ufafanuzi wa posho hizi na kwa kuwa amekubali kupotoshwa kuwa madiwani wanajilipa wakati sio kweli tunajilipa bali tunalipwa naitaka serikali ifanye yafuatayo;
1.Bunge la Jamhuri ya Muungano lishitakiwe maana ndio limepitisha hii bajeti ikiwa na posho ndani yake,walipitisha kifungu kwa kifungu,kwa mujibu wa katiba bunge ndio hupitisha mapato na matumizi ya serikali
2.Walionufaika na hizi posho tangu 2008 waziriejeshe madiwani waliokuwapo na sisi tutakuwa tayari
3.Tamisemi iondoe posho kabisa kwa madiwani wote nchi nzima kama hizi posho ni haramu
Mimi Ephata Nanyaro nipo tayari kurejesha posho hizi kama ni haramu yaani posho ya milioni moja ya 2010-2015 na milioni moja na laki moja ya 2016Jumla 2,100,000,ithibitishwe kuwa ni haramu na sisi tutawajibika.
Chanzo: Ephata Nanyaro (Diwani wa Kata ya Levolosi Jijini Arusha)