Katika safari yangu, nilichokiona maeneo ya Pwani kinasikitisha

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,164
Wadau,

Katika mizunguko yangu ya kikazi kuna kitu nilikuwa nakiangalia hasa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Huu ni msimu wa kilimo, wakati nikiwa kwenye gari kuanzia kanda ya ziwa hadi Morogoro nimeona kuna pilikapilika nyingi za kilimo. Yaani kuanzia kanda ya Ziwa inaonekana green ya mahindi na mazao mengine.

Lakini maajabu ni kwamba wakati nikitokea Dar es salaam kuelekea Arusha, kuanzia Mlandizi karibu mto Ruvu hadi Segera, kila nikitizama kwenye vijiji vya pembeni nimekuwa nikiona green ya mapori tu.

Ukweli nimejiuliza sana, kwanini naona green ya mapori badala ya Mazao wakati huu ni msimu wa kilimo, au eneo hili ni hifadhi ya taifa? Nikajiuliza, hawa watu hawalimi, lakini pia hawafugi, je wanaishije?.

Lakini maajabu mengine ni kwamba eneo lote hili hasa Chalinze hadi Segera, nyumba asilimia kubwa ni za fito na tope (Mbavu za mbwa tunaita), yaani unakuta nyumba mbavu za mbwa iko katikati ya kijani cha pori lakini hakuna mazao wala maandalizi kwa ajili ya kilimo licha ya kwamba ni msimu wa mvua. Vijiji hivi vina umasikini wa kutupa, utajua kwa kutizama mbavu za mbwa zilizopo.

Ndugu zangu, vijana wenzangu mnaoishi maeneo hayo, mnarudisha taifa nyuma, kwanini hamtaki kutumia ukaribu wenu na Dar es salaam mkauza mazao mkabadilisha hali zenu za maisha? Kwanini wakulima wa Songea wanufaike na uuzaji wa mahindi Dar na nyie msitumie fursa ya ukaribu huo? Kwa tabia hii nina uhakika kila mwaka huwa mnaletewa mahindi ya njaa kutoka serikalini.

Nashauri, itungwe sheria ya kulazimisha watu kufanya kazi. Pia wabunge wa maeneo haya, hasa Ridhiwani na wengine, tafadhali hamasisha watu wako kufanya kazi.
 
Mkuu inawezekana ni kweli, lakini ni lini umewahi kusikia hiyo Mikoa unayoiita ya Pwani ambayo ni ya Watu wavivu imekumbwa na uhaba wa Chakula kiasi cha kula Wadudu au kuhitaji Msaada wa Chakula Serikalini ukilinganisha na hiyo Mikoa ambayo wamefyeka Mapori yote kwa ajili ya shughuli za Kilimo?
 
Chalinze wanalima mananasi na wanalisha Afrika Mashariki nzima. Na pia jiografia inatofautiana kuna mikoa inamea zaidi Mahindi mfano (the great five) na kuna mikoa inamea Zaidi mazao mengine hivyo pamoja na mvua kunyesha sehemu ulizotaja hazimei mahindi.

Ni sawa na kwenda kupanda mikahawa pembeni ya bahari haiwezi kumea pale unamea mnazi na mikoko.
 
Hata human rights ya kidato cha nne inajua kua kumlazimisha mtu kufanya kazi ni kuingilia haki yake ya kibinadamu.

Pia kama watu wapo, hawalimi hawafugi, ila hawajawahi kutaka chakula cha serikali kama Singida na mikoa mingine basi kuna shughuli wanafanya. Pengine wenzako ni wavuvi.

Au labda milioni 50 za kila kijiji zinawapa jeuri.
 
Mkuu ulichokisema ni kweli kuwa hayo maeneo hayajalimwa na yana mapori ya kutosha tu, lakini ngoja nikusahihishe kwanza;

Tanga ndio mkoa unaoongoza kwa ulimaji wa machungwa na hawapo nyuma kwenye ulimaji wa kabichi. Pia usiongee kuhusu minazi na miembe hata mahindi wanalima mno expecially wilaya hiyo ya Muheza..

Lakini ngoja nikwambie jambo; watu huwa hawalimi tu kiholela, huwa wanaangalia ardhi yenye tija kirutuba na uwepo wa mabonde ya maji. Na waweza kupita sehemu ukaona kuwa kuna pori ama msitu mkubwa mnooo kwa upande uliopo kumbe katikati ya msitu kuna kuwa na kijiji cha watu wanaishi hapo na kuendesha maisha yao kwa hizo hizo shughuli ambazo wewe umezitilia shaka.

Kupita kwako ndani ya gari pasipo kushuka na kufanya tafiti haitoshi kuamini kile ulichokuja kutuwasilishia hapa...
 
Back
Top Bottom